......Akiwasalimia wachezaji wa Moro Youth
Kocha Mkuu wa Uluguru Ally Jangalu akikabidhwa fomu na mchezaji wake
Kikosi cha Moro Youth
Kikosi cha Uluguru
Mwamuzi akimkagua mchezaji wa Moro Youth aliyeumia
Heka heka uwanjani
Mtifuano Mkali beki wa Moro Youth Hamza Ally akimdhibiti winga wa Uluguru Juma lssa asilete madhara gorini kwake
Kufungwa ni Noma Moja haika mbili haikai, kocha wa Uluguru Ally Jangali akianglia saa wakati tiimu yake ikiwa nyumba kw abao 2-0, kulia ni wasaidizi wake Kocha wa makipa Bure Mtagwa, Kocha Msaidizi Mohamed Mtono, na Meneja wa timu Hamis Malifedha. Wote hao waliwahi kuitumikia Reli ya Morogoro
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Moro Youth imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya shirikisho Maarufu CRDB Bank Federetion Cup Wilaya ya Morogoro msimu huu wa 24-25.
Vijana hao wa Moro ambayo ni kikosi cha pili cha timu ya Moro Kids inayoshiriki ligi daraja la Pili Tanzania [SDL], imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuinyuka timu ngumu ya Uluguru Mountain Academy kwenye mchezo wa fainali uliopigwa juzi Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa.
Toka gemu hiyo inaanza Vijana wa Kiluguru waliwakimbiza vilivyo Vijana wa Moro, muda wote wakiwa kwenyye lango lao wakisaka bao. Juhudi hizo waluguru ziligonga mwamba dakika 27 baada ya Winga wa Moro Youth Benson Kenedy kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Hassan Coaster na kumpita kipa wa Uluguru Poul Simon.
Wakati mali ikielekea kuzama gorini beki Luqman Juma alichupa kama nyani na kuunyaka mpira huo, Mwamuzi aliamua Mkwaju wa penality na kumtoa nje kwa kumzawaidia Umeme’kadi njekundu’.
Kufuatia adhabu hizo mbili kwa mpigo tena za mwanzoni kabisa mwa mchezo ziliwanyong’onyesha Vijana wa Kiluguru na kujikuta wakipachikwa bao la pili dakika ya 78.
Baada ya kunyakua Ubingwa wa Ligi hiyo iliyoshirikisha timu 16 Moro Youth kutoka kwenye Academy Maarufu nchini ya Moro Kids walikabidhiwa Kombe pesa 250,000.
Uluguru Academy inayomilikiwa na wachezaji nyota wa zamani, John Simkoko mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Uluguru Mountain, Hussein Ngurungu Mwenyekiti, Ally Jangalu kocha Mkuu wa taasisi, Mohamed Mtono Kocha Msaidizi na Bure Mtagwa Kocha wa Makipa, wao waliambulia kifuta jasho cha lakini Moja na nusu.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo alikuwa Mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro [MDFA] Mh Selestin Mbilinyi.
Mara baada Mh Mbilinyi kunyakua uwenyekiti huo takribani miezi 5 iliyopita Wilaya ya Morogoro imepiga hatua kubwa kisoka chini ya Uongozi wake Moro Kids imefanikiwa kupanda daraja la pili.
Kwa mafanikio hayo baadhi ya watu waliibuka na kutafuta kanuni za kumuodoa madarakani Mhe Mbilinyi ambaye pia ni diwani wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Siko zote Mungu husimani upande wa mwenye haki hivyo licha ya nguvu kubwa kutumika za kutaka kumng’oa Mh Mbilinyi Mungu alikuwa upande wake na mwisho wa siku watu hao waliferi.
Kwa sasa Mhe Mbilinyi ambaye pia ni diwani wa Kata ya Lukobe ‘Kipenzi cha Wana Lukobe’ anaendelea kukalia kiti hicho kwa mamlaka ya Mungu na wajumbe wa mkutano Mkuu wa MDFAwalimchangua kihalali.
PIchani Mhe Mbilinyi akikagua timu ya Uluguru Mountain.
Picha no 2 Mh Mbilinyi akimkabidhi kombe la Ubingwa Nahodha wa Moro Youth Kondo Maulid.
Angalia picha za Matukio mbali mbali ya fainali hiyo kwenye profaili na Mtandao huu.
No comments:
Post a Comment