Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 7, 2024

BAADA YA MISUKO SUKO MINGI HATIMAYE MAPENZI YA MUNGU YAMETIMIA DADA DIDA


                      Warda Makongwa akiingia ukumbini

                        ...Warda akimtambulisha Dida.      
                                    Gazeti la ljumaa Wikienda


 

.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KAMA ilivyo kwa binadamu wengi hupitia misuko suko katika maisha, baadhi ya watu wanapokumbana na misuko suko hiyo hukimbilia kwa waganga wa kienyeji, lakini kwa Khadija Shahibu Maarufu Dida yeye alipokutana na misuko suko alimbilia kwa mwenyezi Mungu. 
 
Hii inathibitishwa na Mwandishi wa habari hizi Julai 2017, Dida aliyekuwa Mtangazaji wa Time Fm wakati huo kabla ya kutimkia Wasafi Fm, akiwa safari kutoka Dar kuja Moro kushiriki Birthday ya Mdogo wake Warda Makongwa alinusurika Kifo baada ya kupata ajali eneo la Mayesu Mikese. 
 
Kufuatia tukio hilo Dida alipofika Morogoro baada ya kutamatikati kwa Birthday hiyo siku iliyofuata alisoma dua ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru na Kifo kwenye ajali hiyo. 
 
Kwenye dua hiyo iliyosomwa na Shehe Masenga Dida alimwalika Mwandishi wa habari hizi kushiriki lbada hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Warda ambaye pia ni Mtangazaji Maarufu wa Planet Fm ya Mkoa Morogoro.akikitendea haki kipindi cha Mcharuka wa Pwani.
Baada ya kukamilika kwa dua hiyo Dida alitoa sadaka ya Chakucha kwa watu mbali mbali walishiriki lbada hiyo iliyoriotiwa kwenye gazeti la ljumaa wikienda na Mwandishi Dustan Shekidele.
Kipekee nichukua fursa hii kumpa Pole Madam Warda kwa kuondokewa na dada yake Mpendwa, nashukuru kwenye shughuri zako zote ulinialika na kunipa kazi ya kupiga picha matukio yote.
Mara zote kwenye shughuri za Warda, Dida hajawahi kukosa, alichoma mafuta kwenye gari na kuja Moro kumsapoti Mdogo wake.
Watu wengi ni mashahidi ikifika kipengele cha zawadi Dida alifungua pochini na kukumwagia minoti iliyofunuiansakafu.
Dida hakuishia hapo nakumbuka kwenye moja ya shughuri zako alikupa ofa ya kukupeleka China kukufanyia Shoping ya maana.
Mara nyingi baada ya shughuri kukamilika Dida ulikuwa ukinitania “Shekidele mkude Simba leo umenasa umbea gani kwenye sherehe ya Mdogo wangu”.? 
 
Ama kwa hakika Dida tabasamu lako na ucheshi wako tutaukumbuka daima.
 
Nenda mambanaji tataonana badae. 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...