Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WANACHAMA wa Simba tawi la Mawenzi Mkoani Morogoro, wamefunguka mazito kasoro zilizojitokeza kwenye mkutana mkuu wa timu hiyo uliofanyika jumapili iliyopita ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi mara baada ya kurejea mkoani Morogoro Mwenyekiti wa tawi la Mawenzi Yakshan Kidati na mwanachama wake Jonas Nyaki kwa pamoja walionyesha kufurahishwa na hotuba ya Mwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji’MO’huku wakikosoa Katiba ya bodi ya wadhamini wa Klabu hiyo kuchapishwa kwa Lugha ya Kingereza ambayo wanachama wengi hawaifahamu.
“Mkutano ulienda vizuri kama ulivyoshuhudia kwenye Tv, mara baada ya mkutano kutamatika majira ya saa 6 na nusu mchana tuliingia kwenye gari yetu tuliyokodi tumefika Morogoro majira ya saa 11 jioni.
Tumevutiwa sana na maneno ya faraja na Tumaini yaliyotolewa na mwekezaji wetu Mo Dewji, lakini watu wengu tumekoa hatua ya Katiba ya bodi ya Wadhamini wa Klabu kuchapishwa kwa Kiingereza ambacho wanachama wetu hawakifahamu ”alisema Mwenyekiti huyo.
Alipoulizwa kwa mantiki hiyo hawakuipitisha katiba hiyo kwa kutojua kilichoandikwa? Alijibu.
“BMT waliagiza awepo mtu wa kutafsiri kutoka Kiingereza kuja kuswahiri, kwa sababu tunataka jambo letu liinde tumeipitisha Katiba hiyo licha ya uwepo wa mapungufu hayo ya Lugha.” Mwandishi. Ok hongereni kwa kazi nzuri mlioifanya ya kuipitisha Katiba hiyo swali la mwisho ambalo ni la kizushi.
Kwenye Tv nilishuhudia wanachama wote mmekabidhiwa zawadi iliyofichwa kwenye kasha je ndani mlikuwa na kitu gani?
Mwenyekiti. Shekidele Bwana any way kweli tulipewa zawadi na tulipofika nyumbani na kufungua kulikuta jezi ya Simba na Khanga pisi tatu.
Mwandishi. Asante sana mwenyekiti kwa ushirikiano siku nikihitaji ufafanuzi wa jambo lingine nitakupigia simu au nitafika hapa tawini.
Mwenyekiti. Sawa karibu sana unyamani shekidele.
Kwa upande wake Nyaki pichani nje ya tawi naye alionyesha kuchukizwa na Katiba ya bodi ya wadhamini kuchapishwa kwa Lunga za kigeni.
“ Nashangaa asilimia 99 ya wanachama tuliokuwepo ukumbini tunajua lugha ya Kiswahiri kwa nini mambo yetu ya maamuzi yachapishwe kwa Lugha tusiyoifahamu?.
Copy ya Katiba hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza nimekuja nayo iko nyumbani ukitaka kesho nikuletee uione”alisema Nyaki huku akiangua kicheko kama anavyoonekana pichani.
No comments:
Post a Comment