Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 2, 2024

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. PREZDAA BAND YA WALUGURU OG AMKUBALI JULIANA MGELA.





 


Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mmiliki wa band ya Waluguru Original Deogratius Aruphonce Almaarufu Killer Boy ameukubali Mziki wa Mwimbaji wake mpya wa kike Juliana Mgela aliyejiunga na Bend hiyo akitokea Bend ya Maisha Mapya pia ya Mkoani Morogoro.

Akihojiwa na Mlala Nje kuhusiana na ‘Parfomans’ ya Mwanadada huyo ndani ya band hiyo Killer Boy Mluguru Og kutoka Mkuyuni Matombo Wilaya ya MorogoroVijijini alisema.

“ Mlala Nje Shekidele kiukweli sikutegemea kama Jully anauwezo mkubwa wa kuimba kwa siku za hivi karibuni  amejizolea mashabiki kibao kutokana na sauti yake tamu anapoimba” alisema Killer Boy.

Siku za nyuma Mlala Nje aliwahi kuripoti kwamba Jully anauwezo wa kuimba pekee lakini kwenye kipengele cha kunengua bado anajitafuta.

Kauli hiyo ni kama imemuamsha kwani ljumaa iliyopita Mlala Nje alimshuhudia Jully mwenye kikoti cheusi [Kati] akionyesha umahiri wake wa kunengua sambamba na wanenguaji wengine wa bandi hiyo.

Wakati Mlala Nje akiwa bize kupiga picha tukio hilo Juliana alicheza huku akimkodolea jicho  Mlala Nje.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...