Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, August 31, 2024

MAUZA UZA YA AJALI.


Chuma imeingia kwenye Mtaro ndani ya kituo cha Mafuta Msamvu
....Wasamalia wema wakihangaika kuitoa kwenye Ngema
 


Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

Gari ndogo yenye namba za Usajairi T 902 EDZ imeacha njia na kuingia kwenye mtaro ndani ya kituo cha mafuta[Sheli]iliyoo jirani na Stend ya Mabasi  Msamvu kando kando ya barabara kuu ya Morogoro- Dar es salaam.

Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘Live’ bila chenga na Mwandishi wa Mtandao huu limetokea jana mchana ndani ya kituo hicho.

Wakizungumza na Mtandao huu mashuhuda wa tukio hilo walisema” Haya ni mauza uza gari hili jipya limetoka kwenye barabara  kuu ya Moro-Dar yenye msongamano Mkubwa wa magari, chaajabu huko halikutumbukia kwenye Mtaro. lilipoingia eneo hili la Sheli ambalo halina msongamano wowote wa magari limetumbukia kwenye hii ngema”alisema shuhuda huyo na kuongeza

“Tunashukulu  hakuna mtu aliyejeruhiwa ingawa gari limehalibikika kidogo muda huu dereva wa gari hili amekodi hilo Lori kama unavyoshuhudia tunahangaika kulivuta ili litokea kwenye hii ngema”alimalizia kusema shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Mbago. Naye Joseh Damas aliohojiwa alisema” Haya sio mauza uza wala nini kama alivyosema huyu mwenzangu ninachoona mimi huyu dereva alivyokuwa batabra kuu alikuw amakini alipoingia kwenye eneo hili la sheli kapunguza umakini huenda alikuwa akichezea simu kajikuta kaingia mataroni,  kwenye ukweli lazima tuseme ukweli”alisema shuhuda huyo kwa hisia kali

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...