lundo la mashabiki wakifuatilia fainali hiyo huku baadahi wakiketi kwenye makaburi yaliyopo jirani na uwanja huo.
Kocha Ally Jangalu akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu.
Mhe
Mbilinyi aliyeasama mdomo akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kutamatika kwa fainali hiyo.
....Wamuzi wakivishwa medaniMgeni rasmi akimkabidhi wa kombe la Ubingwa Nahodha wa MOTASOA
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MWENYEKITI wa Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro Mh Selestini Mbilinyia, ametoa Ufafanuzi kuhusiana na Ligi daraja la Nne Wilaya ya Morogoro kuhamishiwa Uwanja wa Wazi wa kilakala Makaburini kutoka uwanja wa ndani ya CCM Saba Saba ambao mashabiki walikuwa wakiingia kwa kiingilio cha shilingi elfu Moja.
Ligi hiyo inayosimamiwa pia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ilipofika patamu hatua ya robo fainali ilihamishwa kutoka uwanja huo wa Saba saba na kwenda uwanja wa wazi wa Kilakala, hali iliyozua maswali mengi kwa wadau wa Soka Wilaya ya Morogoro.
Wakihoji ligi hiyo kuhamishwa kutoka uwanja unaoingiza mapato na kwenda uwanja wawazi ambao mashabiki hawalipi kiingilio.
Kufuatia hali hiyo asubuhi ya leo Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Mwenyekiti wa Chama hicho Mh Mbilinyi na kumulizwa swali hilo na kutoa majibu haya.
”Kwanza nikushukuru sana Shekidele kwa kazi nzuri unayoifanya kwa kuripoti ligi yetu kwenye mtandao wako nimeona umeposti picha nyingi za fainali yetu asante sana kwa sapoti yako.
Nirejee kwenye swali lako la msingi ni kweli awari ligi yetu tulicheza uwanja wa ndani wa Saba saba na ilipofika hatua za mwisho mwisho tukahamia Kilakala.
Kwenye hili hatukuangalia mapato tumeangalia kuusambaza mpira wetu kwenye kata za Wilaya ya Morogoro kama unavyojua TFF walitupa maelekezo kwamba ligi daraja la Nne icheze na vijana wenye umri chini ya miaka 20’Under 20’ kwa lengo la kuibua vipaji”alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza.
“Hivyo kupeleka ligi hiyo mtaani tumetoa nafasi kwa wazazi kuangalia vipaji vya watoto wao lkumbukwe kwa umri huo wa miaka chini ya 20 vijana wengi bado wanaishi kwa wazazi wao”alisema Mhe Mbilinyia ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Lukobe kwa leseni ya CCM.
Mh Mbilinyi alimemalizia kwa kusema ligi hiyo iliyidhaminiwa na Dkt Simba imekuwa na mafanikio makubwa kwenye Wilaya yao.
“Kwa miaka ya hivi karibuni huenda hakuna ligi yoyote Tanzania ya daraja la Nne ambayo washindi wamevishwa Medani umeshuhudia mshindi wa Kwanza mshindi wa pili na waamuzi wote tumewavisha medani hii haijawahi kutokea kwenye Wilaya yetu ya Morogoro kwa miaka ya hivi karibuni”alisema Mh Mbilinyi.
Kwenye mchezo huo wa fainali uliozikutanisha timu za Morogoro Tanzanite Soka Academy[MOTASOA] na Zuia Fc ya Lukobe kutamatika kwa MOTASOA kunyakua Ubingwa baada ya kuitandika Zuia Fc bao 2-1 Mtandao huu uliwashuhudia kina Mama wengi wakiwapiga picha watoto wao kwa kutumia kamera za simu zao.
Fainali hiyo pia ilishuhidiwa na kocha Maarufu nchini Ally Jangalu[Pichani aliyeshika Pikipiki ya Boxer] ambaye mara ya mwisho aliifundisha timu ya Kagera Sugar ya Wilayani Bukoba Mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment