Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, August 8, 2024

MOTASOA YATWAA UCHAMPIONI LIGI DARAJA LA NNE WILAYA YA MORO.

Mwamba alijaribu kufunga kwa Tick taka bila mafanikio

Fainali hiyo ilinogeshwa na burudani ya Mnanda kutoka kwa kundi la Mwermbesongo ambapo Mc Monja pichani alinogesha vilivyo fainali hiyo kwa vionjo vyake vya muziki wa Uswazi




Beki wa MOTASOA Yoel Simon akimkata mtama winga wa Zuia Fc Domonick Mihambo nje kidogo ya boksi.

 Mwamuzi wa mchezo huo Ustadh Shabani Juma aliamuru iwe faulo kuelekea lango la MOTASOA.

Mwamuzi huyo ambaye ni Mwalimu wa Madrassa ya Msikiti wa Awayya Mawenzi akiwaelekeza  mabeki wa MOTASOA Sehemu ya kuweka ukuta.






Kipa wa MOTASOA akinyaka mpira kama nyama, Mlinda mlango huyo  alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya Zuia Fc


Waamuzi wa fainali hiyo  wakiongozwa na Ustadhi Shabani Juma[mbwenye mpira kwapani] wakivishwa medani na mgeni rasmi

Timu ya Burkina faso wanakisiki cha Mpingo walifanikiwa kunyakua nafasi ya Tatu ya ligi hiyo. PIchani Kiongoizi wa timu hiyo Mr Kudula akipokea zawadi hiyo ya mshindi wa tatu

Makamu mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Moroigoro Mh Geofrey Ng'itu kulia akimkabidhi bahasha ya pesa Nahodha wa timu ya Zuia ya Lukoba baada ya timu hiyo kunyakua nafasi ya pili.

lkumbukwe Mhe Ng'itu  ni Hakimu Mwandamizi wa moja ya Mahakama za Mkoa wa Morogoro





 

 

   Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Morogoro Tanzanite Soka Academy[MOTASOA] inayofundishwa na Kocha Hussein Mau imefanikiwa kutwaa ubigwa wa Ligi daraja la Nne Wilaya ya Morogoro msimu wa 2023-24. 

MOTASOA yenye Maskani yake eneo la Kikundi Kata ya Sultan Area Mkoani hapa,imenyakua Uchampion huo  baada ya kuichapa timu ya Zuia Fc kutoka Kata ya Lukobe kwa bao 2-1. 

Mchezo huo wa  ligi hiyo ulioshirikisha  wachezaji wenye umri chini ya Miaka 20’ Under 20’ umepigwa Julai 31 kwenye uwanja wa wazi wa Kilakala.

Awali Ligi hiyo namba 6 kwa ukubwa Tanzania Bara   ilichezwa uwanja wa ndani wa CCM Saba saba kwa kiingilio cha buku moja.

Ligi hiyo ilipofika patamu hatua za mwisho mwisho ilihamishiwa  uwanja huo wa Kilakala.

Ili kujua sababu za kuhamishwa kwa Ligi hiyo baada ya Mchezo huo wa fainali kutamatika Mwandishi wa habari hizi  alimfuata Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro  Mh.Selestini Mbilinyi ambaye alisema.

” Shekidele naomba nisubiri dakika 5 niende pale kwenye gari kuna watu wananisubiri nakuja tuzungumze”

” Chaajabu baada ya kumaliza mazungumzo na watu hao  Mh Mbilinyi ambaye pia ni  Diwani wa Kata ya Lukobe aliingia kwenye gari na kuondoka zake.

Juhudi za Kumtafuta ili kupataufafanuzi wa jambo hilo zinaendelea, hivyo  endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Ifahamike Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania linasimamia Ligi 6, Ligi Kuu,Ligi ya shirikisho Maarufu’CRDB CUP’ Ligi daraja la kwanza, Ligi daraja la Pili, Ligi Daraja la Tatu na Ligi daraja la Nne.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...