Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 17, 2024

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. MWANAMUZIKI MWINGINE WALUGURU OG ATIMKIA MAISHA MAPYA. KILLEY BOY AFUNGUKA.

Sebondo akicharaza Drum za Maisha Mapya ndani ya Ukumbi wa Rose Garden

Jushua Malekela kulia mwenye flana ya damu ya rangi ya damu ya Mzee wakiwaongoza vijana wake kulishambulia jukwaa hilo wakichagiza na Utamu wa Drum za Sebondo.
lkumbukwe kwenye Sebene Utamu upo kwenye Dram na kwenye Taarab Utamu upo kwenye Kinanda.


 

                      Na Mlala Nje Dustan Shekidele,Morogoro. 
 
MWANAMUZI Mwingine wa Band ya Waluguru Original ‘Wazee wa Ubaya Ubwela’ Kelvin Katilingi ‘Maarufu Sayona Sebondo’ Mwishoni mwa wiki amejiunga na Band ya Maisha Mapya ‘Wazee wa Fullu Vipaji’. 
 
Kama kawa Wiki end iliyoita Mlala Nje alitinga kwenye shoo ya Maisha Mpya ndani ya Ukumbi wa Rose Garden uliopo pande za Mafiga Mkoani hapa na kumshuhudia Mwanamuzki huyo akicharaza Drum za Band ya hiyo huku akizipa kisogo Drum za Band Pendwa ya Waluguru Og. 
 
Mlala Nje alimfuata Sebondo na kumuliza kulikoni amezikacha Drum za Waluguru na kuzicharaza bakora Drum za Maisha Mpya majibu yake haya hapa.
 
“Maisha Popote Shekidele kweli kwa miaka Mingi nilikuwa Waluguru Og kwa sasa nimeamua kubadiri Upepo nimekuja Maisha Mapya ambayo pia ni Band kubwa hapa Morogoro kama ilivyo Waluguru”
 
Alipoulizwa je ameondoa kwa shari au kwa heri?
 
Alijibu.
“Sina tatizo lolote na Waluguru nimeondoka kwa heri kama nilivyo kueleza awari sababu kuu ni ishu ya kubadiri upepo wa kimaisha.”
Hivi karibuni Mlala Nje aliriripoti habari za Mwanamuzi mwingine wa Waluguru Og Amina Remmy kujiunga na Maisha Mapya, huku Waluguru nao wakijibu mapigo kwa kumnyakua Juliana Mgella kutoka Maisha Mapya. 
 
Kufuatia hali hiyo Leo asubuhi Mlala nje akiwa chumba cha habari alimtwangia simu Mmiliki wa Band ya Waluguru Og Deogratius Arophonce, Almaarufu ‘Killer Boy’ na kumuliza kulikoni wanamuziki wake wengi wanatimkia Maisha Mapya?
Majibu yake haya hapa.
 
”Shekidele wewe unanijua vizuri toka nilipoanza muziki mwaka 2002 band ya Tushikamane iliyokuwa ikimilikiwa na wazungu pale Kilakala, Baadae nikaja band ya Levent Music iliyokuwa ikimilikiwa na hayati Eng Mzee Charles Madinda. 
 
Kwa sasa Mungu kanijalia nimepata vyombo vilivyoniwezesha kuanzisha hii band yangu ya Waluguru. 
 
Uongozi wa Band zote mbili kwa maana ya wale wazungu na Mhandisi Madinda walinihusia nidhamu kazini nakumbuka nikiwa Levent Mzee Bichuka wa Sikinde alikuja kwenye shoo wetu pale ukumbi wa DDC Nunge uliokuwa pia ukimilikiwa na Mzee Madinga na kutueleza wanamuziki kuacha kunywa pombe wakati wa kazi”alisema Killer Boy na kuongeza. 
 
“Mungu ni mwema nimeishi kwenye misingi hiyo ya nidhamu kazini wanamuziki wangu wote kabla ya kumwingiza kwenye band sharti kuu ninalompa nidhamu kanzini akikiuka namtimia kazi.
Hao wanamuziki ulionitajia sio kwamba wamehama nimewafukuza kwa tabia zao za ulevi kazini tuko jukwaani mtu anafanywa pombe mashabiki wetu watatufikilia viti siwataona ni band ya walevi.
 
Kimsingi simkatazi mtu kunywa pombe hata mimi na kunywa lakini tunywe baada ya kazi sio muda wa kazi.”Alimalizia kusema Big Boss huyo wa Waluguru Og. 
 
Muda huu wa mchana Mlala nje kamvutia waya Mmiliki wa band ya Maisha Mapya Joshua Malekela Maarufu ‘Joshkeri Msingisi’ kwa lengo la kumuliza kama kweli wanamuzi hao wanatabia za ulevi wakiwa jukwaani.
 
Kama ni kweli wanatabia hizo kwa nini band yake imekuwa Damp la kuchukua wanamuziki ‘Chapombe’ waliotimuliwa band nyingine?simu yake iliita bila kupokelewa licha ya mlala Nje kuipiga zaidi ya mara 2.
 
Juhuzi za kumtafuta Big Boss huyo wa Maisha Mapya ili kujibu mswali hayo. 
 
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...