UJUMBE WA NENO LA MUNGU
MALAKI 2 -16
“Maana mimi nachukia kuachana,asema Bwana Mungu wa lsraeli,naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia,asema Bwana wa Majeshi bali jihadharini roho zenu msije mkatenda kwa hiyana” Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya Julai 21.
UCHAMBUZI.
Hivi karibuni nilisoma kwenye gazeti kwamba kuna moja ya Majiji makubwa Tanzania utafini umeonyesha kwa mwezi talaka mia tatu[300]zinatolewa.
lkiwa na maana kwa mwezi ndoa 300 zinavunjika,hii inaonyesha watu wengi tumekosa hofu ya Mungu tukipuuza viapo vyetu vya ndoa tukivunja maagano yetu ya kuvumiliana kwenye shida na raha, ugonjwa na uzima mpaka kifo kitakapotutenganisha.
Kwenye hili la kuachana wanaoteseka ni watoto, baba utaona mke mwingine na mama utaolewa na mume mwingine starehe zenu zitaendelea vile vile.
Utakuta watu wanaachana huku wana watoto wadogo 4 mkubwa ana miaka 7 na wa mwishi miaka 2.
Kwa umri huo watoto hao wanatakiwa kubaki na Mama ambaye hana kazi maalumu ya kujipatika na tunajibua sisi wanaume wa siku hizi baadhi yetu ni mabigwa wa kukwepa majukumu hivyo hilo la kurea watoto wamwanaume mwenzio ni wachache sana wenye moyo huo.
Mwisho wa Siku Mlaika hao wa Mungu wasio na hatia wanaacha shule wataingia mtaani kujitafutia riziki wenyewe huko watajiingiza kwenye makundi mabaya ya watoto Machokolaa na wale Panya Road.
Kwenye somo hilo Mungu pia amechukizwa na watu wanaovaa nguo nusu uchi wasiojistili.
Kwenye dhama hizi tunazoziita za Kidigital Maadili yemomonyoka sana,utakuta mwanamke amevaa kigauni kifupi[Kimini]anakwenda sokoni.
Kama hiyo haitoshi utashangaa kumuona Mama mtu mzima mke wa mtu kashona sare ya Kijora[Gauni la Kitambaa chepesi lililochanwa pande zote mbili] kijora pambe ana kwenda kwenye shughuri ya shoga’ke.
Usafiri wake wa boda boda akikaa kwenye hiyo boda boda ndio kabisa hicho kijora pambe kinamuacha uchi anakatiza mtaani watoto na watu wazima wanamtazama.
lshu hii ya ndoa nitaifafanua zaidi kwa mifano iliyo haia kesho kwenye makala ya[Mahaba] mahusiano ya kimapenzi
Kwa wanaume utakuta dume zima na ndevu zake kashusha suluali chini ya makalio huku nduo yake ya ndani ikionekana kwa asilimi 80 anakatiza mtaani mbele ya wanaume wenzie.
Utashangaa hiyo ‘Jeans’ kainunua bei mbaya elfu 70 mpaka laki moja halafu anaishusha anaikanyaga na viati.
Tusidanganyike na haya maisha mafupi hapa duniani tumuogope Mungu na kulikumbuka kaburi letu.
‘Waluguru wanasema Ubaya Ubwella’
Maana yake Ubaya ulioondoka umeludi tena.
No comments:
Post a Comment