Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 13, 2024

UDAKUZ SPESHO NGUMU KUMEZA. CHANGUDOA AMFANYIA KITU MBAYA MUME WA MTU.


Na Mdakuzi Dunstan Shekidele, Morogoro. 

“NDIO Mkome na tamaa zenu wake mnao mmewaacha majumbani Mnahangaika na hawa machangudoa.”

Mama mmoja wa makamo alitoa kauli hiyo nzito kwenye tukio la Mwanaume mmoja ambaye anadai kuwa mume wa mtu kufanyiwa kitu mbaya na Mwanamke  nayedaiwa kufanya biashara haramu ya kuuza mwili wake ’Maarufu Changudoa au dada poa’

Tukio hilo ambalo halikushuhudia Live na Mdakuzi limetokea hivi karibuni kwenye moja ya kambi maarufu za machangudo za mkoani hapa.

Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo wambeya wa mjini wanaoshi kwa kufuatilia mambo ya watu walimrambia Ubuyu huyo Mdakuzi wa mtandao huu na kumueleza ‘Black and White’ za tukio hilo. 

Kwa vile Mdakuzi hakuwepo eneo la tukio hivyo  habari hii anairusha  kwa mfumo wa Kidakuzi.

             WASIKIE WAMBEA SASA.

Shekidele juzi umekosa habari nzuri hapa[anataja jina la kambi hiyo ya machangudoa] machangudoa wamemtaiti mteja wao.

 Ishu ilikuwa hivi nasikia huyo jamaa alifika pale kambi ya Machangu kachagua dada poa mkali kamchomoa na kuuliza bei kambiwa elfu 10.

 Jamaa kutaka sifa iliaonekana anapesa mbele ya kundi la machangu kazama mfukoni toka burungutu la pesa kama laki tatu hivi kachomoa elfu 10 kamlipa huyo dada poa kaingizwa ndani kuibanjua amri ya 6 inayozuia kuzini.

Walipomaliza kuivunja  amri hiyo ya Mungu wawili hao,walitoka nje  Changudoa huyo kamgeuzia kibao Mteja wake huyo kamkunja shati akitaka kuongezwa  elfu 50.

Jamaa kashangaa huku akipinga kwa madai kwamba hawakuwa na makubaliano yoyote zaidi ya yale ya awari ” alisema Mmbeya huyo na kuendelea kumwaga Mtama kwenye kundi la kuku wa kienyeji.

Kosa la Yule jamaa ni ushamba na ujinga uliopitiliza mbele ya machunguda unawaonyesha lundo la pesa ukiwatamanisha lazima wakifanyie kitu mbaya ili wakuchukue hizo pesa.

Wale madada poa wanaumnoja sana waliungana kundi zima wakimtaka  wakamuweka mtu kati mume huyo na kumuamulu kumlipa mwenzao kiasi hicho cha pesa vinginevyo watamjazia watu watakaompiga picha kutumia simu.

Jamaa  kusikia hivyo kawa mpole kakubali kutoa pesa kukwepa fedhehesha kwa jamii, watoto wake  pamoja na mkewe, kazama mfukoni na kutoa burungutu hilo la pesa na kumpa elfu 50 Changudoa huyo aliyekuwa amekunja shati.

Baada ya kupewa wekundu hao 5 muuza sukari huyo alimuachia jamaa huyo ambaye fasta aliita boda boda na kutimka eneo hilo huku akiapa kutoludi tena kwenye kambi hiyo.  

Machanguoda hao kwa umoja wao wakamjibu ’ usipokuja wewe mjomba’ko au mdogo wako  watakuja kama ulivyokuja wewe”alimalizia kusema Mbeya huyo.

Manispaa ya Morogoro inakambi tatu Maarufu za machangudoa  ‘wanaodanga’ majina ya kambi hizo yanahifadhiwa kwa sababu Mdakuzi hataki kuwa sehemu ya kuzitangaza  akikwepa kuwa  Katapila la kuwachongea watu barabara ya kuelekea jehanamu.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...