MARKO 10.17-31
“Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani,mtu mmoja akaja mbio akampigia magoti akamuliza, Mwalimu mwema nifanye nini nipate kuulithi uzima wa milele?
Yesu akamwambia kwa nini waniita mwema?Hakuna aliyemwema ila mmoja ndiye Mungu.
Wazijua amari, Usiue,usizini,Usiibe,Usishuhudie Uongo,Usidanganye,Waheshimu baba yako na Mama yako.
Akamwambia Mwalimu haya yote nimeyashika tangu Utoto wangu.
Yesu akamkazia macho,akampenda akamwambia, umepungukiwa na neno moja, Enenda ukauze ulivyo navyo vyote,uwape masikini nawe utakuwa na hazina mbinguni kisha njoo unifuate.
Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo,akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Yesu katazama kote kote akawaambia wanafunzi wake jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu.
Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake,Yesu akajibu tena akawaambia watoto jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu.
Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Nao wakashangaa mno wakamwambia ni nani basi awezaye kuokoka?
Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu sivyo maana yote yawezekana kwa Mungu.
Petro akawakazia macho, akasema kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu sivyo maana yoye yawezekana kwa Mungu
Yesu akasema Amina nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba au ndugu waume au ndugu wake au mama au baba au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwaajili ya lnjili.
Ila atapewa mara mia sasa wakati huu nyumba na ndugu wake na mama na watoto na mashamba pamoja na udhia na katika ulimwengu ujao uzima wa Milele.
Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na wa mwisho watakuwa wa kwanza.” Hilo ndilo neno letu la Leo jumapili ya Julai 7 sina cha kuchambua kwenye ujumbe huu naamini umeeleweka vizuri, mwenye Masiki na asikie asiye na masikio[…..]
Kinachonishangaza kwenye neno hilo wanafunzi wote wa Yesu walikuwa malofa hakuna mwenye mali hata mmoja lakini walimbana kuhusiana na matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Ukimnyanyasa masikini kwa sababu unakagari kako kanakofanana na jezi unakalolazwa siku ukifa, au unamnyanyasa masikini kwa sababu ya kajumba kako ambako kanafanana na kaburi l utakalozikwa tuache babia hiyo tutakufa hizo mali tutaziacha hapa hapa duniani tutakwenda mbele ya Mungu na roho zetu pekee.
Nani alifirisika kwa sababu ya kumsaidia masikini? kama yupo ajitokeze hadharani binafsi kwa uwezo wa Mungu nitaongoza harambee ya kumchangia kurejesha utajiri wake.
Ifahamike kuwa na nyumba au gari sio dhambi, hata mimi nina nyumba na gari, dhambi ni namna gani tunazitumia hizo mali?.
somo linatufusha tusiwadharau au kuwanyanyasa wenzetu ambao hawana hizo mali kwa maana ya nyumba na gari.
Pia mali hizo zisitufanya kuw ana kiburi kiasi cha kumsahau hata huyo Mungu aliyetupali mali hizo.
Katika kuthibitisha hilo wanafunzi walimuliza yesu kwamba kwa mantiki hiyo matajiri hawataurithi ufame wa Mungu?, akawajibu lisilowezekana kwa wanadamu kwa Mungu lawezekana wataingia kwa Neema ya Mungu.
Akiwa na maana ya wale waliotumia utajiri wao kuwasaidia masikini na kutoa sadaka kwa Mungu fungu la kumi la utaji wao.
No comments:
Post a Comment