Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 4, 2024

ALIYEMFOKEA KIPOFU ALIYEMUOMBA MSAADA AKIONE CHA MOTO.


 

 

             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KWELI hukumu ni hapa hapa duniani, msemo huu umethihilika juzi  Mkoani hapa,baada ya bosi mmoja kumkalipia Mama mwenye  Ulemavu wa macho[Kipofu]aliyemuomba msaada.

Tukio hilo la kuhudhunisha linalipingana pia na Maagizo ya Mwenyezi Mungu, limetokea juzikati katikati ya Mji wa Morogoro jirani na Soko kuu la Morogoro Maarufu Soko la Chief Kingalu na kushuhudiwa ‘Live’ na Mwandishi wa habari hizi.

            TUKIO LILIKUWA HIVI.

Mwanahabari wa Mtando huu aliketi kwenye Bench linalikaliwa na Madalili na wapiga picha za Mitaani eneo la Lunna  jengo la Hospital ya wahindi ya Ahmadya.

Mbele ya hospital hiyo kuna eneo la maegesho ya magari, Mtandao huu ulimshuhudia jamaa mmoja akiegesha gari lake la kifahari  eneo hilo baadae familia yake kwa maana ya mkewe na watoto  watatu walishuka na kuelekea soko la Kingalu.

Baba huyo wa familia alikunyua siti na kujilaza kwenye gari akiisubiri familia yake huku akiperuzi mitandao ya kijamii kupitia simu yake.

Wakati akiperuzi  Mama  aliyekuwa akiongozwa na mtoto wa kiume anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 7, walitinga kwenye gari hilo  wakamsalimia bosi huyo na kumuomba msaada.

Chaajabu bosi huyo hakuitikia salamu hizo badala yake aliwafokea na kuwafukuza huku akiwaambia wanamvuluga kwenye mambo yake hayo ya kuperuzi.

Kwa kauli hiyo kali mtoto huyo aliingia woga masikini ya Mungu kamvuta fasta mama yake wakaondoka eneo hilo kwa kasi wakimhofia bosi huyo aliyeonekana kufura hasi kwa kuombwa msaada.

Sote tulioshuhudia tukio  hilo tuliumia  sana huku kila mmoja akimlani bosi huyo kwa namna anavyojua.

Baada ya nusu saa familia yake imereja na mafurushi ya vyakula walivyonunua kwenye soko hilo, bosi huyo kashuka kwenye gari kafungua boneti akajaza mavyakula hayo na kwenda kula yeye na familia yake huku akimfokea kipofu na mwane waliomuomba pesa ya chakula.

                     MUNGU MKUBWA.

Baada ya kufunga boneti na familia yake kuingia kwenye gari bosi huyo alipowasha gari kwa lengo la kwenda nyumbani wake kula manyakula hayo gari liligoma kuwaka.

Bosi huyo na familia yake wakahangaika  kuliwasha bila mafamikio,baadae tukamsikia mkewe akisema.

 ’Mume wangu kuna nini hili gari ni mpya na halijawahi kugoma kuwaka toka tununue umelifanya nini kwa muda huu mfupi tuliokwenda sokoni”?  

Bosi huyo kamjibu kwamba hata yeye anashangaa, baada ya kushauriana waliamua kumpigia simu  fundi ambaye alimuambia akodi boda boda aje fasta.

Baada ya dakika kama 20  fundi alifika bosi kalipa boda boda elfu 300 na fundi akaanza kazi ya kulikagua gari na kubaini bosi huyo wakati anaperuzi aliacha On kitu kilichonyonya betri hiyo na kukosa nguvu ya kuwasha gari.

Fundi alimtaka bosi  kumkodia  boda boda nyingine afuta waya na betri nyingine kwa lengo la kuibusti betri hiyo, bosi  katoa elfu 3 nyingine fundi kakodi boda boda.

Baada ya dakika 20 akaja na waya na betri nyingine inayoonekana kwenye boneti na kuibusti betri hiyo na gari  likawaka.

Hatujuia fundi huyo alimlia kiasi gani kwani baada ya gari kuwaka fundi kapanda kwenye gari hiyo wakaondoka na bosi huyo tulicho shuhudia ni bosi huyo kulipa elfu 6 za usafiri wa boda boda.  Binafsi najiuliza bosi huyo angepungukiwa nini kama angempa mlemavu yule elfu 1 au miaka 5? Ona sasa Mungu kachukua pesa nyingi kwa njia nyingine.

Kwa hasira ya kupoteza muda mwingi eneo hilo gari lilipowaka  alijisahau kufunika boneti akaendesha  kwa kasi hekima na huruma ya kuwahurumia wanae walikuwa kwenye gari nikaamua kumstua akastua kasima na kulifunga.

Wenzangua niliokaa nao walinichamba sana wakisema”

Huyu mtu sio mstaarabu hakutusalimia mbaya zaidi kumfokea kipofu aliyemuomba msaada mungu kamuonyesha kwa kulizima gari lake, Mungu alitaka kumpa mtihani mwingine kwa boneti kuasua kioo wewe shekidele’

Nikawajibu hivi.’Tumefundishwa na Mungu usilipiza baya kwa ubaya mtu akikupiga shavu hili mgeuzi na la pili, pia siku zote giza linaondolewa na nuru.

Pamoja na hayo kilichonisukuma kumwambia afunge boneti kuna wale watoto na mkewe kwenye jambo hili na his hawana hatia hivyo boneti lile lingebinuka akiwa mwendo kasi lazima gari lingepinduka na hao watoto na mkewe akiwemo fundi wange patwa na majanga ya kupoteza maisha au kujeruhiwa.     CAPTION.

 Gari hilo ambalo limefichwa namba kwa sababu za kimaaidli likitengenezwa na kulia aliyezibwa na kimvulia cha giza kwa sababu maalumu ndiye bosi  aliyemfokea kipofu huyo.

 Siku zote nitakuwa mstari wa mbele kuwatetea wanyonge hata ikitokea kuweka rehani uhai wangu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...