Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 9, 2024

SIMBA YA MTAMBULISHA MCHEZAJI ALIYEISAIDI DAMU CHAFU FC KUTWAA MAMILIO YA MICHUANO YA NDONDO CUP MASHABIKI WA YANGA WAKEJERI.


Abdularack Hamza aliyezungushiwa duara akiwa na kikosi cha Damu Chafu June 28.

 



 Abdulrazack akitambulishwa na Simba Julai 4.


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WAZEE wa Robo fainali ya Michuano ya Kimataifa’CAF Champions League’ Simba Sports Club ’S.S.C’wamemsajiri mchezaji aliyeisaidia timu ya Damu Chafu kunyakua Mamilio ya Michuano ya Ndondo Cup.

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Ulinzi [beki]ni Abdulrazack  Mohamed Hamza ambaye ljumaa ya June 28 majira ya saa 10 jioni alipigwa Picha na Mwandishi wa Mtandao huu uwanja wa Saba saba mkoani hapa,akiwa na kikosi cha timu ya Damu Chafu akiitumikia kwenye mchezo wa Nusu fainali ya Michuano hiyo.

Mchezaji huyo aliyekuwa akiitumikia timu ya Super Sport inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Afrika Kusini baada ya ligi hiyo kutamatika alirejea nyumbani Morogoro kwa mapunziko hivyo Viongozi wa Damu Chafu walimfuata na kumuomba wasaidi kwenye mchezo huo wa Nusu fainali.

Kwenye gemu hiyo iliyokuw ana upinzani mkali kwa muda wote wa dakika 90, Abdulrazak aliyecheza vizuri nafasi ya ulinzi aliisaidia  Damu Chafu kuinyuka timu ya Wakushi Fc yenye maskani yake Manzese Morogoro na kupata tiketi ya kutinga fainali ya michuano hiyo.

Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo  siku 6 mbele kwa maana ya Julai 4 tulishuhudia Abdulrazam Hamza akitambulishwa kujiunga na timu ya Simba na kwamba kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya Ndondo Cup kati ya Damu Chafu na Black Viba iliyopigwa Ijumaa ya Julai 5 Abdulrazack hakuwepo kwenye mchezo huo ambao Damu Chafu alinyakua ubingwa baada ya kuichapa timu ngumu ya Viba kwa bao 1-0 na kukabidhiwa kombe na Pesa taslimu Milion 4 huku mshindi wa pili Viba akinyakua milioni 2.

 MASHABIKI WA YANGA WATUPA VIJEMBE KWA WENZAO WA SIMBA.

Katika mchezo huo wa fainali unaotajwa kuvunja rekodi ya kujaza mashabiki wengi kwenye dimba hilo la Saba saba, Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Shabiki wa Yanga ‘Baunsa’Big Suma aliwatania mashabiki wa Simba akisema.

”Nyie simba mnatuambia sisi yanga ni kambi ya kurea wazee  msimu huu sasa na nyingi  mmechoka kiasi cha kumsajiri mchezaji kutoka timu ya Damu Chafu, kweli beki huyo wa Damu chafu ataweza kumzuia Master Aziz K? msimu huu kuna jitu litapigwa 7.

Haya leo Scaut wenu kwenye mchezo huu wa fainali sijui atamsajiri nani kesho fasta nitaweka data kwenye simu yangu na kuperuzi eji ya Simba.

 Tumeshuhudia kwenye mchezo wa Nusu fainali baada ya Abdulrazack kutoka hapa Saba saba tu kesho yake tumemsikia akitambulishwa Simba akitokea Damu Chafu ya Mafisa Morogoro kweli kwisha kupo.

Kama kuna mtu anabisha Abdularack akutoka Damu Chadu Shekidele alikuweo Ijumaa awaonyeshe picha” alisema shabiki huyo akiwatania mashabiki wa Simba. Lkumbukwe kwenye mchezo huo wa nusu fainali mashabi wa Damu Chafu na Wakushi wakitwangana makonde hali iliyopelekea Polisi kufyatua mabomu ya machozi uwanjani wachezaji wa timu zote 2 akiwemo Abdulrazack walikimbia kukwepa moshi mchungu wa mabomu hayo.

                  


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...