TAMASHA la kanisa la Faith Baptist lenye makao yake Makuu nchini Marekani limefanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro huku baadhi ya waumini hao kutoka Marekani wakivutiwa na Mtoto Glory Dustan Shekidele [kulia] waliyeamua kupiga naye pichana huku wakimtazama na kumwaga matabasamu.
Mwandishi wa habari hizi aliamua kwenda na Glory kwenye Tamasha hilo kwa lengo la kuendelea kumjenga kiimani.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KANISA la Faith Baptist la Mkoani Morogoro limeandaa Tamasha kubwa lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, huku mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Jerry White alimtumia Mwanae kwenye sehemu ya Mahubiri aliyoyatoa kwa umati mkubwa wawatu wa dini zote waliofurika kwenye Tamasha hilo linalofanyika kila Mwaka.
Mchungaji huyo raia wa Marekani yalipo makao Makuu ya Kanisani hilo alitoa mahuri hayo wakati wa Mapunziko ya mchezo wa Soka kati ya timu ya KMC inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara dhidi ta timu ya Kanisani hilo kutoka Marekani.
Mara baada ya Mwamuzi Fikirini Magari aliyechezesha mchezo huo wa Kirafiki wa Kimataifa kupuliza filimbi ya kuashiria kutamatika kwa dakika 45 za awari, Mchungaji Jerry anayeongoza kanisa hilo lililopo Bingwa Manispaa ya Morogoro alipanda jukwaani huku baadhi ya waumini wake wakinyanyua Msalaba mkubwa mbele ya jukwaa kwa muda wote wa mahubiri hayo.
Baadae Mchungaji huyo anayezungumza kiswahiri fasaha alimwita Mwanye jukwaani na kumtumia kama mfano kwenye sehemu ya mahubiri yake akisema.
”Tutafanikiwa kwenda mbingini kwa njia moja tu ya Yesu kristo aliyemwaga damu yake kutukomboa sisi.
Hivyo mali zetu, Umaarufu wetu, Vyeo vyetu, Wazazi wetu vyote hivyo haviwezi kutupeleka mbinguni , huyu ni Mwanangu wa kwanza anaitwa David hawezi kuingia mbinguni kwa sababu mimi baba yake ni Mchungaji hapa haiko hivyo ataingia mbinguni kwa matendo yake mema na kuivaa damu ya yesu iliyomwagika pale Msalabani”alisema mchungaji huyo huku akimvisha mwanae huyo joho linalofanana na damu.
Wakati mahuri hayo yakiendelea wanakwaya wa kanisani hilo kutoka Marekani waliotinga kwenye Tamasha hilo kulinogesha kwa njio za kiswahiri,kwa muda wote wa dakika 15 za mahuribi hayo walichutama makundi makundi huku wakishikana mikono wakifuatilia mahubiri hayo yaliyotolewa kwa lugha ya kiswahiri ambayo hawaifahamu ingawa waliimba nyimbo kadhaa kwa lugha hiyo hadhimu ya kiswahiri.
Hali hiyo ilimsukuma Mwandishi wa habari hizi kuzungumz ana mmoja wawanakwaya hao, ambaye amesema huo ndio umamaduni wao wakati wa mahubiri wanaacha kila kitu na kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa utii wa hali wa juu.
Baadae Mtandao huu utarusha picha za matukio mbali mbali ya mchezo wa soka kati ya timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni’KMC’ dhidi ya timu ya kanisani hilo kutoka Marekani.
Hivyo nakushihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kwa mabari Moto moto za chini ya kapeti
No comments:
Post a Comment