Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 30, 2024

KMC YAISHUSHIA KICHAPO CHA MBWA MWIZI TIMU KUTOKA MAREKANI.




Kikosi cha wazungu hao kikika mbele ya kamera za Mtandao huu.



 Chama hilo la Wamarekani likifungwa bao la 4 na kumuacha kipa wa timu hiyo akiramba nyasi za Uwanja wa Jamhuri.




 


      Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni[KMC] Maarufu Kino Boys, imeishushia Kichapo cha Mbwa Mwizi timu kutoka nchini Marekani.

Gemu hiyo ya kirafiki ya Kimatifa iliyoandaliwa na Kanisa la Faith Baptist  lenye maskani yake eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro, imepigwa  Jumamosi iliyopita  Uwanja wa  Jamhuri Morogoro.

Hadi Mtandao huu unaondokla uwanja hapo dakika ya 72 ya mchezo huu uliopangwa kunogesha Tamasha la Kanisani hilo lenye Makao yake Makuu nchini Marekani, Vijana wa KMC ambao wameweka kambi mkoani hapa kujiandaa na Ligi kuu Tanzania Bara llikuwa mbele kwa bao 4-0.

 Ifahamike Kila Mwaka Kanisa hilo huandaa Tamasha hilo na wageni mbali mbali kutoka Marekani  hutinga nchini na kunogesha Tamasha hilo ambalo kiingilio chake ni bure na ukifika getini unakabidhiwa zawadi ya kitabu cha dini, kuponi ya kujaza taarifa zako na karamu.

Mwandishi wa habari hizi aliyetinga kwenye Tamasha hilo na Mtoto Glory Dustani Shekidele, Pichani  Mwenye gauni la Dack Bluu anyekunywa Juice ya Muwa, ilipotimu majira ya saa 12 alilalamika kuchapwa na baridi kali iliyoshuka kutoka juu ya Milima ya Uluguru iliyopojirani na Uwanja huo.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi huo aliamua kuacha kazi dakika hiyo ya 72 na kupiga gia Pikipiki na kumrejesha dogo huyo kwa Mama’ke akanyonye.

                

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...