Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 23, 2024

UKURASA WA MAHABA. ‘NILIYE KATA NAYE KUNI NDIYE NITAKAYEOTA NAYE MOTO’


Mwandishi wa habari hizi kulia mwenye miwani kama anakwenda kuchomelea vyuma akizungumza na Wastara .

pichani no2 Eto’o na mkewe kwenye matukio 2 tofauti.

 


          Na Dustan Shekidele,Morogoro. 

MPENDWA Mdau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, Nakusalimu katika jina  kubwa la Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi, Ukuu wake usiofananishwa na kitu chochote.

Ama baada ya salamu tuingia kwenye Mada yetu ya leo kwenye kipengele Pendwa cha soma la Mahusiano ya kimapenzi[Mahaba]

Juzi Jumapili kwenye Ujumbe wa neno la Mungu unaoluka kila Jumapili kwenye Mtandao huu, tulinukuu maneno ya Mungu katika kitabu kitakatifu cha Bibibli  Malaki 2-16. Mungu akichukizwa  watu kuachana.

Ifahamike kwenye jumbe huo  Mungu alisema anachukizwa na watu kuachana ikiwemo wanandoa na wachumba wenye malengo ya kuingia kwenye ndoa.

Sote twafahamu kabla ya kuingia kwenye agano la ndoa kwanza tunaanza uchumba kwa lengo la kuchunguzana tabia, kwenye eneo hili ndio mahusiano mengi huvunjika kuliko hata huko kwenye ndoa.

Kufuatia hali hiyo somo hili litajikita kuelezea lshu ya wachumba  kuachana na wachache kuvumiliana na kufika kwenye malengo yao ya kufunguka pingu na maisha na kujenga familia bora.

  Kuna kundi kubwa la wachumba baada ya  kuwachunguzana wenzi wao wanajilishisha kwamba  sio  sahihi  kuingia nao kwenye ndoa. Na maamuzi haya ya mtu binafsi yaheshimiwe na wote hata Mungu kupitia Biblia alisema ndoa na iheshimiwe na watu wote wakiwemo wazazi.

Sasa kama Mungu kawazuia hata wazazi ambao ni miungu yetu ya duniani kuingilia ndoa na mahusiano yetu,wewe Shoga au jamaa unapata wapi ujasili wa kuingilia na kuvunja ndoa ya rafiki yako?

Baadhi wanasababu za msingi za kuvunja uchumba  mfano mtu anatafuta Mume au mke mchana Mungu na mpambanaji wa maisha, kwenye uchumba baadae huyo mchumba uliyepanga kumpa maisha yako awe baba bora au mama bora wa familia unabaini ni mlevi wa kutupwa, au unabaini ni mzinzi simu zake zimejaa namba za michepuke wake.

Ushauri wangu kwako uliyekutana na mchumba wa namna hii, kama unampenda usikimbilie kuachana naye muweke chini mueleze kwa hekima achane na hali hiyo ili malengo yenu ya kufunga ndoa yatimie.

Kumbuka hapa chini dunia hakuna mkamilifu kila mtu ana madhaifu yake kikubwa kurekebishana  na kujenga mahusiano ya kusikilizana na kuheshimiana mkitanguliza Mungu mbele.

Kama naye anakupenda atakusikiliza na kuacha hizo tabia mbaya. Kama hatakusikia akaendelea na mambo hayo basi jua huyo hakupendi  achana atakupotezea Muda.

Ukishachukua maamuzi hayo magumu nakusihi  usikate tamaa zidisha viwango vya lmani na maombi Mungu wako huku ukiendelea kumtumani yeye akupe mume au mke  bora, kwenye hili hata vitabu  vya dini vinasema subrani ni lbada.

Vile vile kuna baadhi ya wachumba huwaacha wenzao kwa hila, akiwa maarufu au tajiri anamucha mchumba’ke aliyetoka naye mbali na kuoa tajili mwenzake au mtu maarufu.

Pia kuna baadhi ya wanawake Mume  kafukuzwa kazi au kafirisika kwenye biashara zake pesa imekata Mwanamke huyo analiamsha dude akitafuta mlako wa kutoka akatafute mwanaume mwingine mwenye pesa.

Kwenye hili ninamifano mitatu iliyohai, mfano wa kwanza.

Takribani miaka 3 iliyopita niriripoti habari ya Jamaa mmoja kutaka kujiua baada ya mchumba’ke aliyemsome kumtumia jumbe mfupi[sms]kwenye simu akimueleza kwamba anamshukuru kwa kumsomesha lakini anasigitka kumueleza kwamba hana mpango wa kufunga naye ndoa kama walivyokubaliana kwa sababu amepata msomi mwenzake na kwa elimu yake hawezi kuolewa na mtu anayebadi nyimbo kwenye simu.

 Jamaa huyo anayefanya biashara ya kubani nyimbo  eneo la Mwembesongo mkoani haa aliyemsomesha mchumba’ke huyo kwa biashara hiyo.

Baada ya kusoma sms  kaenda dukani  kanunua sumu ya Panya kanywa kwa lengo la kujiua, bahati nzuri rafiki yake alikimbia muembe mkubwa na kununua maziwa fresh  akamnyesha na kukata makali ya sumu nakufanikiwa kuokoa maisha yake.

Pili. Hivi karibuni kwenye mitandao ya Kijamii ilitembea picha ya Staa wa zamani wa soka dunia ambaye kwa sasa ni Rais wa chama cha Soka nchini Cameroon Samuel Etoo.

 PIcha hizo mbili tofauti zilimuonyesha  Eto’o akiwa na Mchumba’ke ambaye kwa sasa ubao unasoma ni mke wake.

Niliposoma maelezo ya picha hizo mbili tofauti  yalisema, picha ya kwanza inamuonyesha Eto’o akiwa na mchumba’ke aliyekuwa akifanya kibarua kwenye moja ya  Salooni za kike nchini Ufaransa.

Taarifa hiyo inasema wakati huo Eto’o alikuwa hana kazi yoyote alikuwa kijana mdogo akiwa shule ya soka  ‘Academy’ akijitafuta kisoka, maelezo hayo yalidai bint huyo  ujira aliolipwa hapo Saloon alimega sehemu na kumpa Eto’o ajikimu kimaisha hao chuo cha soka.

Mungu Mkubwa baadae Eto’o gari limewaka kawa mchezaji mkubwa kajiunga na timu kubwa duniani na kulipwa mshahara mkubwa, akaukwa utajiri na Ustaa mkubwa duniani Ustaa na Utajiriu huo ulimfanya Eto’o ashobokewe na wanawake wengi duniani, aliwapiga chini wote na kwenda Ufaranisa kumuona Yule bint wa Saloon ambaye kwa sasa  muonekana wake ndio huo kwenye picha ya pili.

Tatu. Wasanii Maafuru nchini wa sinema za Kibongo Wastara na Sajuki walielewa na kungia kwenye uchumba na mwisho wa siku wakaamua kuanza vikao vya harusi.

Wastara akiwa kwenye boda boda akielekea kwenye kikao hicho cha harusi  kwa bahati mbaya alipata ajali na kuvunjika mguu,ambao baadae ulikatwa baada ya kuvunjika vibaya.

Watu wengi machoka na masikio yalikuwa kwa Sajuki wakihoji je atakubalia kuendelea kumuona mwanamke mwenye mguu mmoja?

Umbeya huo ulivuka na kumsikia Sajuki ambaye alitoka hadharani na kuwajibu  kuwaziba akisema hata Wastara akikatika miguu yote miwili.

Kweli tulishuhudia Sajuka kamuoa Wastara na kuzidia  viwango vya Upendo na mahaba kwa mkewe, baadae walifanikiwa kununua mguu wa bandia ulimsaidia Wastara kuepuka kutembea na magongo.   

Siku chache baada ya kufunga ndoa Sajuki naye kaanza kuugua Wastara kamuugua mumewe mwanzo mwisho, hali ilipozidi kuwa mbaya wakaenda lndia.

Kama mnavyojua mambo ya nauli ya kwenda lndia na gharama za matibabu  pesa imekata, nakumbuka watu mbali mbali likiwemno gazeti la Sani likiongozwa na rafiki yangu Kessa  waliendesha harambee ya kuchangia matibabu ya Sajuki huko lndia.

Wastara katumiwa pesa hiyo ambayo pia ilikata tasipo mumewe kupona, nakumbuka wastara alikaririwa na moja ya magazeti akisema licha ya mumewe huyo kuugua kwa muda mrefu hata kata tama ya kumuguza.

Alifika mbali zaidi akitoa kauli nzito kwamba pesa zikimwishia atauza hata pete zake za ndoa ili kuokoa maisha ya Mpendwa Mume wake.

 Licha ya kauli hiyo Sajuki arifaniki dunia nchini lndia akiwa mikononi mwampendwa mkewa mwenye mapenzi wa kweli kwake.

 Mwandishi wa habari hizi anamuomba mwenyzi mungu kwa sala hii.

 “Hee Mwenyezi Mungu  aliyetuagiza tukuombe bila kukoma tunakuomba msamehe makosa yake ndugu yetu Sajuki  ikukumbeza umwingize kwenye pepo ya milele mambo mengi alivyofanya  hapa  dunia  tumeyaona yamefuata misingi na matakwa yako hee mwenyezi Mungu msamhe kwa yale mabaya aliyofayanya kwa kujua ama kwa kutokujua.

 Mtumishi wako Sajuki kwa kushirikiana na mkewe Wastara wamekuwa somo  zuri kwetu sisi wanandoa na wachumba ambapo wengi wetu kupitia mahusiano yaliyopitia changamoto nyingi ambazo tunaamini wamezishinda, tunayafanya kama kioo cha kujitazama pindi mahusiano yetu yanapoteteleka” Ewe Mungu tunaomba usikie maombi yetu na hatukulazimishi bali kwa utukufu wako. sote tuseme amen.

      KAULI YA MWANDISHI WA HABARI HIZI.

“Kwangu mimi niliyepata naye tabu ya kukata kuni msituni ndiye ambaye nitaota naye Moto.

Utakapo Muacha mchumba’ko au mume\mke kwasababu umekuwa tajiri au Staa Yule wa kwanza unamuona mshamba kamwe huwezi kukaa salama hukunu ya Mungu ni hapa hapa dunia”


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...