Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 2, 2024

A-Z BODA BODA ALIYEFARIKI DUNIA AKIDAIWA KUFAKAMIA POMBE KALI, MAMA MZAZI AFUNGUKA MAZITO.WAKILI NAYE ATIA NENO.


 Bi Hellena Ng’aga mama mzazi wa marehemu akizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana.

 Mtandao huu umetumiwa Clips Video ya shindano hilo toka likimuonyesha boda boda huyo akizimika na baadae kikumbizwa nyumbani kwao.

 


              Hayati Charles enzi za uhai wake.
 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TAKRIBANI  siku nne Mwandishi wa mtandao huu ulikuwa kazini kukusanya taarifa za kifo cha boda boda aliyedaiwa kufariki dunia kwenye shindano la kunywa pombe kali.

Awari Mtandao huu ulitoa taarifa hiyo kwa mfumo wa  kidakuzi kwa kufunika funika  Mambo kwa kuzingatia  maadili ya Uandishi wa habari.

Baada ya kukamilisha matakwa ya kanuni za Uandishi wa habari kwa kuzungumza na wahusika wote kwa sasa Mwanahabari anaeleza A-Z za kifo cha ndugu yetu huyo aliyefahamika kwa jina la Charles John Ng’aga[46] ambaye alikuwa boda boda kwenye kijiwe cha geti kuu la kuingilia uwanja wa Saba saba.

Breki ya kwanza Mtandao huu ulifika eneo la tukio kwenye kijiwe hicho,panapo daiwa kufanyika  shindano hilo la kufakamika Pombe kali.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Athuman Shabani alisema.

”Nikiwa hapa getini Saba saba kwenye biashara yangu niliona Abdul na Charles wakiwekeana bima ya kunywa pombe kali chupa 5 bila kupunzika.

 Wakiwekeana bima Charles kasema anauwezo wa kunywa mfurulizo chupa  5 za Pombe hizo kali huku Abdul akipinga akidai Charles hawezi kumaliza kiasi hicho  ubishi uliposhika kasi wakawekeana bima ya elfu 10 Mwamba kaanza kufakamia ya kwanza alipofika ya 4  ameanza kuregea huku akiwa juu ya boda boda yake Shekidele Clips Video hii hapa ya tukio hilo”alisema shuhuda huyo na kuendelea kufunguka.

Baada ya kuona kazima boda boda wenzake wamewasha boda boda wake wakampakia mshikaki wakampeleka kwao hapo mtaa wa nyuma baada ya masaa kadhaa tunasikia amefariki”alisema Athuman.

Siku hiyo hiyo ya ljumaa Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa marehemu na kushuhudia ndugu na jamaa wakiwa kwenye maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao.

Hekimu ilimuongoza Mwandishi wa habari hizi kusitisha mahojiano na familia mpaka  watakapompunzisha mpendwa wao kwenye nyumba yake ya Milele aliyezikwa jumamosi iliyopita.

 Jana jumatuta Mtandao huu ulitinga tena nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Kiswanya ‘A’ Kata ya Uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuzungumza na Bi Hellena Ng’aga ambaye ni Mama mzazi wa marehemu alipohojiwa alikuwa na haya ya kusema.

”Mwanangu amezimika kama mshumaa asubuhi katoka hapa nyumani na pikipiki yake kaniaga ana kwenda kazini, nashangaa baadae analetwa  hakiwa hoi ajitambui amerehea kama mrenda nilipouliza nimeambiwa kashiriki shindano la kunywa pombe kali[anataja jina la pombe]. 

Baada ya kunywa kazidini kuona hivyo wenzao wamekuja hapa kunibwagia, nilichofanya nimempa huduma ya kwanza kwa kumlisha Malimau”alisema mama huyo na kuongeza.

 Nilivyomnywesha  nilishuhudia katapika vitu vya ajabu  baadae  nilishuhudia tumbo lake likiwamba kama ngoma, kuona hivyo tukaamua kumkimbiza hospital tulipotoka hapo nje  hate kwenye usafiri hajaingia mwanangu amekata roho”amesema Bi Mkubwa huyo na kuangua kilio. 

Mwandishi wa habari hizi alibeba jukumu la kumbembeleza kwa lengo la kukamilisha mahojiano hayo, baada ya kunyamaza aliulizwa swali la mwisho kwamba marehemu ameacha watoto wangapi.?

Mama huyo alijibu.

”Ameacha mtoto mmoja aitwae Happy ambaye jana aliniambia bibi bibi wale waliomleta baba kwenye pikipiki nawajua twende tukawakamate, nikamwambia mjukuu wangu achana nao baba yako ameshakufa basi tumshukuru Mungu kwa hilo”alisema mama huyo na kumwaga tena machozi.

Mwisho Mwandishi wa habari hizi alimuomba picha za enzi za uhai wa marehemu ambapo bi mkubwa huyo aliingia chumbani  na kutoka na picha ya hayati Charles na kumkabidhi.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kiswanya ‘A’ Bi Shamim Tindwa alithibitisha msiba huo kutokea mtaani wake.

”Ni kweli  msiba huo ulikuwepo mtaani kwangu lakini wakati unatokea  nilikuwa safari nimeludi jana jumapili na marehemu amezikwa jumamosi kwa hiyo sina taarifa za ndani juu ya kifo hicho.

 Kila mtu anasema lake licha ya kwamba sikuwepo msibani niliwakilishwa na mjumbe wangu wa mtaa niseme tu hatuwezi kuingia kwenye mkumbo wa hayo yanayosema kwa sababu anayeweza kuthibitisha kifo cha mtu ni Daktari,  hayo unayoyasikia shemeji yangu shekidele  na mimi pia nayasikia hivyo hivyo kwa hiyo ”alisema mwenyekiti huyo ambaye ni mke halila wa Mwandishi wa habari Salum Tindwa.

 

 Mtandao huu ulishiriki mazishi hayo na kushuhudia baadhi ya watu  wakiingia kwenye mjadala mkubwa, ambapo baadhi walidai muhusika aliyeweka bima na marehemu hana kesi ya kujibu kisheria na wengine wakipinga wakida hana kesi ya kujibu.  

Ili kupata majibu ya ubishi huo jana jioni Mwandishi wa habari hizi alitinga ofisini kwa Mwanasheria ‘Wakili’ Shabani Hamza alipoombwa kutolea ufafanuzi kisheria ubishi huo wakili huyo alijibu kwa mifano.

“Kwangu mimi kisheria huyo aliyeweka bima ya kunywa pombe na marehemu hana kesi ya kujibu nitakupa mifano kadhaa.

Siumekuja hapa ofisini kwangu jengo la CCM Wilaya sasa nikuambia wewe ulivunje jengo hili ukikamatwaa kwa uharibifu huo ulioufanya peke yako mimi nitaingiaje kwenye kesi yako?

Mfano wa pili wewe unaona kabisa hili ni kaa la moto nakuambie ukishika kaa hilo nakupa elfu 10 ukashika na kuungua utaenda kunishitaki kwa kosa gani?huo ni mtazamo wangu ila tuendelee kufanya uchunguzi mimi na wewe ili tujilizishe kisheria”alimalizia kusema Wakili huyo maarufu mkoani Morogoro.

Pombe hiyo kali inayotajwa ni zile zinazouzwa kwenye maduka hata ya vichochoroni bei yake chupa moja elfu 2, nimejalibu kufafanua wadau wasije kujua pombe kali ni zile chua kubwa za bei kubwa kwenye mabaa makubwa hapana hizo.  

                          


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...