Na Dustan Shekidele,Morogoro.
ACHENI MUNGU AITWE MUNGU.
Mama mmoja aliyetoka ‘Reba’ hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kujifungua, amenusulika kifo na Kichanga chake baada ya Bajaj waliyoikodi kupinduka mara mbili eneo la Mji Mpya Mkoani hapa.
Ajali hiyo iliyoshuhudiwa ‘Live’ na Mwandishi wa habari hizi imetokea jana Mchana kwenye korongo la njia isiyo rasmi, kufuatia njia rasmi ya Mji Mpya inayoelekea Kichangani kufungwa kupisha matengenezo.
Madereva wengi akiwemo huyo wa Bajaj huchepuka kwenye njia ya panya kukwepa adha ya kuzunguka njia mbadara ya Masika kutokea ofisi za Tanesco Mkoa wa Morogoro.
Dereva huyo ilipojaribu kushuka kwenye korongo hilo huku akiwa na mzazi huyo aliyepakata kichanga chenye umri wa siku moja alijikuta akiporoboka jumla na Bajaj kubimbilika kama boga linanaloshuka milima ya Uluguru.
Mwanahabari wa Mtandao huu aliyekuwa mtaani kusaka matukio ulishuhudia wananchi wakivamia eneo la tukio na kumchomoa Mzazi huyo na kichanga chake.
Mama huyo alipohojiwa alisema.” Nimetoka Reba muda huu baada ya kuruhusiwa nimekodi hii Bajaj kwa bahati mbaya tulipofika hapa kwenye Korongo kibajaj nimepinduka mara mbili wakati kina bimbilika nilimkumbatia mwanangu na bimbilika naye Mungu ni mwema hakumia ila mimi najisikia maumivu kwenye mbavu na mkono”alisema Mama huyo .
Mwandishi wa habari hizi alimshauri kuludi tena hospital kwa ukaguzi wa afya yake na ya kichanga, alikubali ushauri huyo na kurejea hospital kwa kutumia Bajaj hiyo ambayo baada ya kupinduka wasamalia wema waliinyanyua.
Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Kitatu Aman Manzuli anayefanya biashara ya kuchoma mahindi mabichi eneo hilo alisema.
”Ndugu Mwandishi tunashangaa hii barabara imekamilika muda mrefu kwa kiwango cha zege Mwenge umepita mwezi wa 4 na kuizindua lakini wahusika hawaifungui.
Gari, Bajaj na boda boda zinalazimika kushuka kwenye korongo linalosababisha ajali mara kwa mara ”alisema shuhuda huyo na kuongeza.
“ Muda huu nimeshuhudia kibajaji hiki kikipinduka mara mbili tulivyokimbia masikini ya mungu kumbe kilimbeba mzazi aliyetoka reba kujifungua Mungu ni mwema huyo mzazi alikaa katikati na kichanga chake kulia na kushoto kulikuwa na ndugu zake hivyo wakati Bajaj inabimbilika mama kang’ang’ania kichanga chake mwanzo mwishi achema mama aitwe mama.
Kabla ya kunyanyua Bajaj tulimpokea mama kichanga na baadae tukamchomoa yeye kisha tukakiinyanyua Kibajaj”alisema Muza mahindi huyo.
Pichani baadhi ya wananchi wengi wao wakiwa kina mama wakimfariji mwanamke wenzao huku wakikikagua kicganga hicho.
No comments:
Post a Comment