Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 30, 2024

KMC YAISHUSHIA KICHAPO CHA MBWA MWIZI TIMU KUTOKA MAREKANI.




Kikosi cha wazungu hao kikika mbele ya kamera za Mtandao huu.



 Chama hilo la Wamarekani likifungwa bao la 4 na kumuacha kipa wa timu hiyo akiramba nyasi za Uwanja wa Jamhuri.




 


      Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni[KMC] Maarufu Kino Boys, imeishushia Kichapo cha Mbwa Mwizi timu kutoka nchini Marekani.

Gemu hiyo ya kirafiki ya Kimatifa iliyoandaliwa na Kanisa la Faith Baptist  lenye maskani yake eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro, imepigwa  Jumamosi iliyopita  Uwanja wa  Jamhuri Morogoro.

Hadi Mtandao huu unaondokla uwanja hapo dakika ya 72 ya mchezo huu uliopangwa kunogesha Tamasha la Kanisani hilo lenye Makao yake Makuu nchini Marekani, Vijana wa KMC ambao wameweka kambi mkoani hapa kujiandaa na Ligi kuu Tanzania Bara llikuwa mbele kwa bao 4-0.

 Ifahamike Kila Mwaka Kanisa hilo huandaa Tamasha hilo na wageni mbali mbali kutoka Marekani  hutinga nchini na kunogesha Tamasha hilo ambalo kiingilio chake ni bure na ukifika getini unakabidhiwa zawadi ya kitabu cha dini, kuponi ya kujaza taarifa zako na karamu.

Mwandishi wa habari hizi aliyetinga kwenye Tamasha hilo na Mtoto Glory Dustani Shekidele, Pichani  Mwenye gauni la Dack Bluu anyekunywa Juice ya Muwa, ilipotimu majira ya saa 12 alilalamika kuchapwa na baridi kali iliyoshuka kutoka juu ya Milima ya Uluguru iliyopojirani na Uwanja huo.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi huo aliamua kuacha kazi dakika hiyo ya 72 na kupiga gia Pikipiki na kumrejesha dogo huyo kwa Mama’ke akanyonye.

                

Sunday, July 28, 2024

TAMASHA LA FAITH BAPTIST. MCHUNGAJI MMAREKANI AMTUMIA MWANAYE KWENYE MAHUBIRI YAKE.

TAMASHA la kanisa la Faith Baptist lenye makao yake Makuu nchini Marekani limefanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro huku baadhi ya waumini hao kutoka Marekani  wakivutiwa na Mtoto Glory Dustan Shekidele [kulia] waliyeamua kupiga naye pichana huku wakimtazama na kumwaga matabasamu.

Mwandishi wa habari hizi aliamua kwenda na Glory kwenye Tamasha hilo kwa lengo la kuendelea kumjenga kiimani.











 

  

     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KANISA la Faith Baptist la Mkoani Morogoro  limeandaa Tamasha kubwa lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri, huku mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Jerry White alimtumia Mwanae  kwenye sehemu ya Mahubiri  aliyoyatoa kwa umati mkubwa wawatu wa dini zote waliofurika kwenye Tamasha hilo linalofanyika kila Mwaka.     

Mchungaji huyo raia wa Marekani yalipo makao Makuu ya Kanisani hilo alitoa mahuri hayo wakati wa Mapunziko ya mchezo wa Soka  kati ya timu ya KMC inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara dhidi ta timu ya Kanisani hilo kutoka Marekani. 

Mara baada ya Mwamuzi Fikirini Magari aliyechezesha  mchezo huo wa Kirafiki wa Kimataifa  kupuliza filimbi ya kuashiria kutamatika kwa dakika 45 za awari, Mchungaji Jerry anayeongoza kanisa hilo lililopo Bingwa Manispaa ya Morogoro alipanda jukwaani huku baadhi ya waumini wake wakinyanyua Msalaba mkubwa mbele ya jukwaa kwa muda wote wa mahubiri hayo.

Baadae Mchungaji huyo anayezungumza kiswahiri fasaha alimwita Mwanye  jukwaani na kumtumia kama mfano kwenye sehemu ya mahubiri yake akisema.

”Tutafanikiwa kwenda mbingini kwa njia moja tu ya Yesu kristo aliyemwaga damu yake kutukomboa sisi.

Hivyo mali zetu, Umaarufu wetu, Vyeo vyetu, Wazazi wetu vyote hivyo haviwezi kutupeleka mbinguni , huyu ni Mwanangu wa kwanza anaitwa David hawezi kuingia mbinguni  kwa sababu mimi baba yake ni Mchungaji hapa haiko hivyo  ataingia mbinguni kwa matendo yake mema na kuivaa damu ya yesu iliyomwagika pale Msalabani”alisema mchungaji huyo huku akimvisha mwanae huyo  joho  linalofanana na damu.

Wakati mahuri hayo yakiendelea wanakwaya wa kanisani hilo kutoka Marekani waliotinga kwenye   Tamasha hilo kulinogesha kwa njio za kiswahiri,kwa muda wote wa dakika 15 za mahuribi hayo walichutama makundi makundi huku wakishikana mikono wakifuatilia mahubiri hayo yaliyotolewa kwa lugha ya kiswahiri ambayo hawaifahamu ingawa waliimba nyimbo kadhaa kwa lugha hiyo hadhimu ya kiswahiri.

Hali hiyo ilimsukuma Mwandishi wa habari hizi kuzungumz ana mmoja wawanakwaya hao, ambaye amesema huo ndio umamaduni wao  wakati wa mahubiri wanaacha kila kitu na kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa utii wa hali wa juu.

Baadae Mtandao huu utarusha picha za matukio mbali mbali ya mchezo wa soka kati ya timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni’KMC’ dhidi ya timu ya kanisani hilo kutoka Marekani.

 Hivyo nakushihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kwa mabari Moto moto za chini ya kapeti

Wednesday, July 24, 2024

JEZI MYA YA SIMBU NI UBAYA UBWELA INAWEZA KUMTISHA MTU AGOST 8




 

JEZI Mpya ya Simba iliyozinduliwa jana ndani ya Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi Morogoro ikishuhudiwa na mkuu wa mbuga hiyo Mnyama Simba ni Ubaya Ubwela.

Agost 8 Mtu naweza kushangaa ubora wa jezi hizo na kujikuta  linachezea kichapo cha Mbwa Mwizi.

Ukali wa Uzi huo unaweza kumvisha Mshenga akaenda Ukweli kupeleka barua ya posa na kujikuta akazwadi mke Free Mandela. Waluguru wanasema Ubaya Ubwela, wakiwa na Maana Ubaya umeludi.

Je hiyo Agost 8  ubaya utaludi au kirefu kifungashio cha 5 G kitaendelea na kukata ngebe hizo za Ubaya Ubwela tusubiri tuone?

Mabango yenye Jumbe tofauti tofauti

           Mabango yenye Jumbe tofauti tofauti





 

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...