Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 5, 2024

UCHAGUZI MKUU SHUJAA NDU.GU WA SIMBA, KIONGOZI YANGA ATUPA DONGO.


Tawi la Shujaa ndugu wa Simba likiwa jirani kabisa na tawi kuu la Yanga linaloonekana kule mbele.

Tangazo lenye majina ya wagombea ambalo lilibandikwa makao makuu ya Shujaa ndugu wa Simba.

 

       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KIONGOZI wa tawi kuu la Yanga mkoani Morogoro Shaban Daud Abdallah Maarufu ‘Shaban Mabaskeli’ametupa dongo zito kwenye uchaguzi Mkuu wa wanachama wa timu ya Shujaa ndugu wa Simba.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi mara baada ya kutamatika kwa uchaguzi huo uliofanyika June 2 makao makuu ya Shujaa yaliyopo  Mtaa wa Fumilwa ‘B’kata ya Mji Mpya jirani na tawi kuu la Yanga, Shabani alisema.

”Kama unavyojua Shujaa ndugu wa Simba wamefungua ofisi  jirani  na tawi letu  tunatenganishwa na nyumba mbili tu.

Mimi mara kwa mara huwa nakwenda kwenye tawi lao kucheza mchezo wa Dhumna nilipofika nimesoma tangazo wagombea  nafasi zote nyeti kuna mtu mmoja moja hawana wapinzania isipokuwa eneo la wajumbe ndio kulikuwa na upinzania”alisema Shanani na kuongeza.

“ Watani zetu Simba wametumia pesa nyingi kuandaa uchaguzi huo ambao kwangu mimi ulikuwa sio uchaguzi walifanya mkutano wa kuwapitisha hao viongozi walioteuliwa na wazee wa Shujaa”alimalizia kusema Shabani ambaye ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya tawi kuu la Yanga Mkoani Morogoro.

Mara baada ya kupiga dongo hilo Mwandishi wa Mtandao huu alimbana kiongozi kuhusiana na dongo lake hilo.

Mwandishi. Unajua kwamba tawi hilo limegawanyika hivi karibuni baada ya  mgogoro na wenzao wa Shujaa tawi la Simba Ngome kubwa?

Shabani. Najua vizuri na mgogoro huo uliosababisha wapelekena pale kituo cha Polisi Mji Mpya.

Mwandishi. Sasa kama unajua hivyo baada ya Wazee waasisi wa timu ya Shujaa ndugu ya Simba kujiondoa kwenye tawi la Shujaa Ngome kuu na kufufua timu yao ya Shujaa ndugu wa Simba na wazee hao kuteua viongozi wa muda kuongozi timu hiyo kwa muda wa takribani siku 90 kabla ya kuitisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi wawanachama uliofanyika jana June 2.

Taarifa nilizonazo viongozi hao wateule  kwa muda huo waliokaa madarakani  wamefanya mambo makubwa yakiwemo kurejesha baadhi ya mali za timu hiyo hivyo kwa mafanikio hayo wanachama kwa kauli moja waliamua kuwaacha viongozi hao kuendelea na madaraka kwa kutochukua fomu za kuwapinga.

Shabani. Kwa maelezo yako nafuta kauli yangu kazi iendelee

Mwandishi. Asante kwa kunielewa je nyinyi yanga uchaguzi wa tawi lengu mnafanya lini tena?

Shabani. Bado kidogo Shekidele siku ikifika tutakualika uje kuchukua habari

                         

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...