Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, June 4, 2024

MWANACHAMA SIMBA AJITOLEA UNUNUZI WA BASI.

  Mwanachama wa Simba Eleman Haule akizungumza kwenye Mkutano huo.
......Mwenyekiti wa Shujaa ndugu wa Simba Saulos Gelord Maunda akimjibu Haule

 ...Haule akizidi kusisitiza ahadi yake ya kuchangia ununuzi wa basi


        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

HII IMEKAA POA SANA.

Mwanachama wa Simba kutoka kundi la Shujaa ndugu wa Simba la mkoani Morogoro Eleman Haule amejitolea kuchangia ununuzi wa basi dogo’Coaster’ kwa lengo kuisaoti timu yao ya Simba kwenye michezo ya Mikoani na ile ya nyumbani.

Haule ambeye ni mmoja wa wadhamini wa Simba, alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa timu ya Shujaa ndugu wa Simba uliofanyika makao makuu wa timu hiyo eneo la Kaloleni kata ya Mji Mpya.

”Binafsi naipenda sana Simba inapofungwa naumia sana, lakini niwatie moyo haya tunayoyapitia kwa sasa kwenye timu yetu yatapita ombi langu kwa wanachama wenzangu  tuendelea kuisapoti timu yetu kwenye nyakati zote nzuri na ngumu”alisema Haule na kuongeza.

Binafsi Simba kila inapocheza mimi naweka mafuta gari langu na kwenda na rafiki yangu huyu Mjumbe Jackson Nchimbi, ambaye kwenye nusu fainali ya F.A Simba ilipocheza na Azam kule Songea tulikwenda.

Kama hiyo haitoshi  Simba ilipocheza na Yanga kwenye nusu fainali nyingine ya F.A kule Mwanza pia tulikwenda.

Ombi langu kwenu nyinyi viongozi wetu tuhamasishane tununue usafiri wetu wa tawi tunashindwa nini?

Mbona wenzetu wa matawi ya Mbeya kule Tunduma wana Coaster zao kila ninapokwenda mikoani na kutana nao wanakuja na Coaster yao yenye neno za tawi lao kuisapoti Simba, Sasa kwenye hili mimi niko tayari kuchangia million mbili”alisema Haule na kushangiliwa na kundi la wanachama wenzie.

 Mwenyekiti Mpya wa Shujaa ndugu wa Simba Saulos Maunda alisema wamelipokea wazo hilo zuri na watalifanyia kazi kabla kipindi chao cha uongozi kutamatika.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...