Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 7, 2024

MWANDISHI WA HABARI WA MAGAZETI YA SERIKALI AFIWA NA MUME WAKE.

                            Hayati Kubwa enzi za Uhai wake
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa nyumbani kwa marehemu wakiusubiri mwili, kwa mbali Mwandishi wa Mtandao huu ana onekana nyuma mwenye shati nyeupe na miwani ya giza kama anakwenda kuchomelea vyuma.

Mwili ukishushwa kwenye gari ukitokea Muhimbili Dar es salaam


Mwandishi wa habari Mwandamizi wa Magazeti ya Mwananachi Hamida Shariff’Mwenye dera la khanga ’akimpokea Mwandishi mwenzake na kumfariji kwa kuondokewa na Mpendwa baba watoto wake.


INA UMA SANA.
Mara baada ya jeneza lililobeba mwili wa hayati KLulwa kuingizwa ndani likitokea Muhimbili,
watoto wa matehmu waliyezoea kumuona baba yao yakiingia ndani akiwa hai, waliangua vilio baada ya kuliona jeneza lililobeba mwili wa mpendwa baba yao likiingizwa ndani



......Mwili ukitolewa ndani na kuweka kwenye eneo maalumu njje ya nyumba hiyo


......Angness na wanae wakiwa katika majonzi makubwa ya kuondokewa na baba yao wa familia

Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ Thadei Hafigwa akiwasilisha rambi rambi za Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.

                      

                        Votunata akifarijiwa na mtoto mwenzake
        ...Baadhi ya waandishi wa habari wakimfariji mwenzao

 lbada ikienda kanini kuu la Mt  Patrick jana majira ya saa mbili usiku


     Na Dustan Shekidele,Morogoro.   

MWANDISHI wa habari Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali Mkoani Morogoro Agness Haule, amefiwa na Mpendwa Mume wake hayati Silvery Kulwa Valentine[56].

Hayati Kulwa ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Koo iliyopo Mikese Stesheni Wilaya ya Morogoro Vijijini, amefariki dunia June 2 hospital ya Taifa Muhimbili  Dar es salaam alipolazwa akipatiwa matibabu ya maradhi yalioyokuwa wakimsumbua.

Mwili wa‘Ticha’ Kulwa uliwasili Morogoro jana majira ya saa 12 jioni ukitokea Muhimbili, baada ya kushushwa kwenye gari mwili huo uliingizwa ndani ya nyumba yake iliyopo Kijiji cha Pangawe Jeshini eneo la kwa Mkorea, ukisindikizwa na mpendwa mke wake aliyekuwa akimuuguza huko Muhimbili.

Kama ilivyo ada baada ya dakika kadhaa  Mwili  ulitolewa nje,na wananchi mbali mbali walipata nafasi ya kuwasilisha rambirambi zao kwa familia.

Baada ya zoezi hilo kukamilika majira ya saa moja usiku, safari ya kuelekea Mjini kanisa kuu la  Mt Patrick llinza kwa msafara ulioongozwa na Pikipiki ya Mwandishi wa habari hizi.

Baada ya lbada hiyo ya kumuombea marehemu kukamilika majira ya saa tatu kasoro usiku safari ya kuelekea mkoani Shinyanga Kijiji cha Soka Soka Mehatu ilianza.

Leo mpendwa wetu Kulwa anatarajiwa kupunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele Kijijini kwao Mehatu.

Mwalimu kulwa ameacha Watoto watatu ambao ni  Alex, Anjera na Votunatha na Mjane Angness Haule ambaye ni Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Habari Leo Mkoani Morogoro linalomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.  

“Mwendo Umeumaliza ‘Shemeji’Nenda salaama  tutaonana baadae”.

“Bwana ametoa na Bwana ametwa Jina lake lihimidiwe” Ameni.

                      

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...