Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 3, 2024

NDUGU WA SIMBA WAPATA VIONGOZI WAPYA.




                                                              Saulos Maunda.

Mwenyekiti Mwenyekiti wa timu ya Shujaa ndugu wa Simba

Hasshim Mdoe ambaye ni mmoja wa makanda wa Scaut Mkoa wa Morogoro alichaguwa kuwa makamo Mwenyekiti

Ustadh Abshir Moro,alichakuwa kuwa katibui Mkuu wa Shujaa ndugu wa Simba
Majuto Mdoe aichaguliwa kuwa katibu Mkuu Msaidizi

Mara nyingi kitengo cha pesa anakuwa mtu mmoja tu.

Shabani Mkosasura ndiye aliyechaguliwa kutunza fedha za shujaa marafiki wa simba

 Wajumbe wanne wa kamati ya uterndaji ni Christina Jabir [Mama Ramadhan]Mjumbe

             Mohamed Mahinda  Mjumbe
                                 Amina Hassan Mjumbe
                             Jackson Nchimbi Mjumbe

Katibu Mkuu wa MRFA Jimmy Lengwe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa Shujaa ndugu wa simba.


Mgeni rasmi katibu Mkuu wa chama cha soka Mkoa wa Morogoro Jimmy Lengwe akizungumza mara baada ya viongozi hao kuchaguliwa jana



 


  Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Shujaa Sports Club yenye maskani yake Mkoani Morogoro ambayo ni ndugu wa ‘damu’ wa Simba, jana wamefanya uchaguzi mkuu na kufanikiwa kupata Viongozi wapya walioahidi kuendelea kuwasapoti ndugu zao wa Simba kwa asilimia mia moja.

 Uchaguzi huo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Jimmy Lengwe umefanyika jana Makao Makuu ya timu hiyo Mtaa wa Fumilwa ‘B’Kata ya Mji Mpya  kwenye Mjengo wa familia ya Mlanzi ambao sehemu kubwa ya familia hiyo ni Simba lia lia.

 Ikumbukwe hivi karibuni Mtandao huu uliripoti taarifa za timu hiyo ya shujaa kuingia kwenye mgogoro mkubwa uliopelekea kugawanyika kwa makundi Mawili.

Makundi hayo ni Shujaa ndugu wa Simba na Shujaa tawi la Simba ‘Ngume Kuu’awari makundi haya  yalikuwa kitu kimoja wakiwa na ofisi yao Jengo la CCM Kata ya Mji Mpya.

Baada ya Mgogo huo kuibuka hasa timu yao ya Simba ilipofungwa bao 2-0 na Tanzania Prinson kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Tawi la Shujaa Ngome kuu likikabidhiwa timu na Uongozi wa Simba makao makuui, baada ya uongozi huo kutangaza kuutumia uwanja wa Jamhuri kwenye mechi zake zote zilizosaria za Ligi kuu kufuatia uwanja wa Mkapa kufungwa na serikali kwa ukarabati mkubwa.

lnadai baada Simba kubaini hali hiyo ya wenyeji wao kugombana waliamua kuhama Morogoro na kuirejesha timu Dar es salaam.

Baada ya timu kuondoka moto ulizidi kuwaka ambapo makundi hayo mawili yaliingia kwenye vita kali ya maneno baadae wakaingia kwenye vita za kugombea Mali za tawi hali iliyolekea kufikishana  Kituo cha Polisi Kata ya Mji Mpya.

 Shujaa ndugu wa Simba inayoongozwa na wazee waasisi wa timu hiyo walishinda kesi na kukabidhi mali hizo.

Akizungumza jana kwenye mkutano huo wa Mmoja wa  waasisi wa timu hiyo wa Shujaa Mzee Sudi Kiwamba alisema, wamefanikiwa kurejesha Kibanda cha biashara kilichopo ndani ya Stend ya daladala ya Kaloleni iliyopo kata ya Mji Mpya.

Pia wamefanikiwa kukabidhiwa Uwanja wa Soka wa Shujaa uliopo  kata ya Mji Mpya pamoja na nyaraka halisi za usajiri wa timu hiyo.

 Awari mali zote hizo vilikuwa vikimilikiwa na Uongozi wa Shujaa tawi la Simba Ngome Kuu chini ya Uongozi wa Mwenyekiti Said Mkwinda aliyechaguliwa kihalali na wanachama zote wa shujaa ndugu wa Simba na Shujaa tawi la Simba.  

Hivyo baada ya Shujaa ndugu wa Simba kujitenge na Shujaa tawi la Simba wazee wa asisi wa timu ya Shujaa ndugu wa Simba waliteua uongozi wa Muda ulidumu madarakani kwa takribani miezi 3 kabla ya jana kuthibishwa kwa kuchaguliwa kwa kura na wanachama wa tawi hilo. 

    SAFU HIYO YA UONGOZI IKO HIVI.

Mwenyekiti ni Saulos Maunda.

Makamo mwenyekiti, Hashimu.Mdoe.

Katibu Mkuu. Abshir Moto.

Katibu Msaidizi.Majuto Mdoe.

Mtunza fedha’Mhazini’ Shabani Mkosasura.

Wajumbe 4 wa kamati ya Utendaji.

1]Mohamed Mahinda.

2]Amina Hassan.

3]Jackson Nchimbi.

4]Christina Jabiri ’Mama Rama’ Akizungumza na safu hiyo mpya ya uongozi Katibu Mkuu wa [MRFA]Jimmy Lengwe aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha wanamaliza mgogoro huo.

“Niwapongeze kwa kuchaguliwa kuongoza taasisi hiyo ya Shujaa ndugu wa Simba, ombi langu kwenu tena ikiwezekana lianze kesho hakikishine mnamaliza tatizo na wale ndugu zenu wa Shujaa tawi la Simba, kimsingi sisi kama chama hili litatuchanganya kuwa na makundi mawili yanayotumia jina moja”alisema Lengwe.

 Kama kawaida kwenye mkutano huu Mwandishi wa habari hizi amekusanya matukio kibao likiwemo tukio la mwanachama mmoja wa tawi hilo ‘mwenye maokoto yake’kujitoa kutoa pesa za kusaidi tawi  la Shujaa ndugu wa Simba kununua basi dogo ‘Coaster’ itakayo wasafirisha wanachama kwenda mikoani kuisapoti timu yao ya Simba.

Tukio la pili tawi hilo ,a shujaa ndugu wa Simba wapo jirani kabisa na watani za tawi kuu la Yanga la Mkoani Morogoro wanatengenishwa na nyumba 2 pekee. Hivyo baada ya kusoma majina ya wagombea wa tawi hilo yamebandikwa ukutani kiongozi huyo wa tawi la Yanga kawatupia dogo viongozi hao.

 Habari zote hizo  zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...