Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 2, 2024

SOMO LA JUMAPILI. MADA.HUSIKA NI JINSI TUNAVYOKOSEA KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU.


 

   

Na Mtumishi wa Mungu. Dustan Peter Shekidele.

Nawasalimu katika jina kuu la Mwenyezi Mungu, asiyelinganishwa wala kufananishwa na kitu chochote hapa duniania na huko Mbinguni. Ama baada ya salamu tuingie kwenye somo letu la Leo tukikumbushana mambo mbali mbali .

Lengo kuu ni kukumbushana juu ya maombi yetu kwa Mungu, wengi wetu hatujibiwi maombi yetu kwa sababu tunakosea kuomba,  wengine tunapomuomba  hatuna tubra hivyo tusipojibiwa kwa wakati tunakata tamaa na kumuhasio Mungu, tunapeleka matatizo yetu kwa waganga wa kienyeji ambao kimsingi ni binadamu wenzetu walioumbwa na huyo Mungu tuliyemuasi.

Hapo baada ya kutatua tatizo tunazidisha tatizo kwani naamini kwa kufanya hivyo ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu.

Nilimsoma Ayubu kwenye Biblia alipata majaribu mengi ikiwemo kuota majibu Mwili mzima aliomba sana bila majibu. Watu wengi walimsihi akiwemo mkewe kwamba achane na maombi Mbona huyu Mungu anayemuomba ajibu matatizo yake?.

Ayubu alimjibu mke na wote walimkatisha tamaama akiwaambia” Mnataka Mungu awape mema tu mabaya yampate nani.?  

Kauli hiyo ya Mamlaka ilimziba mdomo mke wa ayubu na wote walimtaka kumtenganisha na Mungu kupitia matatizo anayopitia.

                KUKOSEA KUOMBA.

Kwenye hili la kukosea kuomba ninanifano Mingi  leo nitoe mfano mmoja tu wa jinsi tunavyokosea kumuomba Mwenyezi Mungu.

 Iko hivi Mfano mtu amefikia umri wa kuoa au kuolewa anaamua kuingia kwenye Maombi Mungu ampe mtu sahihi kwenye maisha yake mapya ya ndoa.

Naanza kuomba hivi.

” Hee Mwenyezi Mungu nakuomba unipe [Mke\Mume] bora, nimeamua kukushirikisha  kwenye jambo hili nyeti nikiamini kwa akili na uwezo wangu siwezi kupata majibu ya hili bila kukushirikisha wewe.  amen”

Umeona muombaji huyu alivyokosea kuomba, hapa anamuamulu Mungu akavunje ndoa ya mtu mwingine ili apate Mume au Mke wa huyo mtu.

 Kwa ninavyojua mimi neno mke au Mume ni mtu ambaye tayari ameshaolewa au kuoa, akama hujaolewa uwezi kuitwa mke ia kama hujaoa huwezi kuitwa mume.

 Hivyo kwenye maombi yako Unaombaje Mungu akupe Mume au Mke wa mtu?.kwa maombi haya nahisi Mungu hawezi kwenda kuvunja ndoa ya mtu akupe wewe mke au mume muombe wako kwa usahihi atakupa.

Kwenye Maombi haya nahisi tungeomba hivi.

”Hee Mwenyezi Mungu nimefika umri wa kuoa au kuolewa naomba unipie mchumba sahihi atakaye kuwa mume\mke bora kwenye familia yetu.  

Sifa kuu ya huyo mchumba  ambaye baadae utatuunganisha kwenye ndoa kuwa mke na Mume awe mchamungu aliyejaa hofu ya Mungu.

Sitaangalia mali alizo nazo wala uzuri alionao nitaangalia tabia njema na Upendo wake kwako na kwangu ikiwezekana unipe yule [Sinia Bachera]  Mwenzangu’’ Amen.

Kwa maombi haya I believe ‘Naamini’ Mungu wetu ambaye ni msikivu atajibu maombi na kukupa mchumba ambaye baadae atakuwa mke au mume bora.   

Kwa msisitizo ili tujibiwe upesi unapoingia kwenye maombi, uwe msafi wa Mwili na roho kumbuka Mungu alimuambia Mussa pale mlimani kwamba vua viatu vyako unaingia sehemu takatifu.

Mungu hakumaanisha Viatu vya miguuni hapana alimaanisha  usafi wa Mwili na roho.

Kuna baadhi ya watu wanaingia kwenye maombi tena ndani ya nyumba za lbada simu zao zimejaa picha chafu sasa Mungu atajibu vimbi maombi yake ili hali unakumbatia mambo ya lbirisi Shetani.

Kwenye hilo Msanii wa nyimbo la lnjiri nchini Rose Muhando alilidadavua vizuri kwenye wimbo wake ‘vua kiatu’

Kwa leo naishia hapa, Mungu akiendelea kunipa zawaidi ya uhai tutakutana Jumapili kwa madai nyingine .



No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...