KUMBUKUMBU LA TORATI 28;7-10
“BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako,watakutokea kwa njia moja,lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako,na mambo yote utakayo yatia mkono wako,naye atakubarikia katika nchi akupayo bwana Mungu wako.
Bwana atakuweka uwe taifa,takatifu kwake kama alivyokuapia utakaposhika maagizo ya bwana Mungu wako na kutembea katika njia zake.
Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la bwana nao watakuwa na hofu kwako”
Hili ndilo neno letu la Leo Jumapili ya June 9. Mungu naalibariki neno lake na kutupa wepesi wa kulishika na kulifuata.
CAPTION.
Katika kazi ya Uandishi wa habari nimesafiri kwenye njia nyingi za hatari nikitafuta habari.
Namshukuru Mungu kwenye njia hizo zikimewe Mbugha za wanyama wakali, Milima na misitu mizito nikitumia usaifiri wa Pikipiki,i Bwana Mungu alinilinda kwenye safari zote hizo nimekwenda salama na kurejea salama.
Kufuatia hali hiyo Mtumishi mmoja wa Mungu Padre wa kanisani Katolini Jimbo la Morogoro aliamua kuifanyia maombi Maalumu Pikipiki hiyo sambamba na kuimwagia maji ya Baraka.
Padre huyo anayeongoza kanisani Katoliki Palokia ya Area Six alifanya hivyo akithamini mchango wa Mwandishi wa Mtandao huu anayejitoa kutafuta habara za kijamii Vijijini akiwasaidia wananchi wenye matatizo mbali mbali kupasa sauti zao kupitia yeye.
SHUKRANI.
Mtumishi wa Mungu Dustan Shekidele anamshukuru sana Padre huyo kw akutambua mchango wangu kwa jamii, jambo hilo linazidi kunitia moyo kufanya kazi kwa bidii kuwasaidia wananchi wenye uhitaji popote walipo kwenye Vijiji vyote vilivyomo ndani ya wilaya zote 7 za mkoa wa Morogoro.
Awari ndoto zangu zilikuwa niwe mwanasheria[Wakili]wa kuwatetea wananchi wasio na uwezo, wanaodhurumuwa haki zao. Baada ya kukosa nafasi hiyo ya kusomea uwakili kwa sababu za kiuchumi duni, niliamua kutimkia kwenye Uandishi wa habari hapako huku wazazi walimudu kunisomesha wakiwa na lengo la kutimiza ndoto zangu hizo.
Baadhi ya wananchi niliokutana nao waliniuliza swali wakisema
“ Shekidele nakufuatilia sana unajitoa sana kwenye matatizo ya wananchi unasaifiri maeneo hatari kwa pikipiki ukifuata habari za wananchi wenye uhitaji wa Vijijini.
Kila Mwaka tunashuhudia tuzo za Waandishi wa habari zikitolewa wanachukua waandishi wahabari wengine tena wengi wao wa Dar es salaam, wewe hatujasikia hata mwaka mmoja ukipewa tuzo hizo, samahini lani kwa swali hilo ambalo kwa muda mrefu nilikuwa nalo moyoni”alisema Mwanchi huyo mkazi wa Morogoro.
MAJIBU YANGU KWAKE.
Kwanza nashukuru sana kwa kutambua kazi ninazo fanya kwa jamii ya watu wenye uhitaji, hii inanitia moyo wa kuendelea kufanya hivyo.
Hata Mungu alisema mtu akimaliza kazi nitamvisha taji, kwa kauli yako hiyo naichukua kama umenivisha taji.
Nikijibu swali lako la msingi ni kweli sijapewa tuzo, na waandaji wa tuzo hizo hawana makosa yoyote kwa kutonipa tuzo hizo.
Utaratibu wa tuzo zile kila Mwandishi anatakiwa kutuma kazi alizofanya kwenye kamati ya tuzo ambao kamati hiyo inazichambua kazi zote hizo na mwisho wa siku wanatangazwa washindi.
Kwangu mimi huwa sipeleki kazi zangu kwa sababu kazi ninayoifanya ni ya wito,
Hivyo siifanya kwa sababu ya kupewa tuzo na Mwanadamu nafanya kwa lengo la kupewa tuzo kubwa na Mungu aliyenituma kufanya kazi yake ya kupaza sauti kwa wasio na sauti.
Mfano pichani Msafiri Jeremia Mkazi wa Kilosa alikuwa akifanya biashara stesheni ya Treni Kilosa.Kuna abiria alinunua machungwa kwake sasa alipohangaika kutoa pesa kwenye pochi Treni imeanza kuondoka.
Mama huyo kwa sababu alikuwa na moyo wa lmani kachungulia dirishani kamdongoshea elfu moja Jeremia alivyoinama kuokota pesa hiyo kwa bahati mbaya katereza na kujikuta mguu wa kushoto na mkono vimeangukia kwenye Reli na kukatwa na tairi za chuma za Treni hiyo. Jeremia baba wa familia ya wawatoto 4 na mke mmoja anayetegemewa na familia hiyo amekosa utafutaji wa chakula cha familia.
Pongezi nyingi kwa mkewe licha ya Mumewe kupata changamoto hiyo hakumkimbia na badala yake alibeba yeye jukumu la kurisha familia kwa kwenda kufanya vibarua vya kufua nguo kwa majirani na kulima. Kufuatia hali baadhi ya wananchi wa Kilosa walitoa taarifa kwa Mwandishi wa habari hizi ambaye alipigia gia pikipiki yake hadi Kilosa na kuzungunza na familia hiyo.
Baada ya mahojiano hayo habari hiyo ya kuhudhunisha ilitoka kwenye gazeti la ljumaa ambapo wananchi wengi kote Tanzania waliosoma habari hiyo na kuguswa walimchangia mrefu huyo kiasi cha shilingi laki 6 kupitia namba za simu za Mwandishi huyo baada ya familia hiyo kukosa uwezo wa kumiliki simu hata ya kiswaswadu.
Mke wa Jeremia akumshukuru Mungu wakati Mwandishi wa habari hizi akimkabidhi pesa hizo Mumewe, kama hivyo haitoshi
Mwandishi wa habari hizi alizungunza na Afisa Usatawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Mzee Ngunga Mtitu ambaye alikubari Ombi la Mwandishi huyo la kumpokea Jeremia kwenye Kambi ya wazee na walemavu ya Funga Funga iliyopo Mji mpya Manisapa ya Morogoro yalipofanyika makabidhiano ya Pesa hizo.
Baada ya gazeti hilo kutoka Uongozi wa Radio Clous kupitia kipindi chao kiele cha mambo ya Jamii kinacholuka kila siku za Jumapili walimualika Jeremia studio Dar na kufanya naye mahojiano live.
Huko nako baadhi ya wannchi kusikiliza simulizi yake waliguswa na kuchangia pesa,ambao kwa sasa maisha yake walamu yanakwenda vizuri kufuatia sapoti hiyo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment