Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 12, 2024

HAKUNA SHABIKI YOYOTE TANZANIA WAKIWEMO WA SIMBA NA YANGA ALIYEFIKIA KIWANGO C HA USHABIKI CHA MWAMBA HUYU.


 

 

Licha ya kwamba ni zaidi ya miaka 17 toka Shabiki Maarufu nchini hayati Yamungu afariki dunia, Utafiti unaonyesha mpaka sasa hakuna shabiki yoyote hapa nchini wakiwemo wa timu kubwa za Simba, Yanga na Azam aliyefikia kiwango wa ushabiki wa hayati Yamungu aliyekuwa mwanachama na shabiki lia lia wa timu ya Reli ya Morogoro’ Marufu Reli Kiboko ya Vigogo.

Pichani hayati Yamungu akifanya mambo yake kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya  wenyeji Yanga dhidi ya Reli.

Katika mchezo huo wa Ligi kuu uliyopigwa uwanja wa Uhuru uliopo Kata ya Mgulani Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam  yanga ilipokea kichapa cha ‘kizalendo’ cha bao 1-0.

 Bao hilo pekee lilikata ‘ngebe’ za mashabiki wa Yanga waliokuwa wakimzodoa hayati Yamungu uwanjani lilifungwa na mshambuliaji hatari wa Reli David Mihambo’Munyamwezi’ kutoka Utambo Tabora,akiungamisha krosi ya wimba Mbuyi Yondani ‘Faiter’ Msukuma wa Mwanza ambaye ni baba mdogo wa beki wa zamani wa Yanga Calvin  Yondani, ambaye  kwa sasa anakipiga Geita Gold iliyoshuka daraja msimu huu.  

Mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya kabrini Mpendwa wetu Yamungu.ambaye baadae alibadili dini akitoka kwenye dini ya Ukristo na Kujiunga na dini ya Kiislamu.

Baada ya kusilimu Mzee Yamungu alipewa jina jipya la Hamza, ambapo hadi anakutwa na umati alikuwa kwenye dini hiyo ya kiislamu.

 Tutakumbuka daima Mpendwa wetu Yamungu mimi rafiki yako tuliozunguka Mikoa mbali mbali na timu yetu ya Reli, pamoja na wanao Hawa na Shabani tunaendelea kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akusamehe Mkosa yako na akuweke unapostahili.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...