Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 30, 2024

AJALI. MAMA ALIYETOKA HOSPITAL KUJIFUNGUA IMENUSIKALI KIFO NA KICHANGA CHAKE, BAADA YA BAJAJ KUPINDUKA KWENYE KORONGO .











 


    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

ACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Mama mmoja aliyetoka ‘Reba’ hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kujifungua, amenusulika kifo na Kichanga chake baada ya Bajaj waliyoikodi kupinduka mara mbili eneo la Mji Mpya Mkoani hapa.

Ajali hiyo iliyoshuhudiwa ‘Live’ na Mwandishi wa habari hizi imetokea jana Mchana kwenye korongo la njia isiyo rasmi, kufuatia njia rasmi ya Mji Mpya inayoelekea Kichangani kufungwa kupisha matengenezo.  

Madereva wengi akiwemo huyo wa Bajaj huchepuka kwenye njia  ya panya kukwepa adha ya kuzunguka  njia mbadara ya Masika kutokea ofisi za Tanesco Mkoa wa Morogoro.

Dereva huyo  ilipojaribu kushuka kwenye korongo hilo huku akiwa na mzazi huyo aliyepakata kichanga chenye umri wa siku moja alijikuta akiporoboka jumla na Bajaj kubimbilika kama boga linanaloshuka milima ya Uluguru.

  Mwanahabari wa Mtandao huu aliyekuwa mtaani kusaka matukio ulishuhudia wananchi  wakivamia eneo la tukio na kumchomoa Mzazi huyo na kichanga chake.

  Mama huyo alipohojiwa alisema.” Nimetoka Reba muda huu baada ya kuruhusiwa nimekodi hii Bajaj kwa bahati mbaya tulipofika hapa kwenye Korongo kibajaj nimepinduka mara mbili wakati kina bimbilika nilimkumbatia mwanangu na bimbilika naye Mungu ni mwema hakumia ila mimi najisikia maumivu kwenye mbavu na mkono”alisema Mama huyo .

 Mwandishi wa habari hizi alimshauri  kuludi tena hospital kwa ukaguzi wa afya yake na ya kichanga,  alikubali ushauri huyo na kurejea hospital kwa kutumia Bajaj hiyo ambayo baada ya kupinduka wasamalia wema waliinyanyua.

Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Kitatu Aman Manzuli anayefanya biashara ya kuchoma mahindi mabichi eneo hilo alisema.

”Ndugu Mwandishi tunashangaa hii barabara imekamilika muda mrefu kwa kiwango cha zege Mwenge umepita mwezi wa 4 na kuizindua lakini wahusika hawaifungui.

Gari, Bajaj na boda boda zinalazimika kushuka kwenye korongo linalosababisha ajali mara kwa mara ”alisema shuhuda huyo na kuongeza.

“ Muda huu nimeshuhudia kibajaji hiki kikipinduka mara mbili tulivyokimbia masikini ya mungu kumbe kilimbeba mzazi aliyetoka reba kujifungua Mungu ni mwema huyo mzazi alikaa katikati na kichanga chake kulia na kushoto kulikuwa na ndugu zake hivyo wakati Bajaj inabimbilika mama kang’ang’ania kichanga chake mwanzo mwishi achema mama aitwe mama.

 Kabla ya kunyanyua Bajaj tulimpokea mama kichanga na baadae tukamchomoa  yeye kisha tukakiinyanyua Kibajaj”alisema Muza mahindi huyo.

Pichani baadhi ya wananchi wengi wao wakiwa kina mama wakimfariji  mwanamke wenzao huku wakikikagua kicganga hicho.

Saturday, June 29, 2024

BREAKING NEWS .BAJAJ ILIYOMBEBA MAMA ALIYETOKA HOSPITAL KUJIFUNGUA IMEINDUKA

 

Bajaj iliyobeba mzazi aliyetoka Reba kujifungua imepinduka jioni ya leo maeneo ya Mji Mpya

Habari kamili ya hali ya Mama na kichanga itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao pendwa wa shekidele muda wote.

MABOMU YA LINDIMA MICHUANO YA NDONDO CUP.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro Aristo Niktas akikagua timu ya Damu chafu
                ......Akisalimiana na wachezaji wa Wakushi
........Mgeni Rasmi akiwa na Mratibu wa Nondo Cu Warda Makongwa
........Mgeni rasmi akizungunz ana wachezaji wa timu zote mbili
....Warda Makongwa naye akitoa neno kwa wacheaji hao
 Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Michezo Planet Radio Alen Mwinyi’Mpemba wa Chake chake’ aliyekuwa Mc kwenye gemu hiyo akiwasikilia viongozi wake kwa umakini huku akiwa amefunga swala.
                                                    Kikosi cha Wakushi

                             Kikosi cha Damu Chafu


           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

VULUGU kubwa imeibuka  kwenye mchezo wa Nusu fainali ya michuano ya ndondo Cup, hali iliyopelekea Polisi kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa timu za Damu Chafu Fc na Wakushi Fc waliotwangana makonde Kavu kavu.

Chanzo cha ugomvi huo kilianzia gori la kaskanini mwa uwanja wa Saba saba,  mashabiki wa Wakushi walitika eneo hilo kuwaondola mashabiki wa Wakushi, ambao waligoma kutoka hali iliyoibua mashabiki hao kutwangana makonde.

Polisi wenye Mbwa walitika eneo hilo na kuwamulu mashabiki hao kuacha mapigano,kufuatia wingi wa mashabiki hao walizidiwa nguvu polisi.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya afisa wa Polisi mwenye cheo cha nyota moja aliwaamulku vijana wake kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya mashbaiki hao.

 Fasta Maafande hao walitii amri ya bosi wao walichomoa mabomu hayo waliokuwa wameyavaa kiunoni kama mkanda na kuyakodi kwenye mitutu kisha wakawaelekea moto mashabiki hao.

 Mashabiki hao walitawanyika kwa kutimua mbio kama swala huku wakifuta machozi yaliyazaliwahsa na moshi mkali wa mabomu  yao hapa chezea nguvu ya Polisi wewe.

Baada ya dakika 5 hali ilitulia na Mwamuzi mkongwe wa Ligi kuu Athuman Lazi ambaye pia ni Askali Polisi wa kikosi cha kuliliza ghasia[FFU]alipoliza kifili ya kuashiria mchezo  kuendelea.

Gemu hiyo ilitamatika kwa timu hizo zilizosheheni wachezaji wengi wa Ligi kuu na wengini kutoka Ligi kuu ya Afrika Kusini  kwa sale ya 0-0.

Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia mastaa wengini wa ligi kuu wakiwa jukwaani baadhi ya mastao hao ni Kibwana Shomari na Salumu Kihimbwa ‘Chuji’.

 Baada ya ligi mbali mbali kusimama wachezaji wengi wamereja nyumbani Morogoro kwa mapunziko, kabla ya ligi kuu kurejea Agost 8 kwa uzinduzi wa michezo ya Ngao ya Hisani Kati ya Simba na Yanga na Coastal Union na Azam.

Ili kupata mshindi mchezo huo timu  hizo zilielekea kwenye changamoto ya mikwaju ya Pelnaty ambapo Vijana wa Damu Chafu kutoka Mafisi, walifaniwa kutinga fainali  baada ya kufunga Pelnaty zote 5 huku Wakushi kutoka Manzewe wakikosa pelnaty Moja iliyopanguliwa na Kipa wa Damu Chafu.

 Kwa ushindi huo Damu Chafu inayosapotiwa na Mwana Morogoro mkazi wa Mafisa Kelvin John’Mbambe’ anayecheza soka la kulipwa Ulaya imeivua ubingwa  wa michuano hiyo  iliyoandaliwa na Uongozi wa Planet Radio ya mkoani Morogoro.

Fainali ya michuano hiyo imepangwa kupigwa ljumaa  ya Julai 5 kati ya Damu Chafu na Black Viba iliyotinga fainali baada ya kuichapa timu ngumu ya Black  People ‘Taifa la watu weusi’ kutoka ‘Jijinga’ kwa wajanja Mji Mpya  kwa chuma 2-1.

Bingwa wa michuano hiyo  atanyakua kitika cha shilingi milioni  4 huku mshindi wa pili akinyakua million 2.

Friday, June 28, 2024

UDAKUZ SPESHO. KIJANA MMOJA ADAIWA KUFARIKI DUNIA BAADA YA KUFAKAMIA POMBE KALI.

   Muonekana wa Mji wa Morogoro.picha hii Mdakuzi alipiga akiwa juu ya Milima wa Uluguru

Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.

Jana majira ya mchana Mdakuzi alipokea simu kutoka kwa mdau mmoja wa Mtandao huu[Jina kapuni kwa sababu za kiudakuzi] ambaye ni bingwa wa mapishi kwenye sherehe mbali mbali nchini.  

Baada ya Mdakuzi kuokea simu hiyo baba Lishe huyo alisema.

”Shekidele kuna tukio hapa Saba saba  jana jioni kuna vijana wawili waliweka bima ya kunywa pombe kali aina ya Double K 5 kwa mpigo.  

Kijana wa kwanza alianza kuzifakamia pombe hizo nasikia alipomaliza kichupa cha 4 kazimika na baadae inadaiwa amefariki dunia hivyo nenda eneo la tukio ukachukue habari”alisema Mkali huyo wa mapishi mkoani Morogoro. Wachunguzi wa mambo ya kilevi wanadai Ukali wa Double K moja ni sawa na kunywa bia 4.

Kama hivyo ni kweli basi jamaa kanywa bia 16 kwa mpigo.

 Wachunguzi wengine wa mambo waliingia kwenye ubishi wakidai mratibu wa shindano hilo anakesi ya kujibu kisheria, huku wengine wakipinga wakida mratibu huyo hana kesi ya kujibu wakidai muhisika amejiripua mwenyewe.

Kwa sasa  mdakuzi anaelekea eneo la tukio  kufuatilia kwa undani tukio hilo kama ni kweli limetokea, hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kujua ukweli wa tukio hilo.


 

Tuesday, June 25, 2024

WANAENDELEA KUWA WANYAMA AKIWEMO MKANDAJI.KIBU D




 

 

Hadi kufika leo wachezaji hawa akiwemo mwana Morogoro Mzamiru Yassin na Mkandaji wa makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo Dar.

Kibu Denis ‘Kibu D’ndio waliofanikiwa kutoboa na kusaini mikataba mipya ya kusalia unyamani.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...