Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, June 28, 2024

UDAKUZ SPESHO. KIJANA MMOJA ADAIWA KUFARIKI DUNIA BAADA YA KUFAKAMIA POMBE KALI.

   Muonekana wa Mji wa Morogoro.picha hii Mdakuzi alipiga akiwa juu ya Milima wa Uluguru

Na Mdakuzi Dustan Shekidele,Morogoro.

Jana majira ya mchana Mdakuzi alipokea simu kutoka kwa mdau mmoja wa Mtandao huu[Jina kapuni kwa sababu za kiudakuzi] ambaye ni bingwa wa mapishi kwenye sherehe mbali mbali nchini.  

Baada ya Mdakuzi kuokea simu hiyo baba Lishe huyo alisema.

”Shekidele kuna tukio hapa Saba saba  jana jioni kuna vijana wawili waliweka bima ya kunywa pombe kali aina ya Double K 5 kwa mpigo.  

Kijana wa kwanza alianza kuzifakamia pombe hizo nasikia alipomaliza kichupa cha 4 kazimika na baadae inadaiwa amefariki dunia hivyo nenda eneo la tukio ukachukue habari”alisema Mkali huyo wa mapishi mkoani Morogoro. Wachunguzi wa mambo ya kilevi wanadai Ukali wa Double K moja ni sawa na kunywa bia 4.

Kama hivyo ni kweli basi jamaa kanywa bia 16 kwa mpigo.

 Wachunguzi wengine wa mambo waliingia kwenye ubishi wakidai mratibu wa shindano hilo anakesi ya kujibu kisheria, huku wengine wakipinga wakida mratibu huyo hana kesi ya kujibu wakidai muhisika amejiripua mwenyewe.

Kwa sasa  mdakuzi anaelekea eneo la tukio  kufuatilia kwa undani tukio hilo kama ni kweli limetokea, hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kujua ukweli wa tukio hilo.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...