........Mgeni Rasmi akiwa na Mratibu wa Nondo Cu Warda Makongwa
........Mgeni rasmi akizungunz ana wachezaji wa timu zote mbili
....Warda Makongwa naye akitoa neno kwa wacheaji hao
Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Michezo Planet Radio Alen Mwinyi’Mpemba wa Chake chake’ aliyekuwa Mc kwenye gemu hiyo akiwasikilia viongozi wake kwa umakini huku akiwa amefunga swala. Kikosi cha Wakushi
Kikosi cha Damu Chafu
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
VULUGU kubwa imeibuka kwenye mchezo wa Nusu fainali ya michuano ya ndondo Cup, hali iliyopelekea Polisi kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa timu za Damu Chafu Fc na Wakushi Fc waliotwangana makonde Kavu kavu.
Chanzo cha ugomvi huo kilianzia gori la kaskanini mwa uwanja wa Saba saba, mashabiki wa Wakushi walitika eneo hilo kuwaondola mashabiki wa Wakushi, ambao waligoma kutoka hali iliyoibua mashabiki hao kutwangana makonde.
Polisi wenye Mbwa walitika eneo hilo na kuwamulu mashabiki hao kuacha mapigano,kufuatia wingi wa mashabiki hao walizidiwa nguvu polisi.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya afisa wa Polisi mwenye cheo cha nyota moja aliwaamulku vijana wake kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya mashbaiki hao.
Fasta Maafande hao walitii amri ya bosi wao walichomoa mabomu hayo waliokuwa wameyavaa kiunoni kama mkanda na kuyakodi kwenye mitutu kisha wakawaelekea moto mashabiki hao.
Mashabiki hao walitawanyika kwa kutimua mbio kama swala huku wakifuta machozi yaliyazaliwahsa na moshi mkali wa mabomu yao hapa chezea nguvu ya Polisi wewe.
Baada ya dakika 5 hali ilitulia na Mwamuzi mkongwe wa Ligi kuu Athuman Lazi ambaye pia ni Askali Polisi wa kikosi cha kuliliza ghasia[FFU]alipoliza kifili ya kuashiria mchezo kuendelea.
Gemu hiyo ilitamatika kwa timu hizo zilizosheheni wachezaji wengi wa Ligi kuu na wengini kutoka Ligi kuu ya Afrika Kusini kwa sale ya 0-0.
Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia mastaa wengini wa ligi kuu wakiwa jukwaani baadhi ya mastao hao ni Kibwana Shomari na Salumu Kihimbwa ‘Chuji’.
Baada ya ligi mbali mbali kusimama wachezaji wengi wamereja nyumbani Morogoro kwa mapunziko, kabla ya ligi kuu kurejea Agost 8 kwa uzinduzi wa michezo ya Ngao ya Hisani Kati ya Simba na Yanga na Coastal Union na Azam.
Ili kupata mshindi mchezo huo timu hizo zilielekea kwenye changamoto ya mikwaju ya Pelnaty ambapo Vijana wa Damu Chafu kutoka Mafisi, walifaniwa kutinga fainali baada ya kufunga Pelnaty zote 5 huku Wakushi kutoka Manzewe wakikosa pelnaty Moja iliyopanguliwa na Kipa wa Damu Chafu.
Kwa ushindi huo Damu Chafu inayosapotiwa na Mwana Morogoro mkazi wa Mafisa Kelvin John’Mbambe’ anayecheza soka la kulipwa Ulaya imeivua ubingwa wa michuano hiyo iliyoandaliwa na Uongozi wa Planet Radio ya mkoani Morogoro.
Fainali ya michuano hiyo imepangwa kupigwa ljumaa ya Julai 5 kati ya Damu Chafu na Black Viba iliyotinga fainali baada ya kuichapa timu ngumu ya Black People ‘Taifa la watu weusi’ kutoka ‘Jijinga’ kwa wajanja Mji Mpya kwa chuma 2-1.
Bingwa wa michuano hiyo atanyakua kitika cha shilingi milioni 4 huku mshindi wa pili akinyakua million 2.
No comments:
Post a Comment