ZABURI 91.14-16
“Kwa kuwa amekaza kunipenda,Nitamwokoa na kumweka palipo juu,Kwa kuwa amenijua jina langu.
Ataniita nami nitamwitikia nitakuwa pamoja naye taabuni,Nitamwokoa na kumtunza.
Kwa sku nyingi nitamshibisha,Nami nitamwonyesha Wokovu wangu ” Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili ya Mei 12. UCHAMBUZI.
Neno hili la Mungu linatufunidha kwamba ukienda Mungu kweli kweli naye anakupenda, na kukusaidia katika changamoto zxako zote za kimaisha.ia neno hili linatufundisha katika maisha yetu ya kimahusiano ukimpenda mtu kweli kweli naye atakuweka juu kwa kila jambo sambamba na kutunza na kukuhudumia kwa asilimia 100.
Ukimpa upendo wa kisanii atakushusha chini akijitoa na kukufanyia Usanii kwenye changamoto zako pindi utakapohitaji msaada wake,
Jaza upendo na wewe Ujazwe upendo.
Mpende akupendae asiye kupenda achana naye.
Kama umeweza kuacha kunyonya ziwa tamu la Mama yako, chakula kitamu na cha kwanza ulichoanza kukila na kunywa ulipofika hapa duniani.
lweje mtu mliyekutana naye ukubwani tena mitaani akuumize kichwa kiasi cha kujiaiza kwamba huwezi kuishi bila yeye hiyo ni kama kufuru, kuna maisha mengine baada ya kuachana.
Naomba nieleweke kusema hivi sina maana ya kuhamasisha watu kuachana hapana, tunapaswa kuvumiliana kwenye mahusiano yetu sambamba na kubebeana misalaba kwenye madhaifu yetu ya kibinadamu, kwani hapa chini ya jua hakuna mkamilifu sote tunamadhaifu, Mkamilifu ni mmoja tu Mwenyezi Mungu Pekee.
Lakini pia ifahamike sisi binadamu mioyo yetu sio ya jiwe kwamba haisikii maumivu hapana Mioyo yetu ni ya nyama inayosikia maumivu. Pia uvumilivu unakikomo hapa ndipo ambao namaanisha uvumilivu unaofika kimoja jua huyo uliyenaye sio ubavu wako kwa maani sio mume au mke uliyechaguliw ana Mungu,
‘Ume Left’ Msanii Dulla Makabila anawimbo wake unaosema ‘Na wewe pita kushoto’kwa hiyo huyo nayekumiza kila siku Mpishe apite kushoto.
Subiri atakaye kubari kupita kulia kwako siku zote za maisha yako ‘ubavu wako uliondaliwana na Mwenyezi Mungu’.
Subrani ni lbada Mitume yote inasema ‘Kila mwenye Subra yu pamoja na Mwenyezi Mungu.
Mtumishi wa Mungu leo nimechambua kwa maneno makali, niliowakwa wanisemehe, ifahamike dawa ni chungu lakini ni tiba. Mwenye masikio na asikie,
Mtume na nabii lssa, Yesu Kristo anabisha hodi katika Mlango wa Moyo wetu tumfungulie aingie tumfungulie ainge tusiifanye mioyo yetu kuwa migumu kama jiwe, tuache kiburi cha uhai na uzima tukumbuke siku yetu ya kuingia kaburini.
No comments:
Post a Comment