Mwandishi wa Mtandao huu [lkulia] akimkabidhi mifuko ya unga wa Sembe Bi Magreth Mkitunda anayemiliki kituo cha watoto yatima cha Mkitunda.
Hapa Kazi tu, Mlemavu Matama akishiriki kuchimba Msingi wa nyuimba yake iliyopo Kichangani Manispaa ya Morogoro
Mwandishi wa Mtandao huu naye akishiriki kuchimba msingi huo,Shekidele na Matama waliradhimika kuchimba msingi huo baada ya kukosa pesa cha kuwapa vibarua wa kufanya kazi hiyo,
.......Matama akipanga tofari za kuchoma baada ya msingi uliojengwa kwa tofari za njanja kukamilika
Mtama wakie nje ya mjengo wake
Mtama akiwa na mpendwa mke wake Bi Mau Said
meneja wa tigo mkoa wa Morogoro kushoto akinikabidhi simu kisha kuniunga bando la Mwaka mzima
.
LUKA 6-38.
“Wapeni watu vitu,nanyi mtapewa,kipimo cha kujaza na kushindiliwa,na kusukwa sukwa hata kumwagika,ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.
Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa”Hilo ndilo neno letu la leo jumapili ya Aprili 5.
CAPTION
Mwandishi wa Mtandao huu kidogo alichojaliwa na Mwenyezi Mungu aligawana na watu mbali mbali wenye uhitaji ,wakiwemo watoto yatima wa kituo cha Mkitunda Kihonda.
Kama hiyo haitoshi Mwandishi huyo alitumia taaluma yake ya Uandishi wa habari kuendesha harambee kwenye Mtandao Pendwa wa shekidele na kufanikiwa kununua kiwanja na kumjenge nyumba Mlemavu Mohamed Matama ambaye kwa sasa anaishi kwenye mjengo wake na kifahari na mpendwa mke wake.
Kipekee nawashukuru wadao wote wa Mtandao huu walioniunga mkono kufanikisha ujenzi wa nyumba ya ndugu yetu huyo ambaye awari alikuwa akiishi kwenye boma lenye changamoto ya choo. USHUHUDA
Wakati naanza jitihada za kutafuta kiwanja kisha kuanza ujenzi wa nyumba ya Matama, mwaka 2017 nikIhangaika kununua vifurushi vya tigo vilivyoniwezesha kupata Enternet ya kurusha habari kwenye mtandao huu za harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba hiyo.
Mwenyezi Mungu kanilipa mara dufu vifurushi hivyo, mwaka huyo huo nilipigiwa simu na meneja wa tigo mkoa wa morogoro, akinipa habari njema kwamba nimeibuka mshindi wa shinda la tigo la jaza ujazwe.
Nikamueleza mbona sijawahi kucheza bahati na sibu?Meneja huyo aliniambia kwa kununua vifurushi vya tigo moja kwa moja niliingia kwenye shindandano hilo la jaza ujazwe.
Big bos huyo wa tigo Mkoa kanialika ofisi za tigo na kunikabidhi simu janja ‘Smath Phone’ sambamba na Muda wa Maongezi na Enternet ya Mwaka msima.
Hivyo kwa mwaka mzima nilitumia bando la Enternet kuhamsisha wadau kuchangia ujenzi wa nyumbani hiyo kupitia mtandao pendwa wa shekidele.
Kama hiyo haitoshi kwa mwaka mzima nilipiga simu bure kuwasiria na wadau wa mtandao huu pande zote zai duniani niliulizia hadi walizotoa kwenye ujezi wa nyumba hiyo.
.
No comments:
Post a Comment