Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, May 5, 2024

RASMI MORO KIDS YAPANDA DARAJA LA PILI


 

 .

     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

YAMETIA, yametimia, ndio kauli sahihi kuitamka kwa wanachama na wapenzi wa timu ya Moro Kids, ambayo baada ya msoto wa miaka mingi ya kuzalisha wachezaji na kuwagawa kwa timu mbali mbali za Ligi kuu, Ligi daraja la kwanza na  daraja la Pili.

Hatimaye ‘Wana wa Paka’  jana wamepiga hatua moja mbele baada ya kufanikiwa kupanda daraja la pili msimu ujao unaotarajiwa kuanza  mwenzi wa 9 mwaka huu.

 Moro Kids imefanikiwa kupanda daraja  baada ya wapinzao wao Kurugenzi ya Shinyanga kushindwa kutokea jana kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Kambarage huku wapinzani wao Moro Kids waliosafiri kutoka Morogoro hadi Shinyanga wakijikuta wako wenyewe uwanjani huku wenyeji wao wakiingia mitini kwa mara ya pili mfurulizo.

lkumbukwe kwenye mchezo wa kwanza wa Play Off kati ya Moro Kids na Kurugenzi uliopagwa kufanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro Aprili 27 Wasukuma hao kutoka shinyanga hawakutokea uwanjani na Moro Kids kupewa ushindi wa Pointi 3 na mabao 3.

 Mbali na Kurugenzi kupoteza mchezo huo pia ilipigwa faini ya milioni 3, sambamba na kulipa gharama za mchezo, kama hiyo haitoshi kamati hiyo ya masaa 72kwenye kikao chao cha jumanne iliyopita walitangaza kudai pointy 15 kwenye Ligi yoyote watakayo chezo.

 Licha ya adhabu hiuyo kamati hiyo ilipanga mchezo wa marejeano kati ya wenyeji Kurugenzi na Moro Kids uchezwe jana Mei 4.

Leo majira ya saa 5 asbuhi Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu katibu Mkuu wa Moro Kids Mzee Rajab Kindaguru kwa lengo la kujua matokeo wa mchezo huo .

”Wapinzani wetu hawakutokea  uwanjani hivyo tumepewa point nyingine tatu na kufanikiwa kupanda ligi daraja la Pili muda huu tuko njiani  tukirejea nyumbani Morogoro” alisema Kindagule na kuongeza .

” Kimsingi shekidele tunakushukuru sana ni Mwandishi wa habari pekee uliyeripoti michezo yetu mfurulizo toka ligi ya mabigwa wa mikoa kituo cha Pwani na kituo cha Dodoma na sasa kwenye mchezo ya Play Off umetufuatilia na kuripoti kwenye mtandao wako,wewe ni sehemu ya mafanikio hayo lnshallah kesho nitakutafuta”alisema Kigogo huyo wa Moro Kids.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...