Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MBUNGE Machachari wa Jimbo la Mikumi Mkoa Morogoro ambaye pia ni Mwenyekiti kamati ya kudumu ya Bunge’TAMISEMI’ Mhe Dennis Londo, Mwishoni mwa wiki amemtaja Mwanamuziki nguri duniani hayati Michael Jackson,wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROC’
Kabla ya kufungua mkutano huo uliofanyika Aprili 27 ukumbi wa JKTBwalo la Umwema Morogoro, Mbunge huyo alipata wasaa wa kuwahutubia Waandishi hao, ambapo kwenye hotuba yake hiyo aliwataka Wanahabari hao kufanya kazi zao kwa Weledi huku wakiweka utaifa mbele.
‘’Mfano kuna habari kubwa hapa mkoani kwetu Morogoro haijaandikwa, toka mauaji ya yaliyosababishwa na mapigano ya wakulima na wafugaji pale Ludewa Kilosa mwaka 2000,sasa tuko mwaka 2024,miaka 24 imepita hatujasikia tena mtu kufariki dunia kwa mapigano ya wakulima na wafungaji.
Kwa mkoa wetu wa Morogoro hayo ni mafanikio makubwa ambayo yalipaswa kuripotiwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari’’alisema Mbunge huyo ambaye jimbo lake la Mikumi lina pakana na jimbo la Kilosa linaliongowa na Mhe Mbunge
Profesa Kabudi.
AMTAJA HAYATI MICHAEL JACKSON.
Kabla ya kuhitimisha hotoba yake hiyo iliyojaa ‘Madini’ Mhe Londo aliwataka waandishi hao kujikita zaidi kuandika habari husika wanazosikuta eneo la tukio na si vinginevyo.
”Mfano Mwanamuziki Michael Jackson kwenye moja ya mahojiano yake na Vyombo vya habari enzi za uhai wake alisema.
Anamnukuu
“Muonekano wangu unauhusiano upi na Muziki wangu”?mwisho wa kunukuu.
Kwenye maelezo yake hayo Michael Jackson aliwataka Waandishi kote duniani kuangalia na kuripoti ‘Talent’kipaji chake cha kucheza na kuimba na sikutumia muda mwingi kuandika habari za muonekano wa sura yake”alisema Mbunge huyo.
MAJIBU YA MAELEZO HAYO YA JACKSON
lkumbukwe hayati Michael Jacksoni enzi za uhai wake alikuwa na mwanamuziki tajiri dunia hivyo alitumia utajiri huo kujipodoa na kujibadilisha sura kwa kuchonga pua,na kubadirisha muonekana wa ngozi na nywele zake.
Hivyo kwa waandishi wa habari kujikita zaidi kurioti tukio hilo la kujibadirisha sura kwa mwanamuziki huyo kwangu mimi naona wanahabari hao walikuwa sahihi.
Kitendo cha binadamu awaye yote kukosoa umbaji wa Mungu na kutumia utajiri wake kubadiri baadhi ya viongo vyake hiyo ni habari kubwa inayozidi habari ya kipaji cha kucheza na kuimba .
No comments:
Post a Comment