Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, May 19, 2024

UJUMBE WA NENO LA MUNGU RPC ACHANGIA UJENZI WA NYUMBA YA MLEMAVU

CAPTION.
Matama akiingiza Mifuko hiyo 5 ya Cement chumbani wake kwenye nyumba aliyokuwa amepanga mtaa wa River Side kata ya Mwembesongo.

Baada ya kupewa Cement hiyo na mtoto huyo wa tajiri [jina nalihifadhi] tulikosa pesa ya usafiri, tukajitutumia mimi nimebeba 3 kwenye pikipiki yangu na Matama akabeba 2 kwenye Baiskeli yake

Mungu ni Mwema tulifika salama.
. .
Mtumishi wa Mungu Shekidele hakuacha kitu alitinga hadi ofisi ya RPC Mkoa wa Morogoro wakati huo alikutwa SACP Urlch Matei nilivyomuelezea ombi langu alinyanyuka kwenye kiti chake akachana Waleti na kutoa Pesa akamkabidhi Matama akichangua ujenzi wa nyumba hiyo, baadae kamanda huyo bora kabisa alihamishiwa mkoa wa Mbeya. Kwenye shinda

hakushindikani kitu Ofisi ya RPC Iko juu ghorofa ya kwanza huwezi kuaminia licha ya ulemavu wake Matama aliziramba ngazi za ghorofa hilo na kufanikiwa kutinga kwenye ofisni hiyo

Moja ya magezti ya Global yaliyosapoti ujenzi wa nyumba hiyo kwa njia ya makalla
Mtumishi wa Mungu Dustan Shekidele[kushoto]akimuelekeza jambo Mkandarasi wa nyumba hiyo.

Hayati Mzee Hussein aliyejitolea kuchora raman na kujenga msingi bure kwenye nyumba hiyo, Mwenyezi Mungu ampe heri yake huko aliko. 

Anayeshuhudia maongezi hayo ni mmiiliki wa nyumba hiyo ndugu yetu Mohamed Matama.
 .


MATHAYO 5.3—12.

“Heri walio na umasikini wa roho maana ufalme wa Mbinguni ni wao.

Heri wenye huzuni maana hao watafarijiwa.

Heri wenye upole maana hao watarithi nchi.

Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa.

Heri wenye Rehema maana hao watapata Rehema.


Heri wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu.

Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki,maana ufalme wa Mbinguni ni wao.

Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa Uongo kwa ajili yangu.

Furahini na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa Mbinguni kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu” Hili ndio neno letu la Leo Jumaili ya Mei 19.

Neno hili halihitaji uchambuni kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Dustan Shekidele.

Somo hili limejaa maneno ya faraja kwa walioumiwa kwa namna yoyote ile.

Pia somo hili limejaa Tumaini kwa waliodhurumiwa haki na mtu binafsi, Kampuni au taasisi yoyote ya kusimamia haki. Mwisho neno hili linawatia moyo watumishi wa Mungu wanaodhihakiwa kwa kuhubiri neno la Mungu barabarani, kwenye nyumbani za lbada na wale mabalozi wa Mungu wanaosaidi watu wenye uhitaji, wakiwemo Yatima, Wajane na Walemavu.

Nakumbuka wakati mimi napambana kwa hali na mali kwenye Magazeti, Radio, Tv kwenye mitandao ya Kijamii na Mitaani kote huko nikiendesha harambee ya kumjenge nyumba ndugu yetu Mlemavu wa Miguu Mohamed Matama.

Kuna baadhi ya mabajiri niliowaomba msaada wa ujenzi wa nyumba hiyo walininyima msaada na kunidhihaki wakisema.
”We shekidele umekosa kazi ya kufanya mpaka kufikia hatua ya kuhangaika na huyu mlemavu.?

Wakati naambiwa maneno hayo ya dhihaka nyumba hiyo ilikuwa hatua ya kuchimba Msingi, na mshukuru Mungu maneno hayo hayakunikatisha tamaani jukumu hilo nililopewa na Mwenyezi Mungu nimeikamilisha kwa msaada wa wadau wa Mtandao wa shekidele pande zote za dunia.Wahariri wa Global Pubrisher kupitia magazeti ya Uwazi na ljumaa wikiend, Mhariri wa shirika la

Utangazaji Tanzania’TBC’ Abood Media kupitia Mtangazaji wake Zuberi Mkalaboko ambaye baada ya kusoma taarifa za Matama kwenye Mtandao huu alimwita studi kwenye kipindi chake na kufanya naye mahojiano ‘live’yaliyokwenda sambasamba na uchangiaji wa ujenzi wanyumba hiyo.

Kwa Rehema za Mungu nyumba hiyo imekamilika na ndugu yetu Matama ameshahamia kwenye nyumba hiyo na familia yake.

Katika hali ya kushangaza hao matajili wawili walionidhihaki takribani miezi miwli mbele wamekutana na hukumu ya Mungu. .
Mmoja alivamiwa dukani na majambani wamemuibia million 7 pamoja na Bajaj Mpya.

Tajiri mwingine aliyekuwa na uwezo wa kununu Malori mapya 100
kwa mpigo nilitinga dukani kwake na mlemavu huyo nilinunua mifuko 3 ya Cement nikamuomba atusaidie mifuko mingine 2 kwa sababu hitaji letu la kumwaga zege ya msingi kwa maelekezo mifuko 5 na mfukoni nilikuwa na pesa ya mifuko 3 tuliyochangiwa na watu mbali mbali kupitia mtandao ya shekidele.

Tajiri huyo alituangalia mimi na huyo mlemavu kisha akasema Shekidele umekosa kazi ya kufanya? Baadae kaingia kwenye gari kaondoka zake.

Huwezi kuamia baada tajiri huyo kuondoka Mwanaye aliyeshuhudia tukio hilo alinita na kunipa mifuko hiyo 2 iliyokamilisha lengo letu.

Kipekee na namuombe heri kwa Mungu mtoto huyo wa tajiri kwa moyo wa huruma, pia sita choka kuwashukuru na kuwaombea heri kwa mwenyezi Mungu watu wote walionisapoti kwenye ujezi wa nyumba hiyo ya ndugu yetu Matama.

Naamini Mungu alinitumia kama daraja la kuja kwenu kwa njia ya taaluma yangu ya Uandishi wa habari kukamilisha kazi hiyo, hivyo sote tuliochangia hata kwa tofari moja heri zenu mtazikuta kesho Mbinguni.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...