Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, May 18, 2024

UDAKUZI SPESHO. MKE WA MTU ANASHIKILIWA NA POLISI AKIDAIWA KUKUTWA NA SIMU YA WIZI ALIYO KUHONGWA NA MCHEPUKO WAKE.

  

  Na Mdakuzi Dunstan Shekidele,Morogoro.

 WAHENGA walisema hukumu ni hapa hapa duniani,kauli hiyo imetimia hivi karibuni, kufuatia mke wa mtu[jina tunalo] kushikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za Mauaji, baada ya kukutwa na simu ya wizi.

Mke huyo wa mtu alihongwa simu hiyo ya ‘Kiswaswadu’ na mpenzi wake huyo wa nje ya ndoa’Mchepuko’anayekuwa pia nyuma ya Nondo[Lokapu] akituhimiwa kuhusika kwenye mauaji ya Mfanyakazi wa Kazi za ndani’House Girl’aliyekuwa akimiliki simu hiyo.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni Mtaa wa Lukuyu Kata ya Bingwa Mkoani hapa, na kuripotiwa kwa usahihi na vyombo mbali mbali vya habari.

Mara baada ya kutokea kwa Mauaji hayo ya kusigitika ,kama kawaida inapotokea habari kubwa mkoani Morogoro,Mwandishi wa habari hizi hutafuta ‘Engo’nyinyinge mpya ya habari husika na kuujuza umma. 

Hivyo  baada ya tukio hilo kutokea na wahusika wote kukamatwa kwa muda mfupi kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi Mwandishi huyo aliingia kazingi kusaka habari mpya ya tukio hilo.  

Mwandishi huyo alifanikiwa kupata habari mpya lakini kuhusika mkuu Mume wa mke aliyekamatwa na simu aliomba apewe muda wa kuelezea ‘Msala’ huo uliokuta mpendwa mke wake,  kwa mantiki hiyo kwa sasa habari hii tunaiandika kwa mfumo wa kidaku mpaka hapo tutakapo fanikiwa kuzungumza na mume wa mtuhumiwa huyo. 

Pia  habari hizi ilikamilika muda mrefu lakini kutokana na tatizo za Enternet lililotokea hivi karibuni hapa nchini kwetu imepeleka habari hii kuchelewa kuruka hewani.

Moja kwa moja mdakuzi  alitinga maeneo ya Mji Mpya na Mwembesongo nyumbani kwa mke huyo  wa mtu na kurambishwa ubuyu mpya wa tukio hilo  na wambeya wa kitaa A-Z.

”Shekidele njoo tukupe umbeya huyo dada aliyekamatwa na simu ya wizi ni mke wa mtu ambaye mume wake huyo hoi kitandani kwa muda mrefu akisumbuliwa na miguu.

Mwanamke huyo bila huruma mara kwa mara anamuacha mumewe ndani anakwenda kwa mchepuko wake.”
walisema wambea hao wachonga midomo mabingwa wa kufuatilia maisha ya watu.

Wachonga midomo hao wakaendelea kuchonga Penseli wakisema  “Hukumu ni hapa hapa duniani kumbe jamaa huyo ni Jambazi juzi kaenda kua huko Bigwa kapora simu  Kiswaswadu kaja kumhonga mke huyo wa mtu.”

“Taarifa zinadai mmiliki huyo wa nyumba kwa usalama wa nyumba yake na familia yake kabla ya kumkabidhi  simu House Girl huyo aliitega anavyojua yeye  ili ikitoke huyo  dada wa kazi kafanya uharibifu wowote hapo nyumbani na kukimbia basi iwe rahisi kwa bosi huyo kumkamata kupia  simu hiyo.

 Sasa baada ya mauaji hayo  wazee hao wa kazi kuondoka na simu hiyo, mmili kwa kushirikiana na Polisi waliifuatiliana simu hiyo na kumkuta nayo mke huyo wa mtu akiitumia bila wasi wasi wowote”walisema wambea hao na kuendelea kuchonga midomo .

“Polisi wakamdaka kiuraini  alipohojiwa alinyoosha maelezo  kionyesha aliyempa simu hiyo ambaye naye alikamatwa na kutaja mwenzie aliyeshirikiana naye kwenye mauaji hayo”walimalizia kusema wambea hao.

Ili kupata ukweli wa maneno ya wambea hao Mdakuzi wa Mtandao huu alimtwangia simu dada wa mume wa mtuhumiwani huyo na mazungumzo  kwenye simu yalikuwa hivi.

Mdakuzi-Mambo vipi [anamtaja jina]

Wifi- Safi kiasi  nambie

Mdakuzi. Kwa nini safi Kiasi?.

Wifi- Haaa Shekidele inamaana kwa upaparazi wako wote hujui kama huyo mwanamke aliyekamatwa juzi na simu  ni wifi yangu mume wa kaka yangu na hivi ninavyoongea na wewe natoka polisi kuhangaika kama tutapata dhamani kwani yeye hakuhusika kua alikutwa na simu aliyopewa na mcheuko wake.

Mdakuzi- Hooo pole sana best taarifa hizo ninazo sasa ilikuwaje huyo wifi yako kupewa simu na mwanaume mwingine ili hali anamuwe wake ambaye ni kaka yako hebu nipe maelezo ya ziada kwa jambo hili.

Wifi- kaka yangu na wifi yangu walikuwa wanaishi Dar kwa bahati mbaya kaka kapata ajari ya kuvunjika miguu huko kazini kwake, hivyo kamua kumchukua mkewe na kuja hapa nyumbani Morogoro kujiuguza.

Unajua tena sisi wanawake kumbe wifi alikuwa na mchepuko wake huyo kaenda kua huko Bigwa kaja kumpa simu  wifi yangu ambaye kimsingi hakujua kama hiyo simu ni ya waizi na hakujua kama huyo mchepuko wake ni jambazi alijua ni funzi ujenzi tu, basi polisi wamekuja nyumani wamemkuta na hiyo simu wakamkamata.

Mdakuzi- Aisee poleni sana sasa ombia langu naomba nikazungumze na huyo kaka yako kuhusiana na tukio hili la mkewe kuchepuka na kuhongwa simu ya wizi ili nisikie kauli yake.

Wifi-Sawa muda huu baada ya kutoka Polisi ndio naenda kwake kumpikia ambapo kwa sasa jukumu hilo la malezi ya kaka yangu nimelibeba mimi baada ya wifi kukamatwa nikifika nyumbani nitaongea naye akikubali kuhojiwa  nitakupigia uje nyumbani Mtaa wa River Side Mwembesongo.

Mdakuzi-Sawa nisubiri kwa muda gani kwani najua kwa sasa nichwa chako kimejaa mambo mengi unaweza ukajisahu  nikupigie baada ya muda gani nikuulizie? 

Wifi- Kama nusu saa hivi.

 Baada ya nusu saa  alipopigiwa wifi huyo alisema

“Nimeongea na kaka kaomba kwa sasa achwe kwanza kwani majanga haya ya maradhi na hili la mkewe aliyekuwa akimuhudumia kukamatwa yamemchanganya sana hivyo ajakaa sawa kiakili,kasema akiwa sawa anakuita zungumze naye”.

Mdakuzi. Sawa Mungu azidi kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu anachopitia na wewe nikuombe kwa kipindi hiki usiwe mbali naye  kwani anahitaji faraja ya hali ya juu, nikipata muda nitakuja kumsalimia  kirafiki nje ya Uandishi wa habari.

Wifi- Sawa Shekidel karibu sana.

Mdakuzi- Asante

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kamanda Mkama alisema, wamefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Monica  Poul[22]aliyekuwa mfanyakazi wa kazi za ndani  Mtaa wa Lukuyu kata ya Bigwa.

 Big Boss huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro  aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni  Rehema  Omary[30] Mkazi  wa Mtaa Mwembesongo ambaye alikutwa na  simu ndogo  aina ya Tecno iliyokuwa ikimilikiwa na Marehemu Monica.

Wengine ni Mussa Mrisho[23] Fundi Ujenzi Mkazi wa Bigwa na Mbaraka Omary [25] Fundi Ujenzi Mkazi wa Tubuyu.

Kamanda Mkama alisema watuhuiwa hao baada ya  kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na Tv.Radio na Feni vyote hivyo ni mali ya bosi wa House Girl huyo.

 

      


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...