Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 21, 2024

MICHUANO YA RAMADHAN CUP. TANZANITE ACADEMY NA MORO KIDS NI NOMA, GEMU YA LALA MARA 3.

Papatu Papatu  gemu hiyo ya Moro Kids na Tanzanite kipa wa Moro Kids akinyaka mpira katikati ya miguu ya mshambuliaji Tanzanite mwenye.





...Mwamuzi akiwaa m,aelekezo makia nkbala ya zoezi la kuiga pelnaty kuanza, aliwambia





Kipa wa Tanzanite akiangua pelnaty hiyo iliyowaeleka Nusu fainali

 


   Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MORO YA VIPAJI,

Kauli hiyo ya wadau wa soka mkoa wa Morogoro, imetimia wiki iliyopita baada ya Taasisi mbili maarufu mkoani Morogoro zinazojihusisha na  kuibua na kukuza vipaji vya soka, Moro Kids na Tanzanite Academy zimetoka sare mara 3 kwenye robo fainali ya Michuano ya Ramadhan Cup iliyoandaliwa na chama cha soka Wilaya ya Morogoro’MDFA.’

Michuano hiyo iliyoanza kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhan inafanyika uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro ambapo kwa sasa  ipo  hatua ya Nusu fainali.

Kivutia kikubwa kwenye michuano hiyo ni hatua ya robo fainali iliyozikutanisha taasisi hizo, kufuatia timu hizo kusheheni wachezaji wengi wenye Vipaji vya hari ya juu gemu hiyo imelala mara tatu baada ya miamba hiyo kutoka   sare hadi kwenye mikwaju ya Pelnaty.

 Katika Mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1  walipoingia kwenye mikwaju ya Pelnaty pia walitoka sare kwa kufungana Pelnaty 8 kwa 8 huku kila timu ikikosa Pelnaty Moja, mwamuzi aliahirisha gemu hiyo baada ya giza kutanda uwanjani.

Gemu ya Pili timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2 walipoingia kwenye mikwaju ya Pelnaty mambo yakawa yale yale wakafungana Pelnaty 7-7 na mwamuzi kuahirisha tena baada ya makipa wote wawili kulalamika giza kutanda uwanjani.

 Gemu ya tatu imepigwa juzi na timu hizo kutoka tena sare ya bao 1-1 walioingia kwenye mikwaju ya Pelnaty safari hii Moro Kids wameangukia Pua baada ya pelnaty ya 8 iliyopigwa na Vedatus Kizito kudwaka kiufundi na Kipa wa Tanzanite Mohamed Nguvu, hivyo Tanzanite kutinga nusu fainali kwa jumla ya Pelnaty 8 dhidi ya 7 za Moro Kids.

Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia Michezo yote mitatu iliyozikutanisha taasisi hizo na kushuhudia ‘udambwi dambwi’mwingi kufuatia timu zote kusheheni wachezaji ‘Majanck’wenye vipaji vya hali ya juu.

 Kufuatia uwezo mkubwa ulioonyesha na timu hizo mbili Wachambuzi wa soka wamebashiri  mshindi wa robo fainali hiyo ndiye mwenye nafasi kubwa wa kunyakua ubingwa huyo.  

KWA FAIDA YA WADAU WA MTANDAO HUU NGOJA NIWAPE HISTORI FUPI YA TANZANITE. Kwa sasa watanzania wengi wanaijua Taasisi ya Morogoro Kids inayotajwa kuongoza kutoa wachezaji wengi wanaong’ara timu mbali mbali za Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza na  daraja la Pili.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Shomari Kapombe. Mzamiru Yassini na Ladack Chasambi[Simba].

 Dickson Job, Nickson Kibabage. Kibwana Shomary, na Kipa  Abuutwarib Mshery[Yanga] na Pascal Msindo [Azam Fc].

 Wengine ni Shiza Kichuya, [JKT Tanzania] Masenga[Tanzania Prisons]  Hamad Waziri’Kuku’ [Singida Fountaine Gat] Hassan Kessy ‘Kidingile’ [Tabora United] Nasri Kombo’Sccoba’[Mtibwa Sugar] na Juma Abdul[ambaye kwa sasa binafsi sijui nyuko timu gani] lakini aliwahi kung’ara na Yanga na Singida United.

Wachezaji wote hawa wamepita kwenye mikono ya aliyekuwa kocha Mkuu wa Moro Kids Hussein Mau ambaye kwa sasa amejitoa kwenye taasisi hiyo na kuanzisha taasisi yake  ya Tanzanite Academy nakishirikiana na Boniface Kiwale na Mwanasheria mmoja Marufu mkoani Morogoro.

 Tanzanite wameshaanza kuzalisha wachezaji na kuwauzwa sehemu mbali mbali nchini, ikiwemo Mtibwa B, mmoja wawacheji hao ni Said Mkopi Maarufu ‘Malialosa’ ambaye kwa sasa ndio winga tegemo wa Mtibwa ‘B.’

Jana Tanzanite wametinga fainali ya michuano hiyo ya Ramadhan Cup baada ya kuifunga timu ngumu ya  J.L Academy kwenye mchezo wa Nusu fainali,huku mabao yote mawili yakifungwa dakika za mwisho kwa mipira ya faulo nje ya 18, iliyopigwa kiufundi na dogo Abdallah Machumi mwenye umri wa miaka 16 ambaye habari zake na picha zitaruka hewani hivi punde.

Ikumbukwe JL Academy inayomilikiwa na mchezaji wa zamani wa  Reli ya Moro, Mtibwa Sugar na Simba Ulimboka Mwakingwe’Uli’ 

 


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...