Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, May 3, 2024

TASWIRA, MKUTANO MKUU WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MOROGORO.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro akiongoza Mkutano Mkuu Maalumu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro wiki iliyoita


.                     ....Mkilanya akisisitiza jambo kwa wajumbe
...Mwenyekiti Mkialanya kulia akiendelea kuongoza kikao hicho sambamba na Katibu Mkuu wa chama hicho Lilian Lucas Kasenene
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Thadei Hafigwa akifafanua jambo.

Mtunza fedha Loveness Nyawili akiwasirisha rioti ya fedha mbele ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa Mwaka.

Mwandishi wa habari Mkongwe nchini aliyewahi kuvitumikia vituo vya Radio na Luninga vya TBC ,ITV, Abood Media na SUA Media Mzee Bujaga Ezengo Kadako ]Baba Askofu] akichangia kwenye mkutano huo.

 


 Mwandishi Mahiri mkoa wa Morogoro Peter Kimath’Mgosi’akichangia kwenye mkutano huo.


          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

WAANDISHI wa habari Mkoa wa Morogoro, wiki iliyopita wamefanya mkutano Mkuu Maalumu wa Wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro  [MOROPC] kwenye ukumbi wa Bwalo la Umwema JKT.

Mkutano  huo uliohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka Wilaya mbali mbali za Mkoa wa Morogoro umefunguliwa na mgeni rasmi  Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe Dennis Londo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ’TAMISEMI’

 Baada ya  Mbunge huyo kufungua mkutano huo ulioanza saa 5 asubuhi na kutamatika saa 11 jioni umeongozwa kwa Weledi  na Mwenyekiti wa Chama hicho Nickson Mkilanya Almaarufu ‘Nick Fado’.

Mkutano huo ulijadili mambo mbali mbali ikiwemo mapato na matumizi ya fedha kwa Mwaka 2022-23, ambapo Mtunza fedha wa chama hicho  Loveness Nyawili aliwasilisha ripoti hiyo iliyopokelewa na wanachama wote walionekana kulizishwa nayo.

Baada ya ripoti hiyo ya fedha kupita Mkilanya alisimama tena na kuainisha muendelezo wa mipango ya chama hicho ya  ujenzi wa Mjengo wao.

lkumbukwe kwa zaidi ya miaka 8 chama hicho kimefanikiwa kununua kiwanja eneo la Kibwe kata ya Mlimani  jirani na ofisi za Wamo Mkoa wa Morogoro.

Mwenyekiti  huyo mpenda Maendeleo kwa msisitizo aliamua kujitoa muhanga kwa kura kiapo  mbele ya wajumbe wa Mkutano mkuu huo akisema.

“Tumeshuhudia baadhi ya mikoa waandishi wenzetu hawana ofisi wametimuliwa kwenye nyumba baada ya kushindwa kulipa pango, vifaa vya ofisi vimehifadhiwa majumbani kwa viongozi,

Hilo liwe somo kwetu kwenye kikao chetu cha kamati ya utendaji nimewaambia viongozi wenzangu tupambane hadi Mwakani mwezi wa 6 tuhamie kwenye jengo letu tukishindwa kufanya hivyo mimi kama mwenyekiti nitajihudhuru nafasi hii na hilo nalisema tena mbele yenu wajumbe wa mkutano Mkuu.”

 Wajumbe hao walipinga vikali hoja hiyo ya mwenyekiti wao ambaye wanaimani naye kubwa.

“ Mhe Mwenyekiti wetu sisi bado tunaimani na wewe hivyo tunaomba kwenye shwara hilo la ujenzi usi Bert ukijiudhuru nani  atatuongoza kwenye mapambano haya”alisema  Alfan Diu Maarufu ‘Don King’na kuungwa mkoni  na wajumbe  kwa kupewa zawadi ya makofi mengi.

Katika kuelekea kwenye ujenzi huo Mwenyekiti Mkilanya aliunda Kamati ya Ujenzi inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe Latifa Ganzel Mwandishi Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo ambaye pia Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM.

Kama hiyo haitoshi Mkilanya aliendesha harambee ya ujenzi huo kwenye mkutano huo ambapo wajumbe waliahadi kuchangia  matofari na mifungo ya saruji, miongoni mwa wajumbe waliahidi Mifuko ya Cement ni pamoja na Dustan Shekidele.

Kwa haraka haraka kwenye harambee hiyo wajumbe waliahidi zaidi ya mifuko 100 ya Cement na matofari zaidi 600 huku baadhi wakitoa fedha Cash.      

                   NJE YA BOKSI.

Nje ya waandishi wa habari wadau mbali mbali wa habari mkoa wa Morogoro wameahadi kuchangia ujenzi.

 Miongoni mwao ni Mlenzi wa chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Aziz Abood.

 Mwingine ni  Mh Fatuma Mwassa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro,ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera .

Naye Mbunge wa Mikumi Mh Dennis Londo, alitoa hadi yake ya kuchangia ujenzi huo  Aprili 27 mara baada ya kufungua mkutano huo wa Waandishi wa habari.

 

lfahamike [MOROPC]kwa sasa wamepanga  kwenye Ghorofa la Chama cha Walimu Mkoa wa Morogoro eneo la Nunge jirani na Mahakama ya Mwanzo.

                   CAPTION.

Mwenyekiti Mkilanya akiongoza mkutano Mkuu huo wa Waandishi wa habari.

Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye mkutano huo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...