Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMATI ya Masaa 72 ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ Juzi Jumanne imeketi na kutoa maamuzi mbali mbali ya Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la Pili.
Baadhi ya mambo muhimu yaliyoamuliwa na kamati hiyo ni pamoja na kufuta kadi nyekundu ya beki wa Coastal Union Wana Mangushi] Lamick Lawi aliyopewa na Mwamuzi Raphael lkambi Maarufu Raphael Webb.
Refa huyo Janki mwenye maskani yake Mawenzi Mkoani Morogoro.alimlima kadi hiyo baada ya Lamack kumvuta jezi Mshambuliaji wa Yanga Aziz Ki aliyemtoka beki huyo naelekea lango la Coastal.
Kwa mujibu wa sheria beki wa mwisho akimfanyia madhambi mshambulia wa timu pinzani anayeelekea lango kufunga adhabu yake ni kadi nyekundu kwa maana amezuia nafasi ya wazi ya gori kwa kufanya madhambi.
Kamati hiyo imeifuta kadi hiyo kwa maelezo kwamba beki Lawi hakuwa mtu wa mwisho nyuma yake kulikuwa na beki mwingine wa Coastal aliyeelekea eneo la tukio kumkaba Aziz K hivyo Lawi hakustaili kupewa kadi hiyo nyekundu alistaili kadi ya njano.
KWA MORO KIDS SASA.
Baada ya ripoti za msimamizi wa kitu, kamisaa na mwamuzi wa mchezo huo wa Play off kati ya wenyeji Moro kids na Kurugenzi ya Shinyanga uliopagwa kuchezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro Aprili 27 na kurugenzi kushindwa kutokea bila taarifa.
Maamuzi ya kati ya Masaa 72 kwa timu hiyo ya Kurugenzi.
Mosi. imepigwa faini ya million 3 Cash Maney sambamba na timu hiyo kulipa gharama za mchezo huo waliouvuluga.
Pili .Kurugenzi watakatwa Pointi 15 kwenye ligi yoyote watakayocheza, kuanza mchezo wa marejeano dhidi ya Moro Kids utakao chezwa keshokutwa Aprili 4 Mkoani Shinyanga.
Na kwamba Kurugenzi wanatakiwa kulipa million 3 na pesa za gharama ya mchezo wa Morogoro kabla Aprili 4 siku ya mchezo huo wa marejeano,wakishindwa kulipa wanakabiliwa na adhabu nyingine.
Kwa maelezo hayo ya kamati ya masaa 72 ni dhahiri shairi Moro Kids wameshapanda ligi daraja la pili ingawa bado haijatangazwa rasmi mpata mchezo huo wa marejeano utakapofanyika hiyo keshokutwa.
Hata ikitokea Kurugenzi kamfunga Moro Kids haitasaidi kitu kwani adhabu hiyo ya kukatwa alama hizo 15 itaanza kwenye mchezo huo wa keshokutwa.
SWALI LA MWANDISHI WA MTANDAO HUU. Kama Kurugenzi wameshindwa kusafiri kutoka shinyanga kuja Morogoro kwa kile kinachodaiwa ukata wa fedha je wataweza kulipa milioni 3 na gharama za mchezo ndani ya siku hiyo moja iliyobaki kabla ya mchezo wa marejeano.?
Hebu ngoja tuone hiyo keshokutwa picha litakuwaje watalipa pesa hizo au la, Mwandishi wa habari hizi anafuatilia tukio hilo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao pendwa wa shekidele muda wote.
No comments:
Post a Comment