Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 6, 2024

MPIGA PICHA ITV AWA KIVUTIO KWENYE MKUTANO WA MOROPC

                              CAPTION

“ Kujisifu sio dhambi ila dhambi ni kuziendekeza hizo sifa”.

Baada ya kauli hiyo ya faraja ngoja sasa nijipakulia minyama.

Mwandishi Mahiri nchini wa habari za Kijamii, Siasa, Michezo, Burudani na Udaku Mtumishi wawanyonge Dustan Shekidele  ‘Ez Come Ez Go’ wapili kulia waliosimama aliyevaa flana yenye nembo ya Shirika la Ndege Tanzania ‘Air Tanzania’akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe Dennis Londo[wa katikati walioketi].

Mhe Londo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kudumu wa kamati ya Bunge TAMISEMI alikuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’.

Wakwanza kulia walioketi ni Mwenyekiti wa ‘MOROPC’ Sir Nickson Mkilanya na kushoto waliokeni ni Katibu Mkuu wa MOROPC Madamu Lilian Lucas Kasenene ambaye pia ni Mjumbe wa Muungano wa klabu za Waandishi wa habari Tanzania, Union of Tanzania Press Clubs’UTPC’.

Wengine waliosimama ni wanachama wa MOROPC.akiwemo Shehe Hussein Mpiga Picha wa ITV akiwa Mwandishi pekee aliyetika kwenye mkutano huo na vazi takatifu la Kanzu na Bagharashia huku akiwa na signa kubwa kwenye paji lake la uso ikiwa ni ushahidi wa yeye kumsujudia Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardh.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...