Machuma akibebwa juu na wenzake baada ya kufunga mabao 2.
........Akihojiwa na Mtanda huu
. Mwandishi wa Mtandao huu [kulia] akizungumza na kocha Hussein Mau jana kwenye uwanja wa Saba saba kuhusiana na Kipaji cha Machuma.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KATIKA hali isiyo ya kawaida dogo Mwenye kipaji Maalumu cha Soka mkoa wa Morogoro Abdallah Omary Machuma mwenye umri wa miaka 16 amegoma kuzitumikia timu kubwa za Simba na Yanga kwenye kalia yake ya Soka.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakuza kipaji chake kwenye kituo cha kuibua na kukuza vipaji cha Morogoro Tanzanite Soccer Academy,[MOTASOA] ameyasema hayo juzi mara baada ya kutamatika kwa fobo fainali ya michuano ya Ramadhan Cup kati ya timu yake dhidi ya J-L Academy ya ‘Ulimboka Mwakingwe.’
Katika mchezo huo Machuma anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji [Namba 8] aliiwezesha timu yake ya Tanzanite kutinga nusu fainali baada ya kufunga mabao yote mawili kwa njia ya faulo nje ya 18, bao la kwanza akifunga dakika 78 na la pili dakika ya 85.
Baada ya gemu hiyo iliyokuwa na upinzani mkali kwa muda wote wa dakika 90 kutamatika baadhi ya wachezaji wa Tanzanite walimvamia mchezaji huyo na kumbeba juu juu wakimpongeza kwa kuwapeleka nusu fainali.
Mwandishi wa habari hizi naye aliingia uwanjani na kufanya mahojiano mafupi na mchezaji huyo juu ya kipaji chake na malengo yake ya baadae.
Awari alitakiwa kueleza kwa ufupi historia ya maisha yake.
“ Mimi ni mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, ninaumri wa miaka 16 nimesoma shule ya Msingi Maduhu Dumila na kuhitimu la saba mwaka 2019.
Kwa bahati mbaya sikufaulu na wazazi wangu nawakuwa na uwezo wa kuniendeleza kielimi kwa maana ya kunipeleka sekondari.
Kwa kutambua kipaji changu cha soka mwaka 2020 baba yangu kamua kunileta hapa Morogoro kwenye kituo hiki cha Tanzanite ambapo mpaka sasa nafurahi kuwa hapa kwani kituo kina walimu wazuri wakiongozwa na Mwalimu Hussein Mau na ticha Boniface Kiwale”alisema Dogo huyo.
Alipoulizwa maswali mawili kwampigo kwamba kati ya Simba na Yanga anatamani kucheza timu gani kati ya hizo? Swali la pili.
Katika ligi kuu ya Tanzania Bara anavutiwa na mchezaji gani anayetamani kuyafikia mafanikio yake?.
Majibu yake haya hapa.”Katika maisha yangu sina ndoto za kucheza Simba na Yanga ndoto zangu ni kucheza soka nje ya nchi, nimeshuhudia simba na yanga ni vigumu sana kwa mchezaji wa kitanzania kudumu kwa kiwango chako cha soka kwa miaka 3 mfurulizo kwenye timu hizo waliweza ni wachache sana huku wengi wakiferi. Swali lako la pili.
Hapa Tanzania sina mchezaji ninayejifunza kwake namini kwenye kipaji changu kama Mwenyezi Mungu ananisaidia nisipate ‘lnjali’ kwa ulaya navutiwa na winga wa Real Madrid Vini Jr”.
Swali la mwisho toka ujiunge na Tanzanite umefunga magori mangapi?
Machuma. Sikumbuki ila ni mengi sana yanazidi 20 kwenye michezo yote ya ligi na ile ya kirafiki.
Jana Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuzungumza na Kocha Hussein Mau juu ya Kipaji cha Abdallah Machuma ambapo Kocha huyo aliyeibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji wengi wa Ligi kuu wanaotamba kwa sasa Simba, Yanga, na Azam kafunguka mazito juu ya kipaji cha mchezaji huyo huku akimtabilia makubwa.
Mahojiano hayo yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment