Machuma akizungumza na Mtandao huu majuzi mara baada ya kufunga mabao 2 kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Ramadhan Cup dhidi ya JL Academy ya Kihonda Maghorofani.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KOCHA Maarufu nchini anayetajwa kwa sasa kuongoza kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji wengi nchini, wakiwemo wachezaji wa Yanga, Simba na Azam.Ticha Hussein Mau amefunguka mazito juu ya kipaji cha mchezaji Abdallah Omary Machuma.[16].
Mtandao huu jana uriripoti habari za mchezaji huyo na kuahidi kuendelea na stori hiyo Leo kwa kuzungumza na kocha Mkuu wa taasisi ya kuibua na kukuza vipaji ya Morogoro Tanzanite Soccer Academy ticha Hussein Mau.
Kwenye mahojiano hayo yaliyofanyika juzi ndani ya Uwanja wa Saba saba wakati michuano ya Ramadhan Cup ikiendelea, Mwandishi wa habari hizi alitaka jua namna kocha Mau alivyokiona Kipaji cha mchezaji huyo na kukizungumzia kwa undani.
Kocha Mau alijibu Maswali hayo kama ifuatavyo.
”Taasisi yetu kila Mwaka tunazunguka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro kusaka Vipaji, tulikwenda Kilosa eneo la Dumila tukapata wachezaji kadhaa wakati tukiwa kwenye Scaut Dumila Abdallah Machuma hakuwepo, eneo la tukio.
Siku iliyofuata baba yake kapata taarifa kwamba tulikuweo Dumila kusaka vipaji, kanipigia simu kaniambia anakijana wake anakipaji nikamueleza zoezi hilo kwa eneo hilo limeshapita hivyo kama anataka amlete mwenyewe hapa kituoni.
Kweli mzee huyo kamleta mwanaye kampangia chumba eneo la Chamwino baada ya kufanya naye mazoezi wiki moja tu mimi na wenzangu tumebaini mchezaji huyu anakipaji, hivyo kama utaratibu wetu wa kituo tumempa fomu ya mkataba wa kujiunga na taasisi yetu kasaini”alisema ticha Mau na kuongeza.
“Toka ajiunge na kituo chetu mwaka 2020 licha ya kucheza nafasi ya kiunga mshambuliaji lakini ameshafunga mabao mengi, Shekidele wewe ni shahidi umeshuhudia juzi Machuma katupeleka nusu fainali baada ya kufunga mabao 2 yote kwa mipira ya faulo nje ya 18, yaani huyu dogo ni fundi sana wa kufunga mabao ya faulo”alimalizia kusema ticha Mau na kumtabilia makubwa mchezaji huyo kwamba atafika mbali kisoka.
Ticha Mau ambaye awari alikuwa taasisi ya Moro Kids kabla ya kujiondoa na kuanzisha taasisi yake hiyo ya Moro Tanzanite Soccer Academy, anaongoza kwa kuibua nakuendeleza vipaji vya wachezaji wengi nchini wakati akiwa Moro Kids, baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Somary, Nickson Kibabage, na Kipa Abuutwari Mshery[Yanga]. Mzamiru Yassin na Somary Kapombe[Simba] na Pascal Msindo Azam Fc.
Wengine ni Shiza Kichuya[JKT Tanzania] Masenga[Tanzania Prisons] Hamad Waziri ‘Kuku’[Singida Fountain Get] Hassan Kessy’Kidingile’[Tabora United] Zuberi Daby[Mashujaa ya Kigoma] Nassir Kombo’Scobb’[Mtibwa Sugar] na Juma Abdul [aliyewahi kuzitumikia Yanga na Singida United kwa sasa sijui niite sigida gani kwani tayari kuna timu 2 za Singida zilizomeguliwa menguliwa na kuwa timu mbili tofauti].
Wachezaji wote hao kwenye simu zao huwezi kukosa namba za ticha Mau na wanapokuja rikizo Morogoro lazima walipoti kwa kocha wao huyo.
No comments:
Post a Comment