Mhe Latifa Kulia akimkabidhi kazi 100 za CCM Mwenyekiti wa UWT Kata ya Mafika Tabitha Justo
......Mhe Latifa akizungumza na wana wajumbe wa UWT Kata ya Mafiga
Baadhi ya wajumbe wakimsikiliza kwa umakini Mhe Latifa
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MIKAKATI ya kukiimarisha chama, Diwani Viti Maalumu kwa leseni ya CCM Mhe Latifa Ganze juzi amegawa kadi 100 kwa Uongozi wa UWT Kata ya Mafiga, ikiwa ni maagizo ya UWT Taifa kuwataka viongozi wa Kata zote nchini kusaka wanachama wapya kwenye maeneo yao.
Akikabidhi kadi hizo kwa Mwenyekiti wa UWT Kata ta Mafiga Tabitha Justo, Mhe Latifa alisema kwenye moja ya Vikao vya UWT taifa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo taifa Marry Chatanda aliwaagizo viongozi wote walioshiriki kwenye kikao hicho kugawa kazi kwa Viongozi wa Kata kwa lengo la kusaka wanachama wapya.
“ Hii ni maagizo ya Viongozi wetu wa juu, kwenye moja ya vikao vilivyofanyika Dodoma walituagiza kuhamasisha viongozi kata na matawi kusaka wanachama wapya, leo nimewakabidhi kadi hizi 100 kwa lengo la kuzigaw akwa wanachama wapya kama zitakwisha mapema nipigieni simu muda wowote nitawaletea nyingine hata mkitaka kadi elfu moja nawaleta lengo letu ni kuzidi kukiimalisha chama chetu”alisema Mhe Latifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti Tabitha mara baada ya kupokea kadi hizo alimuahidi Mhe Latifa kutekeleza maagizo hayo ya chama kwa kusaka wanachama wapya kwenye kata yao na kuwakabidhi kadi hizo.
Ifahamike kwamba Mhe Latifa kabla ya kunyakua nafasi hiyo ya Udiwani wa viti Maalumu Jimbo la Morogoro alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana [UVCCM] Wilaya ya Morogoro akiitumikia Jumuiya hiyo ya kwa Weledi Mkubwa kabla ya kutoka kwenye jumuiya hiyo kwa kanuni za Umri.
Kwa mafanikio aliyoyaonyesha UVCCM Wapiga kura wa Viti Maalumu hawakusiti kupiga tiki kubwa kwenye jina la Mhe Latifa na kuibuka kidedea kwenye nafasi hiyo .
Moto aliouwasha UVCCM anauendelea kwenye Udiwani huku wachambuzi wa mambo wakimtabilia makubwa kwenye safari yake hiyo ya Uongozi wakitembea kwenye historia yake ya nyuma na sasa.