Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 28, 2024

HII IMEKAA POA SANA. DIWANI VITI MAALUMU ATENGENEZA AJIRA KWA WANANCHI.

Diwani wa Viti Maalumu jimbo la Morogoro Mhe Latifa Ganzel akizungumza na wana UWT Kata ya Mafika leo jioni.

Mgeni Rasm kwenye hafra hiyo Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe Mchungaji Thomas Butabile akizunguna
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Mafiha Tabitha Justo naye akizungunza kwenye hafra hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa UWT Kata ya Mafiga wakimsikilzia Mhe Latifa kw aumakini mkubwa
.....Mhe Lafika kulia  akishirikiana na Viongozi wa tawi la Misufini kufungua Cherahani hiyo

....Mzingo sio mtumba ni mpya kabisa Mhe Latifa akichana manaironi kwenye cherehani hiyo


.....Mhe Latifa akimkabdihi cherehani Mwenyekiti wa tawi la Misufini Johan Ahmed Mahimbi mwenye frana ya mistari stari

.... kkwa furaha wana UWT Kata wakimuao Mhe Latifa baada ya kuwakabidhi cherehani hiyo
.....Mwenyekiti wa tawi la Misufini Jahari akimshukuru Mhe Latifa kwa kuwakabidhi Cherehani hiyo
Kutoka kulia ni Katibu wa UWT Kata Farida Rajabu, Mwenyekiti wa UWT Kata Tabitjha Justo. Mhe Diwani Latifa Ganzel na Mwisho kushoto ni Mhe Diwani wa Kata ya Mafiga  Mhe Mchungahi Thomas Butabile


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

DIWANI wa viti Maalumu kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Jimbo la Morogoro Mhe Latifa Ganzel, ameitendea haki lrani ya chama chake kwa kutengeneza ajira zaidi ya 100, baada ya kugawa mitambo ya kutengeneza sabuni na cherehani kwa matawi manne ya UWT Kata ya Mafiga,

Msaada huo umechangia kwa kiasi kikubwa kutoa ajira kwa wanachama hao wa Matawi ya Manzese, Tanki la Zamani.na tawi la Zahanati ambapo matawi hayo siku za nyuma aliyakabidhi mitando hiyo ya kutengeneza sabuni,na kwamba leo Mei 28 Mhe Latifa ambaye pia ni Mrezi wa UWT kata ya Mafiga amehitimisha ahadi yake kwa kuwakabidhi cherehami Mpya tawi Misufini.

Akizungumza kwenye hafra hiyo iliyofanyika kwenye viwanja wa CCM Kata ya Mafiga Mwenyekiti wa U.W.T Kata ya Mafiga Tabitha Justo, alimshukuru Mhe Latifa kwa kutimiza ahadi yake kwa asilimia mia moja.

” Kwenye ziara yako ndani ya kata yetu ulihadi kutoa Vifaa maalumu vya kutengeneza sabuni kwa matawi 3 , hukuchukua muda mrefu ukatekereza hadi hiyo na kwamba kwa sasa kwenye kata yetu tuna mradi wa kutengeneza sabuni uliotoa ajira kwa watu mbali mbali hata wasio kuwa wana CCM.

Leo umekamirisha hadi yako kwa kuwakabidhi Cherehani tawi la Misufini hongera sana Mhe Latifa hatuna chahakulipa ila hadi yetu kwako ni mitano tena kwako” alisema Mwenyekiti huyo.na kupokea zawadi ya makofi kutoka kwa wanachama wa UWT Kata ya Mafiga huku wakiendeleza wimbo huo wa mitano tena kwa Mhe Ratifa.

Naye Diwani wa Kata ya Mafiga Mchungaji Thomas Butabile aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafra hiyo awari alimpongeza Mhe Latifa kwa kutekeleza ahadi yake kwa matawi yote manne ya CCM Kata ya Mafiga.

“ Mhe Ratifa anakipawa cha uongozi hata kwenye vikao vyetu vya baraza la Madiwani michango yake mingi imekuwa na tija kwa Jimbo letu la Morogoro,wana U.W.T kata ya Mafiga hongeni sana mmepata mrezi bora mwenye viwango wa TBS na mimi kama Diwani wa kata hii najivunia Mhe Latifa kuwa mrezi kwenye moja ya Jumuiya zangu za kata”alimalizaia kusema Mhe Mch, Butabile.

Akizungumza mara baada ya kumkabidhi cherehani hiyo mwenyekiti wa Tawi la Mifusuni Johari Ahmed Mahimbi Mhe Ratifa ambaye kitaaruma ni Mwandishi wa habari aliwapongeza viongozi wote wa matawi ya Manzese, Tanki la zamani na Zahanati kwa kuendeleza kwa weledi mradi huo wa Sabuni unaoendelea kukua siku hadi siku.huku akiwaomba viongozi wa tawi la Misufini kuiga mfano wa wenzao kwa kuendelea kwa weledi Mradi huo wa ushanaji nguo kupitia Mtambo huo wa Cherehani.

Mwisho Mhe Ratifa alitoa maelekezo aliyopewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda kwa wanachama na Viongozi wa UWT Kata ya Mafiga. kwenye maelekezo hayo Mhe Latifa aliwakabidhi na dhana za maelekezo hayo wa Big Boss wa UWT Taifa zana hizo na maelekezo hayo kwa pamoja vitaruka hewani hivi punge hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kujua maelekezo hayo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...