Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, April 18, 2024

UDAKUZ SPESHO. HII KALI. MAMA AZIKA KITOWEO CHA NYAMA ALICHOPEWA ZAWADI NA JIRANI YAKE ALIYENUNIANA NAWE KWA MUDA MREFU.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na Pikipiki yake ya Mwendo kasi’Boxer Mnyama’ akiingia Mtaani kusaka Umbeya wa Kitaa.

 


Na Mdakuzi Dustan Shekidele, Morogoro.

 UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya Filahuni, Mama mmoja [Jina kapuni kwa sababu za kiudakuzi] juzi ameshikwa na butwaa na kujikuta anatetemeka kama sio kutetema Mayele baada ya kuletewa zawadi ya kitoweo cha Nyama ya Mbuzi na jirani yake aliyegombana naye.

Tukio hilo la aina yake limetokea juzi kwenye mtaa mmoja uliopo mkoani hapa, wanaoishi  majirani hao wenye uwezo mkubwa wa nguvu ya kifedha.

Kama kawaida Mdakuzi wa Mtandao huu anayejichanganya kwenye makundi mbali mbali ya watu, vikiwemo vijiwe vya kawaha akisaka Umbeya wa kitaa.

  Juzi Shushu huyo alitinga kijiwe cha Madalali wa Nyumba, Viwanja, Fremu za maduka na Vyumba vya kuishi kwenye kijiwe chao kilichopo eneo la Lunna katikati ya Mji wa Morogoro na kushuhudia madalali hao wakifunguka haya.

” Kuna mama alikuwa anauza moja ya nyumba zake katualika  tukaikagua na kuipiga picha ili tutafute mteja.

Chaajabu wakati Bi mkubwa huyo akiendelea kutuonyesha Mjengo huo  kaja bint mmoja na mfuko uliojaa nyama, tumeshangaa  Bi mkubwa huyo baada ya kupokea nyama hiyo kaanza kutetemke na kuomba ushauri kwetu’’ walisema Mdalali hao na kuongeza kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

‘’ Akisema, wanangu huyu jirani aliyenipa hii nyama tumegombana na hatuongei huu mwaka sasa,chaajabu Leo kachinja Mbuzi kampa mfanyakazi wake  aniletee hii nyama nipike nile kweli jambo hili liko sawa, mbaya zaidi hakuleta yeye kamtuma mfanyakazi wake  kama mlivyoshuhudia’’

 Dalali huyo kaeleza ushauri waliompa.

’’Awari tulimpa nafasi yeye kujua  mawazo yake juu ya tukio hilo yako je, kasema uamuzi wake  naye anampa mfanyakazi wake ailudishe kwa huyo baba huyo.

Tukamwambia hapana asifanye hivyo ili kumkomesha achukue jembe  aizike nyama hiyo, huyu Dalali mwenzangu alimshauri aichukue nyama hiyo aende kushitaka kwa mwenyekiti wa serikali ya Mtaa.

Mwisho wa siku Mama huyo kakubali ushauri wangu kuifukia nyama hiyo mbele yetu,sekeseke hilo hiyo limekuwa  chungu kwetu  zoezi  la biashara ya nyumba  likafa  Mama akiomba tulisitishe kwani tukio hilo limemchanganya akili ’’ walimaliza kusimulia Madalali hao Maarufu Mkoani Morogoro.

Kwa sababu wahusika wote hawajapatikana kuzungumzia tukio hilo, habari hii kwa sasa tunairipoti kwa mfumo wa mafumbo bila kutaja jina la mtu yoyote kwa kuzingatia kanuni na sheria za Uandishi wa habari.

Kwa sasa Mwandishi wa habari hizi anafanya juhudi za kuwasaka wahusika wote wawili kwa lengo la kuzungumza nao  wakipatikana habari hii itaruka hewani na kuweka wazi kila kitu Black and White tukisikia maelezo ya pande zote mbili.  

                          


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...