Afande Sele akiimba sambamba na Bi Mkubwa Denisia Mangweha Mama Mzazi wa Msanii nyota wa Hip Hop nchini Hayati Albeth Mangweha’Ngweha’ kwenye moja ya kumbukizi za kifo cha msanii huyo.
Afande sele akiwa na Tumain’Rehema’ Dustan Shekidele[kulia] na Neema Dustan Shekidele’
lkumbukwe Tumaini na Tunda wamesoma darasa moja shule ya Msingi Nguzo.
MFALME wa Vina nchini. Simba wa Morogoro. Mtu Pori .Seleman Msindi, Baba Tunda Maarufu kwa jina la kisanii Afande Sele ’ akiingia Uwanja wa Jamhuri Morogoro huku akishangiliwa na Umati mkubwa wa watu waliofulika uwanjani hapo.
Afande Sele ambaye ni Msanii nyota nchini wa Muziki wa Hip Hop baba wa watoto wawiki wa kike, Tundajema Maarufu Tunda na Asantesanaa, mpaka sasa anashiriki Ubingwa wa Msanii bora Tanzania wa vina ‘Mistari yenye jumbe nzito].
Ushindi huo aliunyakua mwaka 2004 kwenye shindano la Mfalme wa Rhymes lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers yenye maskani yake Sinza jijini Dar es salaam. lfahamike kamapuni hiyo inayomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Buchosa Mhe Erick Shigongo inachapicha magazeti Pendwa ya Uwazi, Aman. Risasi. ljumaa. Champion na ljumaawikienda ambayo Mwandishi wa habari hizi alikuwa anayatumikia.
Simba huyo wa Morogoro alitwaa ubingwa huo kwenye Shindani hilo lililofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar na kukabidhiwa gari la kisasa ambalo milango yake inafunguka kama ile ya ndege.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo ukumbini hapo, alishuhudia wimbo wa Darubini kali wa Afande Sele wenye mistari yenye ujumbe mzito ulifunika nyimbo za wasanii wengine wa kongwe kama vile Juma Nature kutoka TMK, Dudu Baya, Profesa J. Madojo na Domo Kaya kutoka Arusha’A Town. Mr Nice. Mr Bluu.na Feruz
NGOJA NIKUONJESHE KIDOGO BAADHI YA MISTARI YA RISONG HILO LA DARUBINI KALI.
‘’ Ni Mimi msanii x2 wa Darubini kali.wa Darubini kali. .
Afande nashangaa unaipendaje pepo wakati Unaogoa Kifo? Kitikio. Nashangaa.
Kunatofauti gani kati ya mtu nayeishi Upanga na anayeishi Manzese? Kwani anayeishi Upanga akifa haozi? Afande nashangaa……….]
Watu wengi wanaweza kujiuliza kwa nini Seleman Msindi anajiita Afande Sele?
Jibu kwa wasiofahamu ni kwamba.
Seleman Msindi awari alikuwa Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzani ‘JWTZ’ baadae aliacha kazi hiyo ya jeshi na kutimkia kwenye sanaa, akiendelea na jina hilo la Afande Sele.
No comments:
Post a Comment