Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, April 15, 2024

NUSU FAINALI LIGI YA MABIBWA WA MIKOA, WANYONGE WA YANGA WAIBUKIA KWA MORO KIDS.

Kikosi cha Moro Kids kilichouwakilisha Mkoa wa Morogoro kwenye Ligi hiyo ya Mabigwa wa Mikoa.

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

WANYONGE wa Yanga Hausung Fc ya Njombe, nao jana wamempata mnyonge wao baada ya kuibugiza Moro Kids ya Morogoro mabao 3-0  kwenye mchezo wa Nusu fainali ya Ligi ya Mabigwa wa Mikoa iliyopigwa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

lkumbukwe Februal 3 Mwaka huu Hausung ikiwa timu pekee kutoka daraja la tatu kutinga hatua ya 32 bora ya michuano Mikubwa ya Kombe la Shirikisho ’FA CUP’ilipangwa kucheza na mabingwa wa kihistoriam Yanga.

Katika hatua hiyo ya 32 bora Walima Maparachichi hao walikutana na Yanga kwenye Uwanja wa Chamazi  nje kidogo ya jiji la Dar licha ya kutoa upinzani mkali kwa Yanga mwisho wa siku Hausung walipokea kichapa cha bao 5-1 na kutupwa nje ya michuano hiyo.

Baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo ya F.A Hausung walielekeza nguvu zao kwenye ligi  ya mabingwa wa Mikoa na juhuza zao hizo zilizaa matunda.

Hausung  wakiongozwa na kundi la wabunge wa Mkoa wa Njombe jana walifanikuwa kuifunga timu ngumu ya Moro Kids kwa bao 3-0 na kufanikiwa kupanda daraja la Pili sambamba na kutinga fainali ya michuano hiyo ya Mabingwa wa Mikoa.

Kwa upande wa wawakilishi  wa Mkoa wa Morogoro, Moro Kids waliokufa kiume wanarejeja nyumbani  kusubiri mchezo wa Play Off dhidi ya timu ya  daraja la Pili iliyofanya vibaya kwenye ligi hiyo.

Watacheza nayo michezo miwili mmoja nyumbani na mwingine ugenini,Vijana hao wa Moro Kids wakifanikiwa kuitoa timu hiyo kwenye matokeo ya jumla basi watapata tiketi ya kupanda daraja la Pili na kama wakishindwa kuitoa timu hiyo basi Msimu ujao wataanza Moja kwa moja kucheza ligi daraja la tatu hatua za awari kwenye mkoa wake wa Morogoro kusaka ubingwa wa Mkoa utakaompa tiketi nyingine ya kushiriki tena ligi ya mabigwa wa mikoa.

Hivyo wana Morogoro tuendelee kuisapoti na kuwaombea kwa Mungu wawakilishi hao wa Mji kasoro bahari kufanya vizuri kwenye mchezo wake huo wa Play Off.

 Kama kawaida panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mwandishi wa habari hizi kama madau wa Soka Mkoa wa Morogoro kupitia mtandao huu atawajuza matokeo yote ya Moro Kids kwenye mchezo huo wa Play Off kama alivyofanya kwenye Ligi hiyo ya Mabingwa wa Mikoa kwa kuripoti matokeo yote ya timu yetu ya mkoa wa Morogoro.

                    



 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...