Msimamo wa makundi hayo kabla ya gemu zao za mwisho.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Moro Kids ‘Wana wa pakaya’ kutoka Mji Kasoto Bahari Morogoro] leo saa 8 mchana huu wanacheza mchezo wa Nusu fainali za ligi ya mabigwa wa Mikoa dhidi ya Hausung Fc ya Njombe kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Vijana hao wa Moro Kids kutoka Taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji mkoa wa Morogoro inayotajwa kuongoza nchini kutoa wachezaji wengi wanao ng’ara timu mbali mbali za Ligi Kuu zikiwemo timu kubwa za Simba, Yanga na Azam.
Wakifanikiwa kushinda kwenye mchezo wa leo moja kwa Moja wanapanda Ligi daraja la Pili, ikitokea kwa bahari mbaya wakifungwa watabeba mabegi yao na kupanda basi la Shabiby Line na kurejea nyumbani Milima ya Uluguru Vijiji vya Kinole, Mkuyuni,Kiloka Matombo, Mgeta, Nyandila, Dumila.Turiani Gairo.Kisaki.Mvua.Mikese Ngerengere, Kizuka na Bwawani .
Kuwasaidia wazazi wao kuchimba Magimbi na Mihogo huku wakisubiri kujiuliza kwa mara ya pili kwenye mchezo wa Play Off dhdi ya timu zilizofanya vibaya Ligi daraja la Pili.
Nusu fainali ya pili itapigwa leo hii saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo wa Jamhuri kati ya wenyeji Gunnes Fc ya Dodoma wakipepeta na Arusha City macharii kutoka Jijini la kitalii la Arusha. [A-Town]
Ifahamike timu 4 zilizoshika nafasi mbili za juu kwenye kundi A na B zimetinga hatua hiyo ya 4 bora.
Timu hizo ni Gunnes na Moro Kids kutoka kundi A na Hausung na Arusha City kutoka kundi B.
Kila lenye kheri kwa Wana wa Pakaya Moro Kids kwenye mchezo wa leo dhidi ya walima Maparachichi hao kutoka Mkoa wa Njombe unaoongozwa na Mkuu wa Mkoa Rafiki yangu Anthony Mtaka.
Kama kawaida matokeo ya Michezo hiyo miwli ya Musu fainali itaruka hewani kwenye mtandao huu hivyo uchekae mbali na Mtandao Pendwa wa Shekidele.
No comments:
Post a Comment