Mwenyekiti Kiuno akihojiwa na Mtandao huu.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
JUZI Mtandao huu uliripoti sehemu ya kwanza ya stori ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, Kassim Ramadhan Lukinga Maarufu Kiuno, kudaiwa kumiliki mapembe ya kichawi kwenye nyumba anayoishi.
Kwenye stori hiyo ambayo iko hapo chini kwenye mtandao huu maelezo ya wahusika wa pande zote mbili yaliwekwa kiporo kutokana na urefu was tori hii.
Hivyo leo tunaikamilisha kwa kusikia maelezo ya Mwenyekiti Kiuno na Hamad Mohamed ambaye ni shemeji wa Mwenyekiti huyo aliyemuoa Fatuma Ramadhan Lukinga.
HUYU HAPA MWENYEKIKITI.
Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo April 3 siku iliyofuta April 4 Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mwenyekiti huyo kwa hudi na uvumba kwa lengo la kusikia kauli yake juu ya madai hayo nzito akituhumiwa kumiliki mapembe ya kichawi.
Siku hizo Mtandao huu ulifika nyumbani kwake haukufanikiwa kumpata Mwandishi alitinga kwenye ofisi yake ya kuuza Kahawa na tangawizi pia hakuweo Mjukuu wake aliyekabidhi ofisi hiyo ya kahawa alipoulizwa alisema.
‘’Kutokana na sekeseke la jana babu hajatulia hapa ofisini ila ukitaka kumpata jioni huwa anafuturu pale kwenye hotel ya Mama bonge stend ya daladala ya Mji Mpya”alisema kijana huyo.
Muda wa kufuturu ulipofika Mwanahabari huyo alitinga kwenye Mgahawa huo na kumshuhudia Mzee Kiuno akifuturu.
Kistaarabu Mwandishi alisuburi amalize kufuturu, alipomaliza alimvuta pembeni na kufanya naye mahojiano ambayo yalikuwa hivi.
Mwandishi.Mwenyekiti Shikamoo na pole na majanga yaliyokukuta jana.
Mzee Kiuno. Marahaba na asante shekidele.hapa duniani tuna maadui wengi wengine hawatoki mbali ni watu wako wa karibu.
Mwandishi. Ok kwa faida ya wasomaji wa Mtandao wa Shekidele tunaomba utueleze tukio zima na jinsi ulivyolikabiri.
Mzee Kiuno. Sawa naamini kupitia wewe Mwandishi wa habari nakanusha vikali tukio hilo kwamba mimi sihusiki na mambo hayo.
Iko hivi ile nyumba tunayoishi ni ya urithi baba na mama wamekufa siku nyingi na ndugu zetu wengine wamekufa tumebaki wawili mimi na dada yangu Mama Rama.
Miaka ya nyuma kwa wema kabisa nilimshauri dada yangu kwamba sisi umri umeenda muda wowote tunafariki hivyo ili tusilete mtafaruku kwa wa watoto wetu kugombe hii nyumba bora tuiuze tukiwa hai tugawane pesa kila mtu na wanae akajenge nyumba yao dada amekataa basi nimekaa kimya.
Kwa muda mrefu dada yangu anaumwa chaajabu wameenda kuleta Mganga kaingia kwenye nyumba bila kibali chochote cha kufanya kazi hiyo kwenye mtaa wangu na ndani ya nyumba yangu.
Siku ya kwanza kajifanya kutoa pembe nikaulizwa nikawaambia hii nyumba sio yangu ni ya marehemu baba na tuliobaki ni mimi na dada yangu hivyo tulizwe sote kwa nini nisukumiwa mimi ili hali nyumba sio yangu”?.
Alisema Mwenyekiti kiuno kwa sauti ya ukali na kuendele kufunguka
’’Chaajabu Yule mganga kanifuta kanivuta kando kaniambia nimpe elfu 30 ili kesho asije kuendelea na kazi ya kutoa Ungo nikamkatalia nikamwambia hivyo vitu sio vyangu siwezi kutoa hiyo pesa.
Kaondoka zake jana kaludi mara zote anakuja saa 3 usiku alipofika kawaambia watu wazime taa zate za nyumba kukawa giza totolo ndio kaanza kufanya kazi yake, huyo sio uongo, kama ni mganga kweli kwanini asije mchana anakuja usiku na kuamuru taa kuzimwa?.
Wakati akijianda kutoa huo Ungo Polisi wamefika alipoliona gari la polisi katimua mbia kaacha tungulize zake mpaka sasa ziko pale nyumbani.
Baadae polisi wakawakamata waliomleta huyo Mganga ambao ni shemeji yangu baba Rama na binti yake, jana nilienda polisi kuwatoa’’alimalizia kusema Mzee Kiuno ambaye ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo kwa miaka 30 mfurulizo toka mwaka 1994 mpaka mwaka huu 2024.
HUYU HAPA BABA RAMA.
April 5 Mwandishi wa habari hizi alitinga ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kuzungumza na Hamad Mohamed’Baba Rama’ ambaye ni Mume wa Fatuma Ramadhan Lukinga dada wa damu wa Mwenyekiti Kassim Ramadhan Lukinga.
Baba Rama alipotakiwa kuelezea tukio hilo alisema ” Mpendwa mke wangu Mama Rama miaka mingi yuko kitandani Mgonjwa,kapararaizi tumehangaika huku na kule bila mafanikio sasa March 30 familia yote akiwemo shemeji Kiuno tulikaa kikao kwa kauli moja tukakubaliana kumtafuta Mganga aje hapa nyumbani kumtibia mkewe wangu.
Mganga kaja juzi kabla ya kumtibia mgonjwa kasema nyumba hii ni chafu hivyo aliomba ridhaa ya kuisafisha kwanza nyumba ndio amtibie mgongwa.
Chaajabu Shemeji Kiuno kakataa tukamuamulu mganga afanya kazi yake ndio katoa pembe pale mlangoni, kaondoka akiahidi kurejea tena kuja hapa kuendelea na kazi kutoa Ungo”alisema baba Rama na kuongeza. Alipoludi mara ya pili wakati akiendelea na kazi Shemeji Kiuno kaita polisi, mganga kakimbia nikakamatwa mimi na huyu binti yangu Famia.
Watu wenye mapenzi Mema waliojaa huruma wanaojua kwamba bint yangu ndiye anayemuhudumia mama yake kwa kumpikia na kumuogesha na mimi ndio baba wa familia ninayetafuta riziki mgonjwa ale.
Sasa sote tukiwa Mahabusu kwa muda mrefu nani atakaye fanya hayo kwa huyu mgonjwa?Watu wenye mapenzi mema wamekuja kutudhamini tukatoka mahabusu’’.amesema Mzee Hamad
Alipoulizwa kwamba Mwenyekiti kiuno alipohojiwa amesema yenye ndiye aliyewadhamani, baba Rama alishanga kisha akasema.
“Muongo huyo shekidele unatakiwa kujiongeza yeye ndiye aliyeita polisi wakatukamata na kusweka ndani iweje yeye tena aje kutudhamini”
Alipoulizwa wameshitakiwa kwa kosa gani?
Baba Rama alisema” Tumeshitakiwa kwa kosa la Udharirishaji”.
Wahusika wote wakati wanahojiwa na Mwandishi wa habari hizi walikuwa wakirekodiwa na kifaa maalumu.
No comments:
Post a Comment