Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, April 11, 2024

FAINALI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA.MORO KIDS LEO NI KUFA AU KUPONA

                Msimamo wa ligi hiyo kwa makundi yote mawili.

 
     Mabalozi wa Mkoa wa Morogoro vijana wa Moro Kids.
 

.
                   Na Dustan Shjekidele,Morogoro. 
 
WAWAKILISHI wa Mkoa wa Morogoro kwenye michuano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa Moro Kids leo ni kufa au kupona. 
 
Ligi hiyo inayopigwa uwanja wa Jamhuri Dodoma inafikia tamati leo kwa Moro Kids yeye alama Moja kukipiga na Bukombe Combine ya Geita yenye alama 3.
 
Huku vinara wa kundi A wenyeji Gunnes Fc ya Dododa wakiongoza kundi baada ya kujikusanyia alama 4 ambao watamaliza kwa kucheza na Eagle Sc ya Dar es salaam yenye alama 3. 
 
Kwa msimamo huo yoyote atakaye shinda kwenye gemu yake ya Mwisho inatinga hatua ya 4. 
 
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu kutoka Dodoma Afisa habari wa Moro Kids Josse Mkoko alisema gemu ya kwanza iliyokuwa na changamoto nyingi walifunga bao 2 - 1 na Eagle na gemu ya pili walitoka sare ya bao 1 -1 na wenyeji Gunnes.
Alipotakiwa kielezea changamoto hizo Mkoko alisema.
 
“Kama unavyojua shekidele uchumi wa timu zetu siku ya mchezo ndio tumefika Dodoma asubuhun siku ya mchezo.
 
Tulipofika vikao vya Bunge vinaendelea hapa Dodoma hivyo wageni ni wengi tumetafuta gest tumefakiwa kupata saa 6 mchana na nag emu yetu saa 8 mchana hivyo wachezaji waliingia uwanjani wakiwa wamechoka tukafungwa 2-1 na Eagle” amesema Afisa habari huyo ambaye pia ni mtangazaji mahiri wa kipindi cha Michezo cha Dizim Fm ya Mkoani hapa. 
 
Mtandao huu inaiombe kila lenye kheri wawakilishi hao wa Mkoa wa Morogoro kwenye gemu yao ya leo waweze kuibuka na ushindi na kusonga mbele. 
 
Baada ya gemu za leo Mtandao huu utawajuza matokeo za michezo yote na timu 4 zilizofanikiwa kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...