.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona ya Filahunim msemo huo umetimia juzi usiku baada ya Mganga wa kienyeji aliyekuwa akitoa Mapembe ya kichawi kwenye nyumba anayoishi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kutimua mbio n baada ya Polisi kutinga eneo la tukio.
Tukio hilo ambalo kwa sasa ndio gumzo katika Mitaa mbali mbali ya Mji wa Morogoro limetokea juzi usiku wa April 3 kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kassim Ramadhan Lukinga Maarufu Kiuno.anayetuhumiwa na ndugu zake kumiliki uchawi huo.
Awari April 1 Majira ya usiku wananchi kibao akiwemo Jamillah Ngurungu na Maskuzi walimpigia simu Mwandishi wa habari hizi na kumrambisha ubuyu wakisema.
“Shekidele njoo haraka uchukue habari Mganga anatoa Mapembe nyumbani kwa Mwenyekiti wetu Kiuno” alisema Jamillan anayeishi nyumba inayotazamana na hiyo ya Mwenyekiti.
Baada ya dakika 5 Mwananchi mwingine Bw Maskuzi naye alimtwagia Simu Mwanahabari huyo na kumueleza.
“Shekidele Njoo fasta hapa kwa kiuno watu wamejaa usiku huu wakishuhudia Mganga akitoa Mapembe kwenye nyumba ya Mwenyekiti Kiuno, muda huu anatoa bonge la pembe”alisema Maskuzi anayeishi kota za Paju zilizopo Mtaa wa Makaburi ‘B’.
Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa Kihonda kwenye majukumu mengi ya kikazi muda huo wa saa 3 usiku alipiga gia pikipiki yake hadi kwenye mtaa huo uliopo kata ya Mji Mpya mkoani hapa.
Kufuatia umbali Mrefu wa kutoka Kihonda mpaka Mji mpya alikuta tayari Mganga huyo ameshafanya yake nakuondoka zake.
Baadhi ya wananchi walikutwa eneo la tukio waliokuwa wakilijadi tukio hilo walisema.
“Mwandishi umechelewa kidogo tu Mganga kaondoka sasa hivi, Pembe tumelichoma Moto, tulitumia kuni likagoma kuwaka tumetafuta taili na gari tukamwagia Petrol ndio hilo hapo limeungua yamebaki majivu” alisema Mwajuma lssa.
Mashuihuda hao wameendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi wakimueleza Mwandishi kwamba wakati, Mganga huyo anahangaika kulifukua Pembe hilo lenye ncha kali lilimchoma kwenye mkoni.
“Mkono umevimba Mganga kasema baada ya leo kutoa Pembe hilo kesho April 2 saa 7 mchana atakuja kutoa Ndege[Ungo] anatumia mtuhumiwa kuluka nao nyakati za usiku hivyo kesho muda huo usiwe mbali uje kuchukua habari”. Alimalizia kusema shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Shaban lssa.
Kesho yake mapema sana Majira ya saa 6 mchana Mwandishi wa Mtandao huu alitinga kwenye Mtaa huo ulioo jirani na kituo cha Polisi akisubiri Sangoma huyo afanye yake.
Hadi saa 9 Alasiri Mganga huyo hajatokea, Mwandishi wa Mtandao huu kwa kutumia mbinu za Kishushushu alitinga jirani na nyumba hiyo ya mwenyekiti na kuzungumza na Majirani ambao walisema.
“Kweli Mganga aliahidi leo saa 7 angekuja kumaliza kazi ya kutoa ungo lakini kwa bahati mbaya wakati akitoa Pembe lile la jana lilimchoma kwenye mkono umevimba hivyo kaamua kwenda kwake Mikese kujitibia na kuongeza nguvu sasa hatujui atakuja lini tena tena”walisema Majirani hao walioomba hifadhi ya majina yao kwa kuilinda mahusiano yao na Mwenyekiti wao.
Juzi Alir 4 majira ya saa 3 usiku Mganga huyo alirejea na kwamba wakati akiendelea kusaka Ungo huo ndani ya nyumba hiyo,taarifa zilizopatika eneo la tukio zilidai Mwenyekiti huyo katoa taarifa Polisi.
Hivyo wakati Mganga huyo akiendelea na kazi hiyo ya kuisaka Air Bus hiyo ya kienyeji, Vijana hao wa IG Wambura fasta walitinga kwenye nyumba hiyo.
Mganga huyo alipoliona Difenda likipack nje alitimua mbio akitokea Mlango wa nyuma na kutelekeza vifaa vyake vya kazi zikiwemo tunguli na usinga.
lmeelezwa baada ya Mganga huyo kutimua mbio kama swala Polisi waliwakamata wanafamilia wawili walimkodi Mganga huyo na kwenda kuwasweka nyuma ya Nondo[mahabusu].
Juzi na Jana Mwandishi wa habari hizi alitinga kwenye nyumba hiyo kwa lengo la kufanya mahojiano na wahusika wa tukio hilo na kufanikiwa kuzungumza na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Makaburi A Kassim Ramadhan Lukinga[Kiuno] ambaye amethibisha tukio hilo kutokea kwenye Mtaa wake ndani ya nyumba anayoishi.
Awari Mwenyekiti huyo alihojiwa kama Rais wa Mtaa wa Makaburi A na Mlinzi wa Amani kwenye mtaa huo.
Baadae Mwenyekiti huyo alihojiwa kama mtuhumiwa wa tukio hilo ambapo amefunguza mazito akimshutumu dada yake Fatuma Ramadhan Lukinga, na Shemeji yake Hamad Mohamed mume wa Fatuma na Mtoto wao Famia kwa kumtuhumu kwa ushirikina.
Ifahamike kwa miaka Mingi Bi.Fatuma yuko kitandani anaumwa hivyo baada ya kuhangaika huku na kule bila mafanikio, Mume wa Fatuna na watoto zake kwa amoja waliamua kumwita Mganga huyo kwa lengo la kumtibu Mama yao.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zimedai Mganga huyo alipofika alisema nyumba hiyo ni chafu sana hivyo kabla ya kumtibia Mgonjwa aliomba ridhaa kwa wanafamilia kuisaifi, inadaiwa Mwenyekiti huyo aligoma mganga huyo kuisafisha nyumba hiyo.
Baada ya Mzee Hamad na bint yake Famia kutoka Mahabusu kwa dhamani jana Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuzungumza nao wakaeleza A- Z ya tukio hilo.
Mwenyekiti Kiuno naye alihojiwa kwa mara ya Pili kama mtajwa kwenye sekeseke hilo la kilosi naye kafunguka mazito.
Stori hii itaendelea baadae kwa Kassimu Ramadhan Lukinga Kiuno na Hamad MohamedMume wa Fatuma Ramadhan Lukinga] kuelezea kilichotokea na kinachoendelea kwenye familia hiyo.
Hivyo usikae mbali na Mtanda huu kwa hahari za chini ya Kapeti
No comments:
Post a Comment